Kwa nini viongozi wa Shia wa Iran ni radical sana kuliko wa Sunni??
Wanaonekana radical kwa sababu sio wanafiki na wanaongoza kwa kufuata baadhi ya sharia za dini, hapo Gaza, Wapalestina wanashambuliwa kila siku na ni Sunni, lakini hakuna nchi ya kiarabu ambayo imeonekana kuwaunga mkono ukitoa Iran ambao ni washia. Kiujumla ukiangalia mambo mengi ya washia utaona wapo sawa licha ya mapungufu machache ambayo Kila dhehebu wanafanya. Mfano mtu yeyote anaefanya shiriki anakua kajitoa katika uislamu sasa je Sunni wangapi waonfanya shiriki lkn Bado wanaitwa waislamu.
Washia wanajua haki zao nawako vizuri kwa elimu Dunia na hata dini wanaijua vizuri. Nchi yeyote itakayofuata kuongoza kwa kutumia Sharia za dini basi lazima ionekane radical.
Wanaosema sio waislamu wanasema kuwa wanawakashifu maswahaba baadhi wa mtu, na kingine wanasema kua eti wanamkashifu bi Aisha na kumtukana. Kingine wanasema pia eti wanasema Mtume hakutakiwa kuwa Muhammad bali Alli na kingine eti waliiba jiwe la Kaaba kwa miaka 22 wakalihamishia Iran.
Vitu vingi ni uzushi mtupu, hao hao washia wamewagawayika kwenye takribani makundi manne, Kuna wengine wanasema eti hawaendi kuhiji maka. Hali yakuwa kuhiji maka sio lazima kama huna uwezo na hata washia wenye uwezo wakienda maka wanatengwa sehemu yao na Serikal ya Saudia.
General issue ya shia na Sunni ni issue imekaa kisiasa baada Ayatollah wa sasa alivyorudi kutoka ufaransa na kuchukua nchi aliaahidi mambo makini mawili ambayo ni
1. Kuifuta Israel
2. Kufuta uongozi (viongozi ) wa Sunni hasa hasa falme ya Saudia, kwahio nchi zenye viongozi walioko madarakan wa Sunni kama Saudia wanalipa watu wajifanye ni washia huku wakimkashifu bi Aisha pamoja na maswahiba baadhi wa Mtume.