Shida ya ndoa za mwanaume na mwanamke wote waajiriwa hua zina migogoro sana. Nilishasema na nitasema tena mke apaswa kukaa nyumbani wakiwa na vijiajira hua wanakua natdharau, na dhihaka za mwendo kasi.
Kufikia kuua mke na watoto huyo mwanaume yalimfika hapa. NIONYESHE MWANAMKE MWENYE AJIRA ALIE MNYENYEKEVU KWA MUME WAKE NA MIMI NITAKUONYESHA MBUZI ANAETAGA MAYAI.
Nilimshauri rafiki yangu, "achana na huyo mwanamke" Bahati nzuri alinielewa na maisha yanaendelea!
Ilikuwaje?
Jamaa wanaishi mikoa tofauti na mzazi mwenzake, (japo wamezaa watoto 2 lakini hawana ndoa), kutokana na distance jamaa akaanzisha mahusiano na binti fulani kitaa, binti penzi likamkolea akaamua kumzalia jamaa mtoto! (Akalazimika kujitetea mbele ya mkewe kwamba ameteleza tu) mke akasema poa, maisha yaendelee!
Jamaa katika pilika zake, akabaini kwamba mkewe/mzazi mwenzake analiwa na jamaa mwingine Dom akafanya uchunguzi binafsi na kubaini kuwa kweli mke anagawa uroda kwa mwanaume mwingine, kumuuliza mkewe akawa mbogo!
"Sina mwanaume wa kunichunga, kwani una ndoa na mimi?, hauna cha kunibabaisha, kama una maamuzi ya kufanya yafanye tu! Kwanza unajiona na wewe kidume wakati kutwa kubwabwaja tu"
Baada ya hayo maneno na mengine mengi niliyoyasahau jamaa akapata moto, na kutaka kumfuata huyo mke anakoishi, nikamwambia "Kaka, achana na huyo mwanamke, utaishia jela, japo ulimkosea kwa kuchepuka na kuzaa nje lakini nakushauri achana naye, ni either atakuua au wewe utamuua yeye" bahati nzuri jamaa alinielewa, baadaye alijipatia mwanamke wa Kigoma huko akaoa chap, (mke/mzazi mwenzake akashangaa tu jamaa anapost picha za ndoa na mke mwingine) akaanza mikwara ya nakupeleka ustawi wa jamii, sijui mahakamani jamaa akauchuna kimya! Alichofanya ni kulipa ada za watoto basiii, maswala mengine mama yao anamaliza (si alisema hatishiki wala hababishwi kwa kuwa ana mshahara wake??)
Baadaye mke aliyeachwa, akanitafuta "Shem naomba ongea na rafiki yako, akumbuke tulikotoka, mm nilimsamehe na yeye angenisamehe kwa kumcheat, tulee watoto wetu, maana hata jamaa niliyekuwa naye Dodoma, alishaoa alisema hawezi kuoa mtu mwenye watoto 2, nimebaki na upweke wangu"
Baada ya kumaliza kujieleza meeengi nikamwambia, "Mimi pia nilimshauri aachane na wewe ili usimuue wala yeye asikuue wewe, hii ilitokana na namna ulivyokuwa unamjibu hovyo mumeo, na kuonyesha wazi kuwa hana maana tRNA kwako, kwa hiyo ujue tu, kwamba hata mimi rafiki yake nilikunusuru wewe na yeye msiuane, hayo mengine mnaweza kuyaongea wenyewe kwa sasa kwa kuwa hasira zenu zimekwisha" ila ukumbuke yeye ni mume wa mtu!
Baada ya hapo, alikuwa very down na alipoondoka HAKUNITAFUTA TENA! and I didn't care kabisa! Wakati fulani ni bora kuamua tu haijalishi maamuzi yana matokeo ya namna gani!