Matokeo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 24, 2019: CCM yashinda kwa 99.9%, CHADEMA wapata Kijiji kimoja na Vitongoji 19, CUF nao Kijiji

Matokeo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 24, 2019: CCM yashinda kwa 99.9%, CHADEMA wapata Kijiji kimoja na Vitongoji 19, CUF nao Kijiji

CCM mmesimikwa kidikteta. Kila mtu anajua hamkuchaguliwa kihalali. Rais Magufuli anawagombanisha na wananchi wenu. Na nyie viongozi mlioteuliwa na kusimikwa kidikteta, nyumba mtakazolala zitakosa amani. Mtashindwa hata kuwaeleza jambo lolote wananchi. Labda mjiuzulu mapema kabla hamjaionja shubiri ya nguvu ya uma
 
Wamejitoa harafu wanakwenda kuangalia matokeo ,huu ni ujinga walijitoa harafu wanataka wapate 50% ujinga wa wapi

State agent
 
1574726045191.jpeg
 
Huo ndiyo unaitwa usanii wa hali ya juu..........

Eti Waziri wa TAMISEMI anadiriki kutangaza kuwa Chadema imeshinda Mwenyekiti mmoja wa Serikali za mitaa!

Hivi si mlikiri wenyewe kuwa Chadema wamewaandikia barua ya kuwajulisha kuwa kama chama kimejitoa kwenye huo UCHAFUZI wenu??

Iweje leo Waziri wa TAMISEMI unajaribu kuuhadaa Umma wa watanzania kuwa eti Chadema, ambacho ndiyo chama kikuu cha upinzani nchini kuwa imeshinda Mwenyekiti mmoja pekee, katika nchi yenye wenyeviti wa mitaa zaidi ya elfu themanini nchi nzima??

Hiyo ni mbinu ya kitoto kabisa ya kutaka kuendelea kutembeza bakuri la ombaonba kwenye nchi za wafadhili

Ama kweli hiki chama cha CCM kinaelekea mwisho wake na kinasubiri kuzikwa
 
Kuna mambo hapa duniani yanatokea Tanzania tu.Kwengine kote huko huwezi kuyakuta.
 
Hii ni historia mpya na ya kipekee katika taifa letu.

Wale akina Augustino Lyatonga Mrema waliofanya kampeni za uchaguzi eti wameambulia 0% na hawa akina Chadema na Cuf ambao walitangaza kujitoa ndio wamepata ushindi wa 0.1%

Tanzania tuna mambo ya kujivunia mengi.

Maendeleo hayana vyama!
Sisi tumepiga tu kura hatuangalii upo au umejitoa...
Salama ziwafikie ufipa.
 
Kwani mlikuwa mnashindana na nani jamani ccm mbona siwaelewi mm
 
CCM mmesimikwa kidikteta. Kila mtu anajua hamkuchaguliwa kihalali. Rais Magufuli anawagombanisha na wananchi wenu. Na nyie viongozi mlioteuliwa na kusimikwa kidikteta, nyumba mtakazolala zitakosa amani. Mtashindwa hata kuwaeleza jambo lolote wananchi. Labda mjiuzulu mapema kabla hamjaionja shubiri ya nguvu ya uma
Acha hizo. Kazi na ziendelee kama kawaida.
 
Nimeona nakala ya Polepole akipongeza chama chake kwamba kimeshinda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kwa asilimia 90.[emoji3]

Nimecheka sana, na sababu ya kucheka ni kwamba walio shiriki uchaguzi ni asilimia hata 20 haikufika, wakachukua mamluki baadhi ya vituo kupiga kura zaidi ya Mara moja, na kuwafukuza mawakala hata wale walio jitia hashuo la kushiriki eti ni wapinzani.

Kipimo cha haraka ni kuwa upinzani umeshinda uchaguzi, ispokuwa tume ya uchaguzi ikapora huo ushindi na kuwapa ccm. Yaani hata walio dhani ni wanachama wa ccm hawakushiriki uchaguzi.

2020 Oct ndio mtalia sana ccm, maana wananchi wapo upande wa haki na hawatakuwa tayari kuporwa ushindi wao, kupora haki zao za kugombea hata kupiga kura.

Shame on you CCM na tume ya uchafuzi.[emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom