Mbeya: Mlima Kawetele wameguka, nyumba zaidi ya 20 zadaiwa kufunikwa

Mbeya: Mlima Kawetele wameguka, nyumba zaidi ya 20 zadaiwa kufunikwa

Salaam, shalom!!

View attachment 2963343

Mlima kawetele ulioko ITEZI, Uyole, jijini Mbeya umeripotiwa kumeguka na kuziangukia nyumba zaidi ya 20.

Chanzo Cha janga Hilo inasemekana ni mvua nyingi zinaonyesha Nchi nzima, zilizoloanisha udongo Kwa kiasi kikubwa.

Mwanzoni, iliaminika walioko milimani wako katika USALAMA zaidi, kumbe Si Kweli, Mvua za ernino ndio kwanza zimeanza, tuendelee kuwa na Tahadhari na kudumu katika maombi.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
Amen.

Source: ITV

Itezi Mbeya

----
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Abdi Isango

Ni kweli sehemu ya mlima imeporomoka na tope kusambaa na kuharibu nyumba 17 pamoja na Shule ya Msingi ya binafsi.

Nyumba zimebomoka kabisa hazionekani, ni kama vile hakukuwa na nyumba, tope limesabaa hakuna kipande cha bati au ubao.

Hakuna madhara kwa binadamu isipokuwa wenyeji wanasema kuna ng’ombe wanne wamesombwa na tope hilo.

Uchunguzi wa awali umebaini chanzo ni mvua kubwa zinzoendelea kunyesha, mvua zilinyesha jana na usiku wa kuakia leo, ambapo Alfajiri ndipo tope likaasambaa.

Wenyeji wanasema kwa kuwa kuna shughuli za kilimo, inawezekana kilimo kimesababisha udongo ukose mshikamano na hivyo mvua inaponyesha inakuwa rahisi kukatika.

Chini ya huo Mlima kuna Mto, mbapo umesomba tope hilo Kwenda mbele zaidi, tope lilikuwa kubwa, limesambaa na kusababisha madhara pia katika nyumab nyingine kadhaa.

Mkuu wa Mkoa na Kamati ya Ulinzi wamefika eneo la tukio na kutoa maelekezo ya tahadhari, Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari kwa kuwa mvua zinaendelea kunyesha, pia wanaojenga karibu na mito nao wametakiwa kuchukua tahadhari kwa kuwa mvua bado zinaendelea kunyesha.
View attachment 2963359
Chanzo cha matatizo yote haya ni Magufuli,
alikuwa hasikilizi wataalam
 
Majanga kama hayo yako dunia nzima. Sio swala la kuomba Mungu, tutafute wataalam wafanye tafiti watoe taarifa zenye faida kwa wananchi na maeneo husika.

Kama eneo halifai kwa makazi wahame, au kama kunawezekana kutengeneza kingo kuzuia tope ifanyike.

Kama ni landslike hiyo huwa inachukua eneo kubwa, hivyo utafiti ufanyike ili kujua ni eneo gani ni salama kwa makazi na shughuli za kilimo na ufugaji, ili wananchi waweke nguvu zao huko.
 
Wataalamu waendelee na KAZI Yao,

Na maombi yaendelee kama kawaida.
 
Kuna wadau wanatafuta namna ya kumuangushia jumba bovu yule mshua ila connection inagoma!

BTW:Milima isiyokuwa na miamba ni suala la muda tu chochote kutokea.

Ile ya Mwanza labda lije tetemeko lenye ritcher scale above 8.0.
 
Maombi hayana tija kwenye hivi vitu. Zifanywe tafiti za kweli, zifanyiwe kazi, wananchi wapewe maelekezo ya kitaaluma mambo ya kimaisha yaendelee, wataomba wakihamia sehemu salama.
Sehemu salama ni ipi?
 
Back
Top Bottom