Maxence Melo: Ofisi za JamiiForums, Mikocheni 'zimevamiwa'

Maxence Melo: Ofisi za JamiiForums, Mikocheni 'zimevamiwa'

Wakitumia mabavu kuendelea hadi 2030, kutakuwa na misukosuko sana, ni vyema kukubali mapema kama hukubaliki ukae kando..

Sijui agenda yake ni ipi, yaani akikaa anaelewa fika hapendwi ila analazimisha hadi kubeba watu na malori ya mchanga wanavunjika viuno na kufariki..

Inasikitisha sana...
Suala la kubeba watu kwenye maroli kuwapeleka mikutanoni ni utamaduni wa ccm kwa miaka mingi usimsingizie samia.
 
Alishindwa Magufuli ije iwe kwa nyie majizi na mafisadi.

Iko hivi server za JAMII FORUM zipo Marekani hata Maximelo awezi kujua utambulisho wa Wana jamii forum.

Imetokea Mara 3 attempt Kama hizi

Mpaka kutumia cyber attack lakini imeshindikana kukamata au kutambua member yeyote aliyepo jamii forum

Nawaonywa machawa na mafisadi wa nchi hii msijaribu kuizuia jamii forum kufanya kazi zake.

Hii ndio media pekee pamoja na mwananchi forum ya mange kimambi zilizo huru hata nyie mnazitumia mapaka kupotosha.

Kujaribu kuidhibiti ni kuingilia Uhuru wa Serikali,bunge na mahakama,JWTZ, TISS, Police na sector zote zenye maslahi kwa umma wa Watanzania!.

Nakuonywa Samia achana na jamii forum, jf itakuangusha ingawa ushaanguka!!
 
Tatizo nae mipasho mengi hanyooki,
Anaingia huku anatokea kule,
Mimi juz nilimchana kama ana kitu afunguke aache hiyo mipasho anayofanya,
kama kaamua kuongea aongee aslete taalabu
Actualy in hizi defence si kila kitu ni cha kuweka wazi, he is inside the system so hata yeye analinda opsec yake

It not about mipasho, even yeye pia yasije mrudi
 
Kuna ‘uvamizi’ usio rafiki uliofanyika muda sio mrefu katika ofisi za JamiiForums, Mikocheni jijini Dar wakinitafuta mimi
..
Nalaani vitendo kama hivi, ila umma utaujua ukweli hivi karibuni


UPDATE: Maxence Melo: Uvamizi uliofanywa kwenye ofisi za JamiiForums haujaathiri Shughuli, Miundombinu na wafanyakazi
Vipolishi na vitiss vilivyo pewa pesa za special task akili zao ndio hizooo.....polsi wengine wapo na njaa kali ....kazi yao kukamata vikirikuu , boda na kulinda ATM...tz ya baadhi ya askari mapumbavu
 
Uwa nashangaa serikali ina mambo mengi sana ya kufanya wananchi wengi wana matatizo yanaitaji kutatuliwa huwezi kutatua matatizo ya wananchi unakimbia kukamata wakosoaji?
 
Suala la kubeba watu kwenye maroli kuwapeleka mikutanoni ni utamaduni wa ccm kwa miaka mingi usimsingizie samia.
Kama tunamsifia kwa mengine kwa nini hili nalo tusimsifi? Unataka mazuri ndio yawe yake na mabaya ya wengine? Infact, katika awamu zote za CCM Samia kaenda extra mile na kuboresha juhudi za usombaji watu aka ng'ombe wa mama kuwaleta kwenye mikutano ya hadhara ya chama. Amewanunulia boda boda wenyeviti wa vitongoji na vijiji ili iwe rahishi kuhamasisha watu kuja kusombwa na kupelekwa mikutanoni, kanunua mabasi ya kusomba hao ng'ombe na mengine mengi. NANI ALIFANYA HAYO KABLA YAKE? NANI KAMA MAMA?
 
Selo zitajaa wana jf hakika.
Wengine wanaweza kujiua, ukizingatia ni watu wazito, wakubwa wenye kuheshimika lakini fake IDs zikawadanganya na kufanya tofauti na heshima zao au nafasi zao au kuaminiwa kwao.
 
Back
Top Bottom