Mawakili kesi ya Mbowe na wenzake watatu walibadili mbinu baada ya kuona kila pingamizi la utetezi linagonga mwamba

Kwa maneno machache baada ya kufuatilia hadi ilipofikia, nini imani yako kwenye hii kesi. Je, Mbowe na wenzake watatu, walikua wanapanga ugaidi?
 
Wameshamalizana kesho mbowe atakuwa huru chadema wasije na ngonjera za kuwa mbowe kashinda kesi wajue kabisa lisu washayajenga na mama
Na vipi ACP Kingai na wenzake, watapandishwa vyeo?
 
Nilivyoona kwenye kesi hii ni pale mipango yote ya upande wa Jamhuri yaliyokuwa yakipangwa gizani, yalikuja kuzungumzwa Mahakamani na Upande wa Utetezi. Hali hii iliwaogopesha Sana Jamaa wa Jamhuri. Walijiuliza Mambo yetu ya Siri tuliyoyazunfumza wenyewe imewafikiaje Jamaa wa Upande wa Utetezi?? Inamaana kuna watu miongoni mwetu wanaowapa/ wanaofujisha siri zetu.

Hata Jaji Tiganga mwenyewe alikujaona Hilo na akaanza kuwa na hofu pale anapohitaji kuwabebe upande wa Jamhuri. Unakumbuka hata Jaji Mkuu alifikia hatua ya kuwasemea Mawakili. Aliwalenga hasa wale wa Upande wa Mashitaka.

Mfano mwingine ni miamala iliyafanyika ktk kutuma fedha. Kuna miamala ilivyokuwa inamhusu Hussein Mwinyi (akiwa Waziri wa Ulizieni). Jaji Tiganga alipata hofu ni namna gani hawa Jamaa wa Utetezi waliipata miamala ile. Je waliipata kupitia Kampuni ya simu au kupitia Kwa baadhi ya maafisa wa Upande wa Mashitaka ama vipi.
 
Mimi nadhani kwa ushahidi wa upande wa mashitaka ulipofikia, hadi wameshindwa kuendelea kuleta wengine, jaji kesho atatoa picha nzima ya hii kesi. Ushahidi gani unafikiri unatakiwa hapa ku prove kwamba Mbowe na wenzake ni magaidi? Labda kama hujafuatilia kwa karibu hii kesi. Swila ameimaliza hii kesi, ndiyo maana mawakili wa jamhuri wakaamua kufunga ushahidi.
 
Ila walishindwa kupangua ukweli kuwa Mbowe alimtumia pesa Urio
Hivi mkuu, kuna maeneo nikisoma hoja zako nakuona uko vizuri upstairs, lakini sehemu kama hizi inaleta mashaka kama uko vizuri upstairs. Hivi kwa pesa vile zilivyotumwa, zinakupa useme kuna ugaidi? Hata Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi naye alifanya ugaidi kumtumia pesa Bwire? (akiwa waziri wa ulinzi).
 
Lissu kamuomba Samia hiyo kesi ifutwe, wacha tusubiri majibu
Ifutwe kwa sababu hii kesi ni sawa na "hekaya za abunuwasi'
Wametesa sana watu wasio na hatia
wametesa familia zao bila kumuogopa Mungu
Ila laana yao ni kubwa sana kwani itatesa pia watoto wao hadi vitukuu! hilo walifahamu
 
Maneno machache, nini kifanyike kwa hawa waliotengeneza hili jambo kwa hawa watu wanaotegemewa na familia zao? Kingai na list nzima?
 
Kwa hiyo Mbowe ana kesi ya kujibu?
 
Maneno machache, nini kifanyike kwa hawa waliotengeneza hili jambo kwa hawa watu wanaotegemewa na familia zao? Kingai na list nzima?
Mimi ni muumini wa msamaha kwa hiyo naungana na Lisu (ametamka redioni) kuwe tuwe na maridhiano ya kitaifa watu waombe msamaha hadharani kwa mambo ya hovyo waliyofanya kisha tusonge mbele kama taifa.

Na naamini kuwa hata mheshimiwa Mbowe ni muungwana sana na mzalendo wa nchi hii kwa dhati ya moyo wake na yeye ni mtu wa maridhiano hasa nikifuatilia hotuba zake na hata matendo yake baada ya kufanyiwa hujuma ya rasilimali zake mbali mbali. Tufungue ukurasa mpya kwa kutengeneza katiba mpya ambayo itaziba mianya ya mambo haya ya ovyo kutokea tena.

Kusiwe na kulipizana kisasi kwani tukianza hivyo mzunguko wake hautakuwa na mwisho. Lakini pia biblia takatifu inatuambia kuwa kisasi ni cha Mungu kwa hiyo tumwachie Mungu mwenyewe.
 
Shahidi wa mwisho V/S mama mdogo wenu swali ni kwamba kati ya hawa wawili ni nani mwongo katika kesi hii tokea mwanzo
 
Tunaonyèsha kama kesi ni rahisi lakini tunapambana kutaka iondoshwe kwa amri ya Rais...
 
Hoja nzuri- sasa wakili Kibatala angalia alikopotezea mda
ulitumiwa 500,000 ukatoa 499000 umemwambia mh. Jaji 1000 imeenda wapi? halafu watu mnasema kaupiga mwingi na unaona una uwezo wa kupima uwezo wangu wa kufikiri- kwanza hicho kipimo hakipo
 
Umenena vizuri sana mkuu ili Taifa lisonge mbele, tuanze upya. Lakini kama ingekua ni kitu kinawezekana kufanyika, unaona mtu kama ACP Kingai akiulizwa, anaweza kuongea ukweli na kuomba msamaha ili awe huru kwenye nafsi yake kwa yale aliyoyafanya kuifikisha hii kesi ilipofika?
 
Lissu kamuomba Samia hiyo kesi ifutwe, wacha tusubiri majibu
Kama ana akili timamu na ni mstaarabu atafuta tu bila kumuomba maana hata ye akitafakari iyo kesi haina kichwa wala miguu, kinachomsumbua anajua bila kutumia mabavu upinzani huwa wanawanyoosha vizuri tu kwenye election.....naye ni fever ya 2025 inamsumbua
 

Pascal njoo Huku usome namna watu wanafanya analysis! Andiko safi kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…