Mbeya: Watu wa Igurusi na Chimala msitoke nje Usiku, Simba wamekata kamba na kuruka kutoka kwenye gari

Mbeya: Watu wa Igurusi na Chimala msitoke nje Usiku, Simba wamekata kamba na kuruka kutoka kwenye gari

View attachment 3487751
Find i(t)
Assuming the circuit has reached steady state at t=0
Kuandika hesabu kazi vialama vyake
Likikushinda, sema nikuletee yale ya kutafuta chatgpt, hilo hulikuti mule....
Wewe maswali yako ni ya kitoto hapa jf walikuja waprofesa feki wa UDSM wakanikimbia nioiwatega je transformer inafanya kazi na umeme wa dc wakaja na jibu la hapana ...waulize kilicho wakuta mimi sitoi majibu gpt hiyo gpt nimeizidi logic
 
Tatizo sio tu hao simba kula hao watu.

Hapa tuangalie chanzo cha ugonjwa ili tuutibu na usijirudie kizembe tena.

Simba wamewezaje kuruka wakiwa wanasafirishwa mbona inaonesha kuna uzembe wa wazi hapa.

Isiwe yale mambo ya gharama ya banda la kuwasafirishia inapangwa 30mil ila inatumika 7 au 10m kisa waliwahi wakusafirisha kwa mtindo huo hvyo wanasafirishia mazoea.
 
Mbwa wanajua harufu ya Simba kwa hiyo huwa wanahama wote kijijini mpaka simba waondoke
Hiyo harufu wamejifunzia wapi hali ya kuwa hawajawah kuonana na Simba before?....

Mbona maporini wamasai wanakaa na Mbwa na eneo ambalo Simba wapo?
 
Hiyo ni hatari sana. Idara ya wanyamapori ni mojawapo ya idara ya hovyo kuwahi kuwepo nchini. Miaka kadhaa nyuma kwenye hii awamu ya 6 kulitokea matukio ya fisi kuwala watu hasa watoto maeneo ya wilaya ya Karatu ikaleta sana taharuki. Binadamu zaidi ya 20 waliliwa na fisi hadi aliyekuwa mbunge vitu maalum CHADEMA Cecilia Paresso akapeleka hoja bungeni. Ikavuja kashfa kwamba hao fisi walitolewa Ngorongoro na kupelekwa nje ya hifadhi kutokana na fisi kuwa wengi mno. Idara haikuwahi kujibu kitu. Mama Samia anangeifumua hiyo idara inayokula hela za bure.
Imekuwaje leo umeshindwa kutetea unatuchanganya watazamaji 🤣🤣🤣
 
Hii Ngoma nimechukua juzi tu baada ya kuikumbuka wale Simba walikuwa ni wa mazingara ata jamaa alihisi

Bonge la movie.

Waafrika mtachelewa kila kitu kwa hizi imani za ushirikina.
 
Hii pia ukisoma history ya ujenzi wa tazara pia kulikua na hizi SAGA za vibaruab/ manamba kuliwa na Simba kwenye mapori / hifadhini huko morogoro hifadhini mikumi
Hii nayo ni story ila nafikiri haijaandikwa.
 
Hivi unapoona idara ya wanyamapori ni ya hovyo kiasi cha kutamani ivunjwe, unaelewa kwamba hiyo hasira yako inatokana na tatizo kubwa zaidi la kimfumo?

Kwamba uzembe, ukosefu wa uwajibikaji, na ukimya wa mamlaka sio tu kasoro za watu binafsi bali ni matokeo ya mfumo usio na mizania ya uwajibikaji.

Unajua kwamba hiyo ndiyo sababu watu wanapaza sauti wakitaka katiba mpya, katiba itakayoweka misingi ya wazi ya uwajibikaji, mgawanyo wa madaraka, na ulinzi wa haki za raia dhidi ya uzembe wa taasisi?

Lakini cha kushangaza, humu humu jukwaani, hoja za katiba mpya zikianzishwa, nyinyi mnaonekana kuwa wapinzani wakubwa.

Mwanzoni nilