Hebu kwanza: Hivi hili swala la kuiondoa bandari ya Zanzibar kutokuwemo kwenye maswala ya Muungano, lilijadiliwa na kupitishwa Bungeni?Mnakubaliana chumbani? Mnaliondoa kwa siri? Au waliliondoa baada ya kuwa na wazo la kuuza za Watanganyika? Kuna kitu mbaya kitakuja, sidhani kama watanganyika watakubali hili kutendeka kwao......
Au ni ule utaratibu tu wa kushughulikia "kero za muungano' ndio uliotumika?
Mwenye kujua hili tafadhali alieleze hapa vizuri nasi tuelewe utaratibu uliofuatwa hadi bandari ya Zanzibar likawa siyo swala la muungano.
Kuna mambo mengi yamefanyika kienyeji enyeji tu, huko Zanzibar wanajiamlia kufanya mambo ambayo hawana mamlaka nayo.