Mayele aliianzisha vita ambayo haiwezi, kulia lia hakutomsaidia kitu

Sio lazima mchezaji kuipenda timu, ile ni ajira yake na yeye ni binadamu upendo wake unaweza kuwa kwenye timu nyingine sio jambo baya.
Labda sijaeleweka. Sikumaanisha kuipenda timu kama Mrisho Ngassa alivyoipenda Yanga, bali nilimaanisha hakuwa anaipenda Yanga kutokana na waliyomfanyia kwenye mkataba.
 
hana adabu,hana heshima,hana shukrani,eti nilikosea kucheza tanzania,,!huyu asuingie tena nchi hii,kama ana watu na vitu aliacha hapa aje kuvichukua,hata huyo kibaraka wake yasmin ambae nae katukanwa,kama zinamtosha ataachana nae
 
Ameikosea Yanga... kuna timu zingine zinamhitaji hapa tz... msitumie mbinu zenu za kiu topology kumzuia kuja kucheza tanzania
 
Mayele ni mchezaji wa kawaida sana.

Ningependa harudi Tanzania acheze Simba ama Azam ndio mtaamini kauli yangu.
 
kuishi na washirikina kuna hitaji hekima sana Fiston Kalala Mayele atakua kapata somo kwamba mchawi hana rafiki
 
Ndo maana anaflop Misri.
 
Yanga ilimbeba sana akawa maarufu.
 
Yaani uje Yanga tukukuze kipaji badala ya kuitumikia timu unatimka, sawa basi ukitimka huko uliko kaa kimya kama Feitoto!! Maneno ya shombo ya nini?
 
Mayele alijua akienda Misri atafunga tu kirahisi kama alivyofunga Tanzania jamaa anapenda sana media hata kocha wa Mamelodi alimwambia aache hizo mambo acheze mpira maana alipokosa Visa ya kuingia SA kwa wakati mechi yao na Mamelodi SA akaandika kwenye mitandao Mamelodi wameshawishi asipate Visa ili asishiriki na akasema Mkuje Misri...Mamelodi kama kawa wakatimba Misri na wakashinda ndio kocha akamwambia achana na upuuzi wa Media cheza mpira wakongo wengi wana vipaji ila mambo ya kushindana ndio yanawapoteza hata kwao vita ipo kwa sababu ya tabia zao za kipuuzi kama hizo...
Mayele hakua na sababu ya kutukana sehemu ambayo imemfanya apate jina na watu walimheshimu kweli sema kafanya mambo kama sio Professional.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…