Maxence Melo: Ofisi za JamiiForums, Mikocheni 'zimevamiwa'

Maxence Melo: Ofisi za JamiiForums, Mikocheni 'zimevamiwa'

Heahima kwako kaka.

Nipo kila siku labda tunapishana tu.

Hii habari inanikumbusha mbali sana miaka ya urais wa Kikwete Max alivyoshikiliwa tukapigana mpaka akaachiwa.

Kikwete aliwaambia wale polisi wamuachie Max kwa sababu kumshikilia kukikuwa kunalipa taifa jina baya sana.

Inaonekana siku hizi hawajali image ya nchi tena.
Asante kaka.

Kweli sio sahihi kabisaa 😔 🤔 kilicho fanyika sio sahihi kabisaa kabisaaa. Tuna laani na kukipinga kwa nguvuuuuuuuu zotee
 
Na ni kwanini mtukane? Hamuwezi kujenga hoja bila kutukana. October tunatiki.
Screenshot_20250703-140259~2.png
 
Pole sana Melo. Tunakushukuru sana kwa update.

Kuvamiwa ofisi za JF, ina maana ya kuwavamia wanaJF wote. JF ndiyo chombo pekee cha habari kilicho huru. Kuvamia JF, ni uvamizi wa uhuru wa upashanaji habari. Kama uhuru wa JF utauawa itakuwa ni mazishi ya chombo pekee cha habari huru kilichokuwa kimesalia. Mungu wetu mwenye nguvu atulinde na watu wenye dhamira mbaya dhidi ya Taifa letu. Wanaoyafanya haya ni maadui wa Taifa letu.
 
Ukuzuia watu wasitukane unawachochea wafanye mapinduzi ya nguvu.

Huelewi wapi?

Wewe unafikiri nchi za magaharibi zinavyoruhusu uhuru mkubwa wa wananchi kutukana, unafikiri viongozi ni wajinga ?
Hii uliisoma wapi? Leta source ya kuvalidate post yako kwamba ukizuia watu wasitukane unawachochea wafanye mapinduzi ya nguvu.
 
Kila mmoja akumbuje password yake ya ule mtandao wa Kenya 🇰🇪 😳 😑 😂
 
Hii uliisoma wapi? Leta source ya kuvalidate post yako kwamba ukizuia watu wasitukane unawachochea wafanye mapinduzi ya nguvu.

Kwani kila kitu lazima nisome? Mimi mwenyewe siwezi kuandika?

Hii ni mantiki tu ukiwanyima watu sehemu ya ku let off steam kwa kutukana uongozi kwa njia zinazoonekana unawachochea waiondoe hiyo serikali kwa kwenda underground kupanga mapinduzi kwa njia zisizoonekana.

Ndiyo maana watawala wa nchi zikizoendel3a wamwruhusu free speech wajue watu wanakerwa na nibi, waweze hata kuwadhibiti vizuri.

Ukiwanyima watu nafasi ya kuitukana serikali serikali inakosa feedback mechanism ya kujua wananchi hawapendi nini, inajitengenezea mazingira ya ku fail zaidi.
 
Back
Top Bottom