Maridhiano ya CCM na CHADEMA Ndiyo Kawaida ya Vyama vya Siasa Duniani Ilivyo?

Maridhiano ya CCM na CHADEMA Ndiyo Kawaida ya Vyama vya Siasa Duniani Ilivyo?

Again, ningekuwa na hela za kutoa sadaka; nisingesita hata kidogo kutoa sadaka juu ya hili jambo la Katiba Mpya 2025.
Na kwa usahihi, Katiba Mpya inastahiri kuwepo kabla ya 2024 kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Mbona una presha sana kwani katiba mpya ni sababu ya uchaguzi tu? Kuna masuala ya muungano, uwajibikaji, kubana matumizi, kupunguza majimbo n.k why unafikiria kwa angle ya "katiba Ili tuwahi chaguzi". As if katiba ni kwa ajili ya kushinda ubunge na Urais pekee. So myopic thinking
 
Na hapa ndio shida inaanza, nani kakwambia hakuna katiba mpya before 2025? Hii 2023 Bado Ina miezi 8 hapo Bado miaka 2 mingine hivi kweli tukose katiba for 2.8 years?

Tuache pessimism
Wewe jamaa kabla ya kuandika hiyo 2.8years ulifikiria uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, harakati za uchaguzi mkuu 2025 na kuvunjwa kwa bunge? Yaani muda uliopo ni mwaka huu 2023. Kuanzia 2024 kila chama kitakuwa kwenye harakati za uchaguzi na hata bunge halitaweza kupitisha hiyo bajeti ya kushughulikia katiba. Suala la katiba kwa sasa haliwezekani kabisa. CHADEMA walimpuuza sana Zitto aliyeshauri wapiganie kwanza tume huru. Nadhani kwa sasa watakuwa wamemwelewa ila muda sio rafiki tena.
 
Swala la waTanzania kuwa "waoga", siyo kweli.
Acha uongo, walimu na madaktari ni mara ngapi walikua wanaandamana alafu walainika baada ya kupigwa biti?! Hii nchi imejaa waoga hata bila kuhitaji Chadema Kuna mambo basic kma mfumuko wa bei, ukatili wa wanawake, panya road n.k uliwahi ona mtu anaandamana? Sisi ni watu wa NDIO MZEE na ndio maana watawala wanatuburuza wanavyotaka.
 
BASI IGA NA USHOGA UWAFUNDISHE NA WANAO
Heshima mkuu 'shinyangakwenu"
Katika yooote yaliyoandikwa mle, wewe wazo moja tu ndilo lililokuijia akilini kuhusu mada husika, kweli?

Na kwa bahati mbaya sana, mashoga wapo hapa kwetu, tuwe tumeiga au la.
 
Ni kwa bahati mbaya sana, CHADEMA hawajawa na ushawishi huo kwa aTanzania. S
Unapimaje ushawishi wa chama bila tume huru? Yaani tukiporwa kura majimbo yote 200+ ndio unaamini hatuna ushawishi? Niambie indicator Moja ya kukosa ushawishi! FnN-oayXwAAZiX6.jpegFnN-oayXwAAZiX6.jpeg
FnN-oayXwAAZiX6.jpeg
 
Mbona una presha sana kwani katiba mpya ni sababu ya uchaguzi tu? Kuna masuala ya muungano, uwajibikaji, kubana matumizi, kupunguza majimbo n.k why unafikiria kwa angle ya "katiba Ili tuwahi chaguzi". As if katiba ni kwa ajili ya kushinda ubunge na Urais pekee. So myopic thinking
Sijui wewe umenionaje mimi kuwa na 'pressure' ambayo wewe huna!
Sijasema popote kwamba Katiba Mpya inahusu mambo ya uchaguzi pekee, lakini ni sehemu muhimu katika maswala ya uchaguzi. Hii ndiyo sheria mama ya sheria zote.

Mkuu zitto jr, naona tutapotezeana heshima bure, heshima tuliyowekeana kwa muda mrefu sana. Kama hutaki kusoma ninayoandika juu ya jambo hili la Mbowe na CHADEMA, ondoa hiyo 'pressure' inayokupanda inayjionyesha kwenye maandishi yako.
Imekufanya nianze kukuona kama nisiowapa staha hapa jukwaani.
 
Acha uongo, walimu na madaktari ni mara ngapi walikua wanaandamana alafu walainika baada ya kupigwa biti?! Hii nchi imejaa waoga hata bila kuhitaji Chadema Kuna mambo basic kma mfumuko wa bei, ukatili wa wanawake, panya road n.k uliwahi ona mtu anaandamana? Sisi ni watu wa NDIO MZEE na ndio maana watawala wanatuburuza wanavyotaka.
Sikumbuki ni mara ngapi umeniita "mwongo" kwenye siku za hivi karibuni.
Bila shaka kuna jambo ninalojadili linalokuchoma moyo wako ndani kabisa.

CHADEMA haiaminiki kwa wananchi, hilo ndilo lingekuwa jambo la kujiuliza sana ndani ya chama.
 
Unapimaje ushawishi wa chama bila tume huru? Yaani tukiporwa kura majimbo yote 200+ ndio unaamini hatuna ushawishi? Niambie indicator Moja ya kukosa ushawishi!View attachment 2543239View attachment 2543239View attachment 2543239
Kwa hiyo, na ushawishi wote huu, kunahaja gani tena ya chama kwenda kupiga magoti mbele za CCM?

Unaweza kuniambia halaiki yote hiyo, wote ni "watu waoga"?
Kushindwa kwenu kuwashawishi waone matumaini kwenu mnaanza kuwatumia lawama wao?
 
Sikumbuki ni mara ngapi umeniita "mwongo" kwenye siku za hivi karibuni.
Bila shaka kuna jambo ninalojadili linalokuchoma moyo wako ndani kabisa
Kumradhi kama ni lugha kali lakini sipendi mis-information. Yaani una quantify vipi chama hakuna ushawishi ilihali uchaguzi wa 2015 kilipata mora than 40% ya kura zote. Na 2020 licha ya wizi kilipata zaidi ya 3 million parliamentary votes. Kwa context tu aliyefuatia alikua ACT alliyepata almost laki 2 kwa bara na visiwani!!

Yaani ACT walipata kura sawa na Sugu pekee!! Alafu mtu unadai hatuna ushawishi? Sasa unadhani CCM ndio Ina ushawishi kwa ufisadi wote iliofanya?? Au ACT ambayo huku bara hata Kuna majimbo hayajawahi kuisikia??

Fqgja2gWcAEESv8.jpeg
 
Kwa hiyo, na ushawishi wote huu, kunahaja gani tena ya chama kwenda kupiga magoti mbele za CCM?
Ushawishi bila tume huru ni kupoteza muda tu, hivi nani alikua na ushawishi zaidi ya Maalim kule zenji ila mbona hakua Rais? Kwa tume hii hata Obama aligombea kupitia Chadema Bado ataangukia pua.

So sisi hatujapiga magoti ila tulitafuta suluhu ya kisiasa mezani why ionekane ni defeat. Odinga mbona Alifanya handshake na Kenyatta? Mandela na kina De Klerk? Why kwetu ndio ionekane kusalimu amri as if tumeenda kwenye serikali ya Umoja hivi!!

Siasa sio violence ni majadiliano tu yanatisha ndio maana tuna bunge na mahakama hakuna haja ya kuingia Barabarani kama unachotaka kinapatikana kwenye mifumo rasmi.
 
Kumradhi kama ni lugha kali lakini sipendi mis-information. Yaani una quantify vipi chama hakuna ushawishi ilihali uchaguzi wa 2015 kilipata mora than 40% ya kura zote. Na 2020 licha ya wizi kilipata zaidi ya 3 million parliamentary votes. Kwa context tu aliyefuatia alikua ACT alliyepata almost laki 2 kwa bara na visiwani!!
Nilisha andika humu mara kadhaa "sina sababu yoyote ile, ya kusema uongo, au 'misinform'", sina maslahi na yeyote isipokuwa Tanzania pekee.
 
Unaweza kuniambia halaiki yote hiyo, wote ni "watu waoga"?
Ndio..... 2020 tulipoibiwa kura Kuna yeyote alijitokeza Barabarani? Na hili tatizo sio kwa wanasiasa ila hata mambo ya kijamii. Tumeibiwa mabilioni na CCM umewahi ona tunaolalamika? Umewahi ona hata TLS inafungua kesi kupinga tozo? Tuna institutions weak na wananchi weak hawana ujasiri wowote.

