Mbeya: Mwalimu aua mke na watoto wawili, naye ajiua kwa kunywa sumu

Mbeya: Mwalimu aua mke na watoto wawili, naye ajiua kwa kunywa sumu

Watu wasiiharibu taasisi ya ndoa kwa mambo yao ya kipumbavu..Akili za kijinga kabisa hizi
 
Huyo mwanaume kwq sura tuu anaonekana mkatili,dictactor na mtu wa shari mnaosema mke kachepuka msihukumu labda hata alinyimwa paja la kuku akala yy mwanaume akaona amedharaulika.
 
Huko njombe jamaa kamuua mchizi kisa alimkumbatia mkewe wakati wanacheza dansi kwenye sherehe, tofali moja la kichwa mwamba kazima
Dah [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] wakunjombe nao kumbe Wana vituko ? [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] Yote hii Lisa papuchi
Alaaniwe aliyeleta papuchi
 
Shida ya ndoa za mwanaume na mwanamke wote waajiriwa hua zina migogoro sana. Nilishasema na nitasema tena mke apaswa kukaa nyumbani wakiwa na vijiajira hua wanakua natdharau, na dhihaka za mwendo kasi.

Kufikia kuua mke na watoto huyo mwanaume yalimfika hapa. NIONYESHE MWANAMKE MWENYE AJIRA ALIE MNYENYEKEVU KWA MUME WAKE NA MIMI NITAKUONYESHA MBUZI ANAETAGA MAYAI.
Nilimshauri rafiki yangu, "achana na huyo mwanamke" Bahati nzuri alinielewa na maisha yanaendelea!

Ilikuwaje?
Jamaa wanaishi mikoa tofauti na mzazi mwenzake, (japo wamezaa watoto 2 lakini hawana ndoa), kutokana na distance jamaa akaanzisha mahusiano na binti fulani kitaa, binti penzi likamkolea akaamua kumzalia jamaa mtoto! (Akalazimika kujitetea mbele ya mkewe kwamba ameteleza tu) mke akasema poa, maisha yaendelee!

Jamaa katika pilika zake, akabaini kwamba mkewe/mzazi mwenzake analiwa na jamaa mwingine Dom akafanya uchunguzi binafsi na kubaini kuwa kweli mke anagawa uroda kwa mwanaume mwingine, kumuuliza mkewe akawa mbogo!
"Sina mwanaume wa kunichunga, kwani una ndoa na mimi?, hauna cha kunibabaisha, kama una maamuzi ya kufanya yafanye tu! Kwanza unajiona na wewe kidume wakati kutwa kubwabwaja tu"

Baada ya hayo maneno na mengine mengi niliyoyasahau jamaa akapata moto, na kutaka kumfuata huyo mke anakoishi, nikamwambia "Kaka, achana na huyo mwanamke, utaishia jela, japo ulimkosea kwa kuchepuka na kuzaa nje lakini nakushauri achana naye, ni either atakuua au wewe utamuua yeye" bahati nzuri jamaa alinielewa, baadaye alijipatia mwanamke wa Kigoma huko akaoa chap, (mke/mzazi mwenzake akashangaa tu jamaa anapost picha za ndoa na mke mwingine) akaanza mikwara ya nakupeleka ustawi wa jamii, sijui mahakamani jamaa akauchuna kimya! Alichofanya ni kulipa ada za watoto basiii, maswala mengine mama yao anamaliza (si alisema hatishiki wala hababishwi kwa kuwa ana mshahara wake??)

Baadaye mke aliyeachwa, akanitafuta "Shem naomba ongea na rafiki yako, akumbuke tulikotoka, mm nilimsamehe na yeye angenisamehe kwa kumcheat, tulee watoto wetu, maana hata jamaa niliyekuwa naye Dodoma, alishaoa alisema hawezi kuoa mtu mwenye watoto 2, nimebaki na upweke wangu"

Baada ya kumaliza kujieleza meeengi nikamwambia, "Mimi pia nilimshauri aachane na wewe ili usimuue wala yeye asikuue wewe, hii ilitokana na namna ulivyokuwa unamjibu hovyo mumeo, na kuonyesha wazi kuwa hana maana tRNA kwako, kwa hiyo ujue tu, kwamba hata mimi rafiki yake nilikunusuru wewe na yeye msiuane, hayo mengine mnaweza kuyaongea wenyewe kwa sasa kwa kuwa hasira zenu zimekwisha" ila ukumbuke yeye ni mume wa mtu!

