Masikini wasipewe vibali kujenga mjini. Huchafua miji na vijumba vyao

Masikini wasipewe vibali kujenga mjini. Huchafua miji na vijumba vyao

Kama nimekuelewa Hivi Mkuu
Umeandika fact ila Kwa sababu ya masikini hua hatukubali ukweli mchungu na tuna roho mbaya
Ngoja nikoment kimasikini Zaidi hapo chini

Acha kujiona bwege wewe u anajiona una akili Sana mtoa mada ulitaka tuishi wapi na tulishawahi kuja kukuomba Hela ya kula?

(In Masikini wa akili voices)


😄😄😄😄😄

Nipigeni mniue ukweli nishausema
 
Nakubaliana na wewe by 100%. Masikini pia wasiruhusiwe kuzaa, wahasiwe maana tutaendeleza ile kitu wanaita viscious cycle ie masikini kuzaa masikini na huyo masikini kuzaa masikini mpaka kijiji kinajaa masikini tupu. I am also poor, let us be pushed outside the town and live wherever befits us , not in civilised societies


😄😄😄😄

Acha wazae ili tupate vibarua katika viwanda vyetu. Ndivyo matajiri wanavyotuwazia hivyo
 
Mungu akiwa upande wako huwa tunajawa viburi, majivuno na kejeli za kila aini. Amini amini nakwambia Mungu akigeuza shingo na asikutazame tena, huwa nimajuto yasio na ukomo.

Hekima, busara na utu ndio Jambo jema kuliko pesa.


Mimi sina pesa Mkuu ninaye Mungu.

Hekima, busara na utu ni pamoja na kusema ukweli na haki.

Sisi masikini Kwa kweli hatustahili kujenga nyumba mjini zitakuwa ni takataka tuu
 
Kuna kitu kinaitwa mixed economy, masikini na matajiri wanategemeana. Capitalists waliliona hili, huwa wanajenga apartments katikati ya mji na kuweka flats chache wanaziita affordable flats kwa wasio na uwezo.

Tajiri anatengeneza biashara na masikini anategemea ajira katika biashara hizo..
Mtaongea yote ila ukweli Utabaki pale pale sisi masikini maeneo yetu ndio changanyikeni Nyumba hazina parking. Ukipita unatokea chooni kwa watu.
 
Naomba ufafanuzi kama kuna tofauti kati ya Masikini na Wenye kipato cha chini/kidogo.

Maana kuna hata zile flats zikijengwa kwa ajili ya Kada fulani ya Serikalini baada ya muda zile flats huwa kama stoo za Mkaa...tofauti kabisa na zile flats zinazojengwa na kupangishiwa Wanaolipa 1m kwa mwezi.
 
Umekosea kumtaja Mungu na uhusiano uliopo baina ya maskini na matajiri.je umesahau kwamba yeye aliwachagua masikini wa dunia hii kuwa matajiri wa imani.na Imani ndo kila kitu..maskini Ana mchango wake kwenye maendeleo ya mji husika halafu Huu Ushauri uwe kwenye majiji makubwa na sio tawala zetu hizi za mikoa
Andiko zuri Kiasi chake nali rate 3 star
 
Umeongea ukweli kabisa..majiji yote tanzania serikali ichukue ardhi..kisha ijenge magorofa katika mpango mzuri wa mji..na kuyapangisha..yeyote atakaye taka kuja mjini haruhusiwi kujenga bali kuja kupanga..hapa serikali itapata pesa maisha yake yote.

#MaendeleoHayanaChama
Serikali ipi? Hii ya NSSF ya kujenga nyumba za vyumba viwili kwa 25M na kutaka kuwauzia masikini kwa 45M?
 
Habari Wakuu!

Kama kichwa kinavyoeleza hapo, ingawaje Masikini naye mtu japokuwa hana kitu lakini hatuwezi kuukataa ukweli kuwa Masikini ndio mashetani yanayoishi na kuonekana live kwa macho yetu wenyewe.

Kuna watu hapa watasema nawasema vibaya MASIKINI, wengine watasema najisikia, nawadharau na kuwatolea maneno makali hao Masikini. Lakini nataka kusema hapa mimi mwenyewe ni masikini, hivi mambo niyasemayo hapa yananihusu hata Mimi.
Sisi masikini ni mashetani tunaoishi live katika macho ya nyama.

Tatizo la miji kuwa michafu, na watu kujenga pasipo mpangilio linasababishwa na Masikini. Unajua masikini ni mashetani hivyo hawanaga mipangilio, wapo rafu wanajenga hovyo hovyo.

Kama ingekuwa amri yangu, masikini leo hii wasingepewa ruhusa/kibali kujenga kwenye miji na majiji makubwa. Wakaishi huko porini huko kwenye mashamba wakalime.

Serikali kama inataka miji ijengwe kwa mpangilio mzuri basi lazima litolewe tamko kuwa Masikini hawatapewa kibali cha kujenga mijini, na mtu yeyote anayetaka kujenga nyumba mjini anapaswa awe na kiasi cha pesa kisichopungua milioni 50.

Masikini wawekewe sheria kali zitakazowabana ili wasilete ushetani wao Duniani.

Kama wanataka kuishi mjini basi serikali ijenge nyumba za kupanga, au mashirika na makampuni ndio yafanye kazi hiyo kujenga Apartments ili hao masikini wapange.

Matajiri sina neno nao, nafahamu wao wanamuwakilisha Mungu kwani Mungu ni tajiri, ndio maana matajiri hujenga na kuweka mambo/vitu vyao katika mpangilio mzuri.

Miji yote iliyotekwa na masikini lazima iwe michafu inayonuka, vijumba vimejengwa hovyo hovyo Kama takataka.

Masikini wajengewe miji Yao huko nje kabisa ya miji au maporini huko wakae wenyewe, au Kama wanataka kuishi mjini basi wapangishe nyumba zilizojengwa na serikali au matajiri.

Sitaki kuzungumzua habari ya machinga jinsi wanavyovuruga miji na kusababisha uchafu wakaapo barabarani.

Niishie hapa Masikini wenzangu wasije nipiga mawe, najua wataniona lakini ukweli nimewapa, wengine watanichukia lakini hilo halinipi shida kwani mashetani ni kawaida Yao kuwa na chuki.

Mashetani yakikupenda jua ni Kwa unafiki na yanakitu yanakihitaji kutoka kwako.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dodoma
Kama kuna masikini, basi ni hiyo serikali unayotaka iwahamishe wananchi, tena masikini wa fikra.
Ukisema wasiruhusiwe kujenga, kwangu ina maana wana ardhi. Sasa mwenye ardhi ni masikini kweli?
Hiyo serikali na taasisi za kifedha, kwa kutumia ardhi kama dhamana, ingeratibu mpango wa kuwakopesha raia wake, liporomoshwe jengo la hadhi unayotaka ili isionekane ni takataka, sehemu ya jengo ikapangishwa na kurejesha mkopo na sehemu ikawa makazi ya mwenye ardhi, kila mtu angeyafurahia maisha haya.
 
Back
Top Bottom