Maridhiano ya CCM na CHADEMA Ndiyo Kawaida ya Vyama vya Siasa Duniani Ilivyo?

Hata utawala wa makaburu Africa Kusini uliisha kwa mazungumzo na maridhiano, CCM hata hawajafikia kiwango cha makaburu. Mandela na ANC walikaa mezani na makaburu, hiyo kwa wengine walitafsiri ni kuungana.
Nilijuwa huko kichwani kuna kitu.

Lakini, huoni mwisho wa siku ANC walishika hatamu?
Yale maridhiano hayakuwa ya ANC kujisalimisha kwa makaburu kwa njia yoyote ile.
 
Vyama vya siasa vikimalizwa kwa siasa za mazungumzo na maridhiano ni sawa kabisa na hiyo ni sehemu ya demokrasia, ila sio kwa hofu na vitisho vya risasi, utekaji, unyang'anyi na njia nyingine haramu za binadamu wasiostaarabika.
Hapana, hili sikubaliani nawe.

Vyama vya siasa kiuhalisia vinakuwepo, kwa sababu ya kuwepo na tofauti zao katika mambo wanayoyaamini.
Kuvimaliza, hata kama ni kwa njia ya mazungumzo, maana yake ni kwamba havikuwa na zaidi walichokisimamia kama vyama, bali vilikuwepo kwa maslahi tu, ambayo sasa yatapatikana kwa njia za maridhiano.
 
Mkuu Nkanini jibu swali ,Mimi Sina chama Cha siasa ,,lakini je hayo yanayofanywa na mwenyekiti kukutana na mwenyekiti ndio maridhiano yanavyokuwa???
 

Lakini Zanzibar hakuna utamaduni wala Mila, kuna Uislamu tu, sasa huo utamaduni wa Kitanzania unaouongelea ni upi?
 
Ninakuelewa unayosema hapa, ila sikubaliani kamwe na hitimisho lako, kwamb kazi kuu ya maridhiano ni kuondoa ukandamizaji huo, na kwa sababu hiyo ndiyo uwe sababu ya vyama vya upinzani kubwaga manyanga hata katika msisingi ya wanayoyasimamia kama vyama pinzani.

Ndiyo, ridhiana kuondoa ukandamizaji, lakini huwezi kuweka rehani misingi ya chama katika kuyaondoa hayo maovu.
 
Tanzania ina vyama vya siasa karibia 20, kikimalizwa chama kimoja au viwili vitatu bado utabakiwa na vingine vingi tu vya kuchagua kuendelea navyo. Pia nchi hii kuna urahisi sana wa kuanzisha chama cha siasa, kikimalizwa chama kimoja kuna fursa kubwa ya kuanzisha chama kingine.

Usiogope.
 
Mkuu Nkanini jibu swali ,Mimi Sina chama Cha siasa ,,lakini je hayo yanayofanywa na mwenyekiti kukutana na mwenyekiti ndio maridhiano yanavyokuwa???
Exactly mkuu, politics sio vita sisi wote ni watanzania, na pia elewa President Samia ameenda hapo kama President sio chairperson wa ccm,na vikao vyote kati ya viongozi wa CDM na President Samia vilifanyika state House SIO LUMUMBA (Kwenye centre of power),mbona President Obama alimtumia President Bush Jr kumwakilisha wakati wanatoka vyama tofauti?sasa soma hili,CIC Malema (alijitoa ANC kwa hasira kubwa)sasa amekubaliana kufanya kazi na ANC!,kumbuka fujo za EFF bungeni dhidi ya serikali ya ANC,Leo wanatawala pamoja jiji la Durban!
 
Nimekuelewa zaidi ya ulivyoeleza hapa.
Kwa hiyo sina sababu ya kufafanua zaidi.
 
Kwani tinapangiwa na watu wa Duniani?
 
