Basi chukua mche mmoja wa mti na jembe, nenda pembeni ya barabara ya lami, upande Kisha ukitoka kazini jioni daily, pita na dumu la maji umwagie Hadi ukue.Kila kitu mpaka mfanye muwasubirie viongozi
Jukumu la kutunza mazingira ni la wakazi/wananchi wa maeneo hayo wenyewe
Ova
Yuko site muda tu mbona hukumsikia hapo "kiphande khile thu ndoho kimekatikah" 😂😂😂Lucas Mwashambwa upo salama?
Chanzo cha matatizo yote haya ni Magufuli,Salaam, shalom!!
View attachment 2963343
Mlima kawetele ulioko ITEZI, Uyole, jijini Mbeya umeripotiwa kumeguka na kuziangukia nyumba zaidi ya 20.
Chanzo Cha janga Hilo inasemekana ni mvua nyingi zinaonyesha Nchi nzima, zilizoloanisha udongo Kwa kiasi kikubwa.
Mwanzoni, iliaminika walioko milimani wako katika USALAMA zaidi, kumbe Si Kweli, Mvua za ernino ndio kwanza zimeanza, tuendelee kuwa na Tahadhari na kudumu katika maombi.
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
Amen.
Source: ITV
Itezi Mbeya
----
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Abdi Isango
Ni kweli sehemu ya mlima imeporomoka na tope kusambaa na kuharibu nyumba 17 pamoja na Shule ya Msingi ya binafsi.
Nyumba zimebomoka kabisa hazionekani, ni kama vile hakukuwa na nyumba, tope limesabaa hakuna kipande cha bati au ubao.
Hakuna madhara kwa binadamu isipokuwa wenyeji wanasema kuna ng’ombe wanne wamesombwa na tope hilo.
Uchunguzi wa awali umebaini chanzo ni mvua kubwa zinzoendelea kunyesha, mvua zilinyesha jana na usiku wa kuakia leo, ambapo Alfajiri ndipo tope likaasambaa.
Wenyeji wanasema kwa kuwa kuna shughuli za kilimo, inawezekana kilimo kimesababisha udongo ukose mshikamano na hivyo mvua inaponyesha inakuwa rahisi kukatika.
Chini ya huo Mlima kuna Mto, mbapo umesomba tope hilo Kwenda mbele zaidi, tope lilikuwa kubwa, limesambaa na kusababisha madhara pia katika nyumab nyingine kadhaa.
Mkuu wa Mkoa na Kamati ya Ulinzi wamefika eneo la tukio na kutoa maelekezo ya tahadhari, Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari kwa kuwa mvua zinaendelea kunyesha, pia wanaojenga karibu na mito nao wametakiwa kuchukua tahadhari kwa kuwa mvua bado zinaendelea kunyesha.
View attachment 2963359
Magu Uliyemtaja ni Mwenyekiti wa kitongoji Cha Kiwetele, Ileje Mbeya?Chanzo cha matatizo yote haya ni Magufuli,
alikuwa hasikilizi wataalam
Nyie wa Isanga kwani siyo mlimani pale?Maeneo mengi ya Mbeya huko Itezi sijui Isyesye kule milimani sio salama kabisa ni vile watu wanataka kujenga sehemu yeyote ila kwa kuangalia tu baadhi ya maeneo unayaona ni hatarishi kabisa..
Tuntufye Kyala bhosa bhumi....😀Poleni bhandu bha Kyala...
Wataalamu waendelee na KAZI Yao,Majanga kama hayo yako dunia nzima. Sio swala la kuomba Mungu, tutafute wataalam wafanye tafiti watoe taarifa zenye faida kwa wananchi na maeneo husika.
Kama eneo halifai kwa makazi wahame, au kama kunawezekana kutengeneza kingo kuzuia tope ifanyike.
Kama ni landslike hiyo huwa inachukua eneo kubwa, hivyo utafiti ufanyike ili kujua ni eneo gani ni salama kwa makazi na shughuli za kilimo na ufugaji, ili wananchi waweke nguvu zao huko.
johnthebaptist kwao ni Tanangozi
Sasa km wanasema kafanya hivyo Rufiji atashindwaje Mbeya?Magu Uliyemtaja ni Mwenyekiti wa kitongoji Cha Kiwetele, Ileje Mbeya
johnthebaptist unaitwa huku!johnthebaptist kwao ni Tanangozi
Hiki ni kizazi cha laana mzee.Magu Uliyemtaja ni Mwenyekiti wa kitongoji Cha Kiwetele, Ileje Mbeya?
Maombi hayana tija kwenye hivi vitu. Zifanywe tafiti za kweli, zifanyiwe kazi, wananchi wapewe maelekezo ya kitaaluma mambo ya kimaisha yaendelee, wataomba wakihamia sehemu salama.Wataalamu waendelee na KAZI Yao,
Na maombi yaendelee kama kawaida.
Sehemu salama ni ipi?Maombi hayana tija kwenye hivi vitu. Zifanywe tafiti za kweli, zifanyiwe kazi, wananchi wapewe maelekezo ya kitaaluma mambo ya kimaisha yaendelee, wataomba wakihamia sehemu salama.
Ambayo haina landslide.Sehemu salama ni ipi?
Ukataji miti kwenye maeneo yenye miinuko na Kingo ni hatari sana. IPO haja ya kunza mazingira na kuyalinda, serikali na asasi mbalimbali na sisi wananchiWamekata miti yote kwenye huo mlima landslide lazima itokee .
Kwahiyo vipi kuhusu Matetemeko, vimbunga, mafuriko, Ajali ya moto, volcano nknk?Ambayo haina landslide.