Maswali ya kuudhi - Umeoa? Umeolewa? Unao/olewa lini? Una watoto wangapi?

Umeolewa?

Nikikuuliza hivyo labda ni vile nataka nijue status yako kabla nikupige sound nisije kutongoza mke wa mtu.
 
Kwani huu utamaduni wa kusubiri posa kwa waafrika umetoka wapi ? Tamaduni nyingine za ajabu sana, lakini swali lingine ukiwa unasubiria hiyo posa una kuwa unachachua au huchachui ? Kama jibu ni la kipengele cha kwanza basi kazi unayo.

Lakini, pili kwani kuna ubaya gani ukiulizwa maswali hayo kwamba umeoa au umeolewa au una wake wangapi au watoto wangapi ? Kuoa mbona jambo zuri sana na kuwa na watoto kadhalika kinyume cha viwili hivyo ni makadadirio tu kisha subira ifate.

Nipo ....
 
Dunia inabadilika....watu hatutaki kubadilika....bado tunafrika za kitambo.[emoji6][emoji854]
Dunia inabadilikaje mintarafu jambo hili na fikra za kitambo zilikuwaje dhidi ya hizi za sasa ?
 
Transparency ni nzuri ndio.

Ila hiyo transparency ni kwa nani?
Hivi Mama D nikikuuliza jina lako nani, hilo si jambo personal!??? Halafu, kama hufeel kuulizwa kitu by then, unasema tu ^pass^ kama zile brain challenges. Inaeleweka. Maswali utaulizwa tu, utake usitake. Ndiyo nature ya mwanadamu, no way.
 
Ukizaa hivyo wanavyoshauri kibao kinabadilika unaitwa msimbe umejizalia bila ndoa[emoji3]

Binadamu ni kiumbe mtata sana
 
Acheni kudanga oleweni muone kama hayo maswali yanaudhi.mbona ya kawaida sana....? Sasa ndoa ni ya kuficha nayo.....? Acheni umalaya tulieni na ndoa zenu
 
Una wake na watoto wangapi Jurjani?
 
Ni Maswali ambayo sijawahi uliza, maswali yangu ni; Unajishughulisha na nini? Umejenga? Nyumba ngapi? Ushanunua usafiri?
 
tumeachana na mke swali linalofatia hapo ni kuulizwa watoto wako wapi??!!wako na wewe au na mamaake?!
 
Ni Maswali ambayo sijawahi uliza, maswali yangu ni; Unajishughulisha na nini? Umejenga? Nyumba ngapi? Ushanunua usafiri?
Sasa hayo maswali ni magumu kuliko hata ya familia.
 
Sasa hayo maswali ni magumu kuliko hata ya familia.

[emoji23][emoji1], basi ndo maswali yangu, sijawahi kuuliza kuhusu ndoa ama watoto.Hasa hili la unajishughulisha na nini? Hata tukipotezana kwa miaka tukikutana ndo swali la kwanza.
 
Pole sana. Huwa hatuulizi kwa nia mbaya bali ni kwa nia njema tu. Kwa sababu huenda anayekuuliza hivyo unakuta amependa /amevutiwa na wewe. Hivyo unakuta anatamani uwe mtu wake so ni lazima aulize ili ajue hali yako ya mahusiano na hali za uzao wako. Akishajua kwamba jimbo liko wazi basi atapambana ili uwe wake.
Sikia Mama D katika maisha haya ya hapa Duniani huwezi mpata mwenye vigezo vyote kama unavyohitaji iwe kwa asilimia 100 kwa sababu sisi ni binadamu hivyo hatujakamilika. Hivyo hata ukimpata mwenye vigezo vyote kuna sehemu tu atakuwa anapwaya. Tupunguze standards nyingi.
 
Acheni kudanga oleweni muone kama hayo maswali yanaudhi.mbona ya kawaida sana....? Sasa ndoa ni ya kuficha nayo.....? Acheni umalaya tulieni na ndoa zenu
Anayedanga ni nani?
 
Kuna hili la "Tafuta mwanaume wa maana akuoe" linachosha sana. kwenye jamii zetu mtu usopoolewa/ usipozaa mtihani sana
 
Hii inanihusu
Sijui wanafikiri sisi tunapenda hii hali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…