Mbona Ruzuku ya CHADEMA Ina kuuma Sana?. Hiyo ni haki ya CHADEMA waitumie wapendavyo. Ruzuku inatolewa kwenda kwenye akaunti ya chama sio ya mtu binafsi.
Huyo bado ana hasira za kuachwa
 
Hebu kwanza jibu nilichokuuliza mwanzo, usijibu swali kwa kuuliza swali lingine, hiyo kwangu inaonesha hujui mantiki ya kile unachosimamia.

Naona unaendelea tu kuzungumzia mambo yasiyo na standard, unapenda sana kujadili hisia ndio maana neno sheria limekukera, nani aliesema tuwaige wazungu kila wanachofanya? una hoja nyepesi unazoziamini ni nzito, hatubanwi na yeyote kuiga kila wanachofanya wazungu- fact.

Nimetumia neno sheria kwasababu hiyo ndio standard ya kujua kama mtu/taasisi fulani imekosea au vinginevyo, sijui kwanini matumizi ya hilo neno yakukere! itakuwa ni kwasababu unajua hauna majibu ya kile ulichoulizwa.

Nakuuliza tena, hiyo asali unayolalamika Chadema wamelambishwa [ kupokea ruzuku] au kama huzungumzii ruzuku kwenye asali yako useme, ipo kisheria au haipo kisheria?

Usitake kubadili maana ya kile nilichokuuliza bila sababu, mimi sijawaambia CCM wasifuate sheria popote, sasa unaponiambia mbona wao huwa hawafuati sheria, maana yake unataka na Chadema wavunje sheria!

Unaposema nachojaribu ku-spin hakiwezekani, huo ni mtazamo wako, sikulazimishi uamini tofauti, lakini pia, nawe usilazimishe wengine waamini kile unachoamini wewe, kama umeamua kuimba "asali" bila ushahidi, endelea kuimba mapambio yako ...
 
Unaendeshwa na hisia zaidi, hauna fact, na bahati mbaya unatumia hisia zako kuhukumu jambo negatively, this is not fair.

Unaposema Mbowe ameamua kwamba kwanini ahangaike na watu wasio na shukrani, ulikaa nae wapi akakwambia haya?

Unaposema wakina Mbowe wamejinufaisha, kwa lipi baya walilofanya mpaka useme hivyo? hebu tujibu nasi tujue.

Punguza kukataa tamaa kunakosababishwa na kuamini hisia zako potofu, hoja zako zinachekesha sana.
 
Ila nyie wasomi mnashangaza sana, wapinzani walisema tunahitaji tume huru, bunge live, sijui demokrasia kama USA mnatusema kwamba tunataka kuiga wakati mazingira ni tofauti!!

Kujibu swali lako, hawahitaji kufanya maridhiano huko nje maana mtu akiangushwa anaangushwa wazi bila excuse sio kama huku rafu nyingi so Kila chaguzi ni zaidi ya vita.

So kwa context ya Africa maridhiano kibao yamefanyika, tuliona Tsvangirai Zimbabwe, Tuliona Mandela sauzi, Odinga Kenya, na Garang kule Sudan.

So kwa Afrika sio kitu kigeni
 
'Of course' hatuwezi kuwa "waigaji" siku zote, sasa niambie tuanze kuhimiza waje waige nini, kutekana, kuvunja sheria tunazotunga sisi wenyewe, n.k..?
Kumbe unajua hatuwezi kuwa waigaji siku zote, basi ulichoandika kule juu kwangu hakina maana tena, ndio maana nikakwambia huna hakika na mantiki ya hoja unayosimamia, ndio maana ukajibu swali langu kwa kuniuliza maswali yako, pale ulikuwa unanikwepa tu, lakini jibu ndio hili uliloandika hapa!.
 
Kadri navyozidi kukusoma nacheka tu, unazungumzia dalili na sio fact, halafu unahukumu kupitia hizo dalili, subiri fact ndio uhukumu, haraka na pressure za nini?

Inaonekana propaganda za lumumba zimekuingia sana, wale waliosema leo Mbowe atatangaza kuwasamehe kina Mdee, vipi wamesahewa?!

Rilaxx.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…