Mayele aliianzisha vita ambayo haiwezi, kulia lia hakutomsaidia kitu

“Wanashambulia hadi familia yangu, nimemposti mtoto wangu wa kwanza ilikuwa siku ya Birthday yake watu wanaandika ushambaushamba mpaka baba yangu akanipigia simu anasema ‘ni nini hiki mbona sio wewe wanaanza kuingia kwenye familia, nilichomjibu baba ni kuwa nilikosea kucheza Tanzania”

Fiston Mayele akizungumza katika mahojiano na Azam Tv.

Hili linaloendelea litufundishe jambo, kuna mambo ya kuongea na kutokuongea, ikumbukwe yeye ndie alieanza kuirushia maneno Yanga na bado anaendelea. Sidhani kama ataiweza vita na mashabiki (maneno, ushirikina) na kama ndio mtu wa kujali yanayoandikwa mtandaoni hali itazidi kuwa mbaya kwake.

Ushauri wangu ni bora akae kimya kuliko kuendeleza maneno.

View attachment 2960619
Inasikitisha sana kuona kwamba kumbe Mayele alikuwa anacheza Yanga huku haipendi.
 
Mafanikio yote aliyowapa bado mkamtupia majini, acheni roho mbaya
 
Inasikitisha sana kuona kwamba kumbe Mayele alikuwa anacheza Yanga huku haipendi.
Sio lazima mchezaji kuipenda timu, ile ni ajira yake na yeye ni binadamu upendo wake unaweza kuwa kwenye timu nyingine sio jambo baya.
 
amesema mguu wake umevimba hadi leo, ulianza alipoamua kuondoka yanga. acheni uchawi.
Kama huu sio
E10E208B-E57B-427B-89AF-7B0C2BA02858.jpeg
 
Huyu anataka kwenda Kolobwanji anatafuta sababu Yanga wasimzuie Kama mkataba wa kuuziana Yanga na Pyramid unazuia asiuzwe Simba au Azam kabla ya Yanga kupewa nafasi ya kwanza kumnunua wakimhitaji.
Kama mkataba una vipengele hivyo ana mlima wa kupanda kuja kucheza nje ya yanga.
 
mayele ni mjinga na nilimdharau aliposema Yanga wanamroga. yeye ndiye aliyaanza na aache ujinga wa mitandao acheze mpira. huwezi kuwika kila sehemu. wamechemka magwiji wakubwa yeye nani kwenye soka mpaka asi flop kwamba lazima awike kila sehemu.
 
Wameondoka wengi Yanga waliopendwa hata kuliko hawa kina Mayele,na wala hawakutukanwa. Tatizo ni pale wanapoanza kukashifu timu. Majibu wanayapta kwa mashabiki wafia timu ambao ukiwaheshimu wanakuheshimu,ukiwadharau wanakudharau.
Asichojua ni kwamba Mashabiki wana nguvu sana kwenye timu. Hawezi kuisema timu vibaya alafu akaliwe kimya.
 
mayele ni mjinga na nilimdharau aliposema Yanga wanamroga. yeye ndiye aliyaanza na aache ujinga wa mitandao acheze mpira. huwezi kuwika kila sehemu. wamechemka magwiji wakubwa yeye nani kwenye soka mpaka asi flop kwamba lazima awike kila sehemu.
Anadhani atakiwasha muda wote, kushuka kwake kiwango isiwe sababu ya kuhusisha hali hiyo na Yanga, anakosea sana binafsi nilikuwa namkubali ila amenisikitisha kwa kauli zake.
 
mimi ni shabiki wa Simba na nilimpenda sana akiwa yanga. nitaichukia klabu yetu wakimsajili huyo fala. nachukia mchezaji anayekua mjingamjinga kudhihirisha ushirikina wake. kama uchawi aroge kimyakimya huko asitudhihirishie kuhusudu kwake ushirikina.
 
Shida ya timu zetu kuna ile kukomoana, simba wanaweza kufikia hatua ya kumsajili ili tu upande wa pili tuteseke.
 
Back
Top Bottom