Baada ya hapo, alikuwa very down na alipoondoka HAKUNITAFUTA TENA! and I didn't care kabisa! Wakati fulani ni bora kuamua tu haijalishi maamuzi yana matokeo ya namna gani!
 
Watu wanne wa familia moja katika kijiji cha Kibumbe, Kata ya Kiwira wilayani Rungwe wamfariki dunia baada ya kudaiwa kunywa sumu inayotumika katika mimea ya mbogamboga shambani kwa kile kilichoelezwa ni wivu wa mapenzi.

Watu hao akiwamo baba, mama ambao ni walimu wa Shule ya Msingi Ikuti na watoto wao wawili walibainika waamefariki baada ya harufu kali kuanza kutoka ndani ya nyumba yao waliyokuwa wakiishi.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Septemba 14, 2022 jijini Mbeya na kaka wa marehemu George Mjaka ambaye amesema familia hiyo ya Adam Mtambo imeteketea wakati matukio ya mauaji ya familia yakiendelea kuongezeka wilayani humo.

Amesema wawili hao walikuwa na ugomvi wa kimapenzi ambapo wote wawili walikuwa walimu wa Shule ya Msingi Ikuti.

“Dada yangu Furtunata mumewe na watoto wao wawili tuliwakuta wamefariki. Tulipoingia tuliona mapanga chini, nyundo na ndani tukaona sumu yaani dawa za kumwagilia mboga na kikombe na kijiko.

"Kabla tulikuja huku tukaona kuna harufu inatoka ndiyo tukavunja mlango baada ya polisi kutupatia ruhusa ya kufanya hivyo,” amesema George.

Naye Mwenyekiti wa kitongoji cha Kibumbe, Ulimboka Mwakyenja amesema mauaji yanayoendelea ya kutisha katika kitongoji hicho Serikali inapaswa kuingilia kati, “Naomba Serikali isiichoke kuendelea kutoa elimu kila mahali ikiwemo kanisani.”

Diwani wa Kiwira, Michael Mwamembe amesema, “Kwa taarifa zilizopo kulikuwa na migogoro ya ndoa ambayo wamesuluhisha kwa muda mrefu, kila siku kuna haja ya Serikali kuliangalia suala hili kwa umakini mkubwa.”

Mkuu wa wilaya ya Rungwe, Dk Vicent Anei ametoa onyo na rai kwa wananchi kutochukua maamuzi hayo yakiwemo mauaji yanayosababishwa na imani za kishirikina.

“Kujitoa uhai ni jambo gumu sana lakini watu wanajitoa uhai na wanaua familia zao pia kwakweli Serikali tutafanya utafiti tuone namna gani tutapambana na janga hili kwa kuwa ni kubwa, changamoto binadamu tunazimaliza lakini si kwa kuamua namna hii, huyu kaua watoto wasio na hatia malaika wa Mungu inaumiza sana.”

Baadhi ya majirani wamesema wanandoa hao walikuwa na migogoro ya muda mrefu kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Chanzo: Mwananchi
 
Angewaacha watoto au ile ya kusema... tena hawa watoto siyo wako...

So sad.
 
Nilimshauri rafiki yangu, "achana na huyo mwanamke" Bahati nzuri alinielewa na maisha yanaendelea!

Ilikuwaje?
Jamaa wanaishi mikoa tofauti na mzazi mwenzake, (japo wamezaa watoto 2 lakini hawana ndoa), kutokana na distance jamaa akaanzisha mahusiano na binti fulani kitaa, binti penzi likamkolea akaamua kumzalia jamaa mtoto! (Akalazimika kujitetea mbele ya mkewe kwamba ameteleza tu) mke akasema poa, maisha yaendelee!