Hata hao team JPM walitoka povu Mitandaoni ila hata siku Moja hawatoandamana kupinga utawala wa Samia. Ni kelele tu ila hakuna anayeweza jitokeza hadharani akampinga Rais.
 
Panapo majaaliwa, na kama Samia hatagombea, labda!
Subiri uone uchaguzi wa 2025 ni kama wa 2010 yaani mama anapambania Urais kivyake ila ubunge hakuna mbeleko. Na ndio utaona Red wave ya Chadema ikisambaa kuanzia Kanda ya ziwa Hadi magogoni.
 
Nilisha andika humu mara kadhaa "sina sababu yoyote ile, ya kusema uongo, au 'misinform'", sina maslahi na yeyote isipokuwa Tanzania pekee.
Sasa why udanganye hatuna ushawishi, unadhani Rais hajui matokeo halisi ya 2020? Umeona anahangaika na demands za ACT au NCCR??

Chadema waligomea task force na Bado Samia akawasikiliza independently alafu unasema hawana ushawishi?
 
Ushawishi bila tume huru ni kupoteza muda tu, hivi nani alikua na ushawishi zaidi ya Maalim kule zenji ila mbona hakua Rais? Kwa tume hii hata Obama aligombea kupitia Chadema Bado ataangukia pua.

So sisi hatujapiga magoti ila tulitafuta suluhu ya kisiasa mezani why ionekane ni defeat. Odinga mbona Alifanya handshake na Kenyatta? Mandela na kina De Klerk? Why kwetu ndio ionekane kusalimu amri as if tumeenda kwenye serikali ya Umoja hivi!!

Siasa sio violence ni majadiliano tu yanatisha ndio maana tuna bunge na mahakama hakuna haja ya kuingia Barabarani kama unachotaka kinapatikana kwenye mifumo rasmi.
Mkuu 'zitto jr', hii mifano ulishaitoa humu, na ninarudia tena, siyo mifano inayofanana hata kidogo.
Hiyo ya Mandela, ni tofauti kabisa na hizo za akina Maalim, Odinga, Tsvangilai, sijui na wengine wapi.

Hizi mnazosaka CHADEMA na CCM ni hizo za akina Raila. Hizi ni za kuatafuta maslahi tu, kunradhi sana kwa kurudiarudia haya.
CHADEMA ilipokwishafikia haikuwa na sabau tena ya kwenda kuomba.
Ukweli ni kwamba CCM ndio walitakiwa kuanza kuomba po; na wametumia fursa mliyowapa kuwaondoa kwenye kona waliyokuwa wamejibamiza tayari!

Sasa wao ndio mmewapa udereva tena.
 
Subiri uone uchaguzi wa 2025 ni kama wa 2010 yaani mama anapambania Urais kivyake ila ubunge hakuna mbeleko. Na ndio utaona Red wave ya Chadema ikisambaa kuanzia Kanda ya ziwa Hadi magogoni.
Nilishakuelewa juu ya hili; na kusema kweli ndiyo sababu kuu inayofanya tutofautiane sana hivi karibuni.
Kumbuka, kama ni Samia, hata ubunge mtatoka jasho sana.
Ndiyo, mtapata kiasi, lakini siyo mawimbi ya wabunge kama unavyotegemea.
 
Sasa why udanganye hatuna ushawishi, unadhani Rais hajui matokeo halisi ya 2020? Umeona anahangaika na demands za ACT au NCCR??

Chadema waligomea task force na Bado Samia akawasikiliza independently alafu unasema hawana ushawishi?
Sasa mngeshikilia hapo hapo. Mngemshukuru sana kwa yote mazuri aliyofanya kurekebisha maovu mliyofanyiwa na baada ya hapo mkaendelea na safari yenu ambayo tayari ilikuwa inatokota kuifyekea mbali CCM.

Badala yake, mkageuka kuwa waokozi wa boti lililokuwa linazama.
Si maajabu hayo?

kawavuta majini, sasa ni jukumu lenu tena kujiokoa wenyewe.
 
Back
Top Bottom