Mayele aliianzisha vita ambayo haiwezi, kulia lia hakutomsaidia kitu

Mayele aliianzisha vita ambayo haiwezi, kulia lia hakutomsaidia kitu

“Wanashambulia hadi familia yangu, nimemposti mtoto wangu wa kwanza ilikuwa siku ya Birthday yake watu wanaandika ushambaushamba mpaka baba yangu akanipigia simu anasema ‘ni nini hiki mbona sio wewe wanaanza kuingia kwenye familia, nilichomjibu baba ni kuwa nilikosea kucheza Tanzania”

Fiston Mayele akizungumza katika mahojiano na Azam Tv.

Hili linaloendelea litufundishe jambo, kuna mambo ya kuongea na kutokuongea, ikumbukwe yeye ndie alieanza kuirushia maneno Yanga na bado anaendelea. Sidhani kama ataiweza vita na mashabiki (maneno, ushirikina) na kama ndio mtu wa kujali yanayoandikwa mtandaoni hali itazidi kuwa mbaya kwake.

Ushauri wangu ni bora akae kimya kuliko kuendeleza maneno.

View attachment 2960619
huyu ni nani?
 

Attachments

  • Screenshot_20240405_232604_Gallery.jpg
    Screenshot_20240405_232604_Gallery.jpg
    75.4 KB · Views: 1
Gongowazi wana ushetani mwingi sana mimi nilijua yameisha kumbe bado wanaendelea kumtumia majini mtoto wa watu.
 
Huyu anataka kwenda Kolobwanji anatafuta sababu Yanga wasimzuie Kama mkataba wa kuuziana Yanga na Pyramid unazuia asiuzwe Simba au Azam kabla ya Yanga kupewa nafasi ya kwanza kumnunua wakimhitaji.
 
Yanga na wanayanga wajifunze kupotezea... Msiwaandame mno wachezaji wanaotoka njee ya yanga.
Huu ni ushamba wa kiwango cha lami. Sijawahi ona jambo kama hili kwa simba na wanasimba kwa ujumla.
Anyway mtoto umleavyo ndivyo akuavyo...
Wameondoka wengi Yanga waliopendwa hata kuliko hawa kina Mayele,na wala hawakutukanwa. Tatizo ni pale wanapoanza kukashifu timu. Majibu wanayapta kwa mashabiki wafia timu ambao ukiwaheshimu wanakuheshimu,ukiwadharau wanakudharau.
 
Mayele alikosea kucheza utopoloni. Sio tanzania .hao utopolo akili hawana. .mchezaji wao yeyote akiwa mzuri akiondoka lazma watamchukia .angalia Morriston,feisal na sasa mayele. Hyo timu ndo tabia zake.we timu inaandika barua kuomba wapewe goli wana akili hao?
😂😂😂😂😂😂😂
 
Hapana. Mashabiki wa Yanga wamekuwa wakimfuatilia Mayelle na wachambuzi wao. Akifunga wanampost kuwa kafunga, asipopangwa wanasema anasugua benchi, hilo la majini limeongezea kasi tu.
Zilikuwa zinaanzishwa nyuzi' Leo katetema'. Shobo. Nzi WA kijani Wana shobo balaa😄😄😄
 
ALIKOSEA KUJA KUCHEZA TANZANIA...HALAFU MASHABIKI MAKOLO YANAKWAMBIA MAYELE KASHASAINI MKATABA NA KOLO FC
 
Back
Top Bottom