Maridhiano yanahitajika haraka sana ndani ya uongozi mpya wa chadema, hali inaweza kua mbaya zaidi mbeleni hilo lisipo tiliwa maanani

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Body languages, tones na facial expressions za viongozi waandamizi wa chadema hususani wa kamati kuu, zinaonyesha kabisa bado kuna migawanyiko na uhasama ndani ya chadema.

Lakini pia jana pale Ikungi Singida tumeshuhudia kwa uwazi zaidi kwamba umoja ni changamoto ndani ya uongozi mpya wa chadema, kuaminiana kwa viongozi wapya wa chadema kuna tia mashaka sana, na nikama kuna kamgomo baridi hivi kwa baadhi ya viongozi wa kanda jirani, wilaya na mikoa jirani katika kujitolea kwenye shughuli za chama hususani kwenye kuhudhuria tukio kubwa kama la kumpokea kiongozi wa chadema taifa pale Singida.

Kuna mnyukano na kushughulikiana kimya kimya kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhujumiana au kususiana kwenye kufanikisha agenda za chama. Bilashaka kwenye uchaguzi, hii itakua fimbo muhimu ya kukomoana chadema.

Ni mwendo wa kulazimisha furaha na smile za kinafiki miongoni mwa viongozi waandamizi wa chadema. Unaona kabisa kiongozi wa chadema kashika mike anaongea but mwili uko pale but moyo unawaza kwingineko kabisa.

Ni muhimu sana hatua za makusudi za maridhiano zikachukuliwa ili kuepusha kuumizana wenyewe kwa wenyewe, kitu ambacho pia kitawaharibia na kuwarudisha nyuma wao wenyewe.

Wasione aibu kutumia falsafa ya 4Rs za Dr.Samia Suluhu Hassan zitawasaidia sana kua pamoja.Chadema kuna changamoto ya ummoja.

Una maoni gani ndugu mdau?πŸ’

Mungu Ibariki Tanzania.
 
WEWE unavichekesho sana, kama siyo mwendawazimu!!!!!!!!!!
Wewe ni CCM halafu Lumumba buku 7, uanze kuto mawaidha mazuri kwa CDM; my neck
 
Wasipokuwa na umoja si faida kwenu ccm mnapata ushindi kwa urahisi,shida nini aisee mbona Chadema haiwatoki mdomoni.
 
Acha wahujumiane tu huku sisi CCM tukiendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya mamilioni ya watanzania. Ikiwezekana wagawane chama na wanachama ili kila mtu aondoke na chake.
 
Umekuwa bwana mshauri , post ya ngapi hii? Waandikie barua
 
Hakuna ansyekusanya watu bure. Mbowe alikuwa anatoa hela. Nyie mnadanganyana eti wanakuja wenyewe. Lazima muisome namba. Na bado
 
Kuna wanaoamini hatakama No reform tukapambane hivyo hivyo.
 

Dada chawa umeingia chooniπŸ˜‚ Lissu sasa mwenyekiti na hakuna drama. Mwezi ujao tuna anza kutafuta pesa za kusaidia taifa hili. Mambo yanasonga mbele
 

Ona hili punga. Maneno mengi lakini zero content.
Ameshindwa kutoa uthibitisho au hata mfano mmoja tu wa huo upuuzi aliouandika.

Kwa mada puuzi kama hizi, hata hiyo book 7 anayolipwa, hastahili.
 
Kwani covid 19 hawajasamehewa tuu?
 
Huna hadhi ya kujadili mambo ya cdm.
Ungejikita kufanya uchawa tu huko uliko maana ndio unachoweza.
 
WEWE unavichekesho sana, kama siyo mwendawazimu!!!!!!!!!!
Wewe ni CCM halafu Lumumba buku 7, uanze kuto mawaidha mazuri kwa CDM; my neck
watakapanza kuumizana wazi wazi ndipo itadhihirika kwamba chadema inaongozwa na vibaka au matapeli.

kama mtaalamu mwandamizi wa siasa ndani ya vyama, nimetekeleza wajibu wangu na sidaiwi chochote,

jukumu ni lao sasa, vinginevyo washupaze shingo tu kwa manufaa yao na chama chao πŸ’
 
Wasipokuwa na umoja si faida kwenu ccm mnapata ushindi kwa urahisi,shida nini aisee mbona Chadema haiwatoki mdomoni.
kama mtaalamu mbobevu wa masula ya siasa za vyama nchini,

singependa watu wa chama kimoja wanaumizana kwa chuki binafsi ,

kama hakuna shida basi waendeleze uhasama tu πŸ’
 
Acha wahujumiane tu huku sisi CCM tukiendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya mamilioni ya watanzania. Ikiwezekana wagawane chama na wanachama ili kila mtu aondoke na chake.
wanaelekea huko huko,
fito zitagawanwa muda si mrefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…