Jamaa katika pilika zake, akabaini kwamba mkewe/mzazi mwenzake analiwa na jamaa mwingine Dom akafanya uchunguzi binafsi na kubaini kuwa kweli mke anagawa uroda kwa mwanaume mwingine, kumuuliza mkewe akawa mbogo!
"Sina mwanaume wa kunichunga, kwani una ndoa na mimi?, hauna cha kunibabaisha, kama una maamuzi ya kufanya yafanye tu! Kwanza unajiona na wewe kidume wakati kutwa kubwabwaja tu"

Baada ya hayo maneno na mengine mengi niliyoyasahau jamaa akapata moto, na kutaka kumfuata huyo mke anakoishi, nikamwambia "Kaka, achana na huyo mwanamke, utaishia jela, japo ulimkosea kwa kuchepuka na kuzaa nje lakini nakushauri achana naye, ni either atakuua au wewe utamuua yeye" bahati nzuri jamaa alinielewa, baadaye alijipatia mwanamke wa Kigoma huko akaoa chap, (mke/mzazi mwenzake akashangaa tu jamaa anapost picha za ndoa na mke mwingine) akaanza mikwara ya nakupeleka ustawi wa jamii, sijui mahakamani jamaa akauchuna kimya! Alichofanya ni kulipa ada za watoto basiii, maswala mengine mama yao anamaliza (si alisema hatishiki wala hababishwi kwa kuwa ana mshahara wake??)

Baadaye mke aliyeachwa, akanitafuta "Shem naomba ongea na rafiki yako, akumbuke tulikotoka, mm nilimsamehe na yeye angenisamehe kwa kumcheat, tulee watoto wetu, maana hata jamaa niliyekuwa naye Dodoma, alishaoa alisema hawezi kuoa mtu mwenye watoto 2, nimebaki na upweke wangu"

Baada ya kumaliza kujieleza meeengi nikamwambia, "Mimi pia nilimshauri aachane na wewe ili usimuue wala yeye asikuue wewe, hii ilitokana na namna ulivyokuwa unamjibu hovyo mumeo, na kuonyesha wazi kuwa hana maana tRNA kwako, kwa hiyo ujue tu, kwamba hata mimi rafiki yake nilikunusuru wewe na yeye msiuane, hayo mengine mnaweza kuyaongea wenyewe kwa sasa kwa kuwa hasira zenu zimekwisha" ila ukumbuke yeye ni mume wa mtu!

Baada ya hapo, alikuwa very down na alipoondoka HAKUNITAFUTA TENA! and I didn't care kabisa! Wakati fulani ni bora kuamua tu haijalishi maamuzi yana matokeo ya namna gani!

Mkuu wewe ni MWANAUME!

Jipige kifuani ukisema wewe ni mwanaume! Safi kabisa!
 
Mbaya sana mm ningelimwachia watoto wake nikakae mbali kabisa kama ni ajira pia naachana nayo natafuta maisha mengine tofauti kabisa apambane na hali yake
Hii dhambi ya wivu na migogoro ya mapenzi kuna kitu ndani ya pazia
Ugumu wa maisha + wivu wa mapenzi =?
 
unazaa mtoto wa kike. unamlea. anaenda kuolewa na jinga kama hili anauliwa kikatili namna hii. inaumiza sana.
Issue inaanza ndani ya familia hasa wazazi,Kama ulikosea malezi au wewe/ninyi mlikuwa wazazi wa hovyo, basi hayo ndio matokeo
 
Mkuu Comment ya sita hy unazungumzia swala hili nahisi kuna mengi unayajua
Elimu ni pana.
Usijifungie kwenye box.Zijue siri za dunia kwa kujifunza elimu kuhusu nguvu zinazotawala dunia na ujue jinsi ya kuzitawala.
Magonjwa ya kiroho ndio chanzo cha vurugu zote za mwanadamu
 
Dah [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] wakunjombe nao kumbe Wana vituko ? [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] Yote hii Lisa papuchi
Alaaniwe aliyeleta papuchi
Bila papuchi ungezaliwa mkuu
 
DNA effect!

Mapenzi kitovu cha uzembe!

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom