Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Mkuu ngoja nikusaidie kidogo kwenye huu utata, mfano wakristo na waislamu humtambua Yesu kitofauti sana kiasi kwamba wakristo hufikia hadi kusema yule aliyeelezwa kwenye Qur'an sio Yesu ni mtu mwengine kabisa. Sasa linapokuja suala la majini napo ni hivyo hivyo, waislamu wanawaeleza majini kama viumbe ambavyo vimeumbwa na Mungu na kwamba hivyo viumbe sio malaika wala sio binaadamu ila wakristo wanawaeleza majini kuwa ni kundi tu la malaika na si kwamba ni aina tofauti ya viumbe vilivyoumbwa na Mungu.

Kwahiyo hapo kuna utofauti mkubwa, ndio maana mkristo anashangaa inawezekana vp kundi la malaika waliyoasi kusema miongoni mwao wapo wema? wakati huo huo waislamu nao wanashangaa inawezekana vp malaika kumuasi Mungu?

Kwahiyo mwisho wa siku wakristo wanawazungumzia majini kama malaika na waislamu wanawazungumzia majini kama viumbe wengine kabisa.
 
Waganga wako wengi mkuu sasa mbona hawaitwi kuwa ni mabingwa wa usomaji wa Qur'an kama Sheikh Yahya? Nitajie mganga mwengine mbali na sheikh Yahya ambaye ni mjuzi sana wa Qur'an?
Dr sure.
Nimekwambia wapo waganga ambao elimu zao ni ndogo sana kwenye utabibu.
Utabibu au Quran?
Mimi nimesema manabii feki wala sijamnyooshea kidole yeyote na sio nafasi yangu kuwapima katika hao manabii kujua yupi feki na asiye feki hilo nawaachia wenye kuamini hao manabii, labda uniambie hakunaga manabii feki manabii wote ni manabii wa kweli.
Ndio maana nimekwepa kumtaja yeyote,maana tukiwaweka kwenye mizani ya hukumu hata huyu wa waislam hatoboi,haina maana.
Uchawi umekatazwa kwenye Qur'an kwahiyo kama wachawi wanatumia Qur'an basi ni kwa imani zao ni kama tu wachawi hao hao kwa imani zao wanavyotumia maandiko ya Zaburi.
Nimetaja waganga waliosoma zaidi Quran,hii ya wachawi umereact haraka tu.
 
Majini ni malaika walioasi, ambao hapo wanatajwa kama joka na malaika zake. Pia kwenye biblia hakuna mahala utapata neno jini
Sawa kabisa ikiwa umekiri kuwa kwenye biblia hutapata neno jini, Embu nisaidie majibu ya haya maswali:-

1. Unadhani ni kwanini biblia haijawataja majini ?
2. Umejuaje kuwa huyo joka na malaika zake wanaotajwa na biblia ndio majini?
 
At least umeanza kuleta Aya na hadithi ndio maana nikasema hapo tunaenda pamoja sasa

Japo umetoa hadithi but gallow bird anasema hadithi ni porojo
Hadithi ni porojo,angalia tu muundo wake,imepokelewa kutoka kwa fulani anasema fulani alimsikia bi aisha akisema mtume alisema...huu uhuni
 
Je wanaoenda kufanyiwa uganga wa Adhana wanaitakidi kwa Allah na si kwenye Adhana na mganga mwenyewe?

Ni kweli wote wanaogangwa ni waislamu hakuna wakiristo ambao hawamuamini hata huyo Allah (S.W)?
Swali zuri..
Nadhani utakuwa unamfahamu swahaba aliyeitwa Abu Sa’id Al-Khudri (RA), Swahaba huyu anasema katika hadithi mashuhuri sana iliyopokewa na Imam Bukhari katika Sahih Bukhari, Hadithi namba 5736 katika mlango wa tiba inasema.
Kundi la Maswahaba wa Mtume ﷺ walitoka safari. Walipofika kwa watu wa kabila fulani, waliomba wageni lakini wakakataliwa. Baadaye, kiongozi wa kabila hilo aling’atwa na nyoka, wakajaribu kila tiba lakini haikufaa. Mmoja wa watu wa kabila hilo akasema: “Jaribuni kuwaendea wale wageni, huenda wana tiba.”

Walipowaendea, mmoja wa Maswahaba akasema: “Ndio, mimi nasomea (rukya), lakini kwa kuwa mlikataa kutupokea, sitamsomea hadi mtupe malipo.” Wakakubaliana kumpa kondoo. Akamsomea Suratul Fatiha mara kadhaa, na yule mgonjwa akapona mara moja kana kwamba hakuwa na tatizo.
Waliporudi kwa Mtume ﷺ na kumweleza, Mtume akasema:
“Ulijua vipi kuwa Suratul Fatiha ni rukya?”
Kisha akasema:
“Mlifanya vyema. Gawanyeni malipo, na nipeni sehemu yangu.”

Sasa lengo lakukupa hii hadithi ni kuwa ni hadithi yenye mambo mengi hasa kaika maswala ya tiba ila nitaelezea kulingana na swali lako, ..Je huyu mtu aliyesomewa surat fatha imani yake ilikuwa kwa Allah au kwa msomaji au kwa surat fatha? majibu mimi na wewe hatuna kwakuwa masuala ya imani juu ya kitu ni katika mambo ya ndani ya nafsi ambayo mtu anaweza kudhihirisha kupitia mdomo kumbe ndani ya nafsi yake ni kinyume chake.
Ndio maana siku ya hukumu atahukumu ALLAH mwenyewe.
Kufupisha maelezo chukulia mfano wa dawa za hospitali zetu hizi pale tunapokunywa imani inakuwaga wapi? Je ni kwa ALLAH au kwa doctor au kwenye dawa?
 
Hii Hadith ndio muongozo wenu wazee wa Rukya nataka tujadili hayo masharti ya Rukya tuyaone na yanavyofanyika ni sawa?

Sasa wewe wasema anaejua ni Allah na hukumu atatoa yeye siku ya mwisho ni kweli hilo hakuna anaepinga ila ukweli ni kuwa uganga wa visomo unaofanywa na masheikh wetu haukidhi vigezo na masharti kama ilivyoelekezwa ila tukisema ni shirki hamtaki

Kama hili la Adhana eti nayo ni Rukya? Kwa kuadhini kabisa tena muda sio wa sala?
 
Kabla hatujaja huko kwenye masharti ya Ruqya.. Vipi kwanza bado mtazamo wako ni kuwa kupiga adhana kwa ajili ya kufukuza mashetani ni shirki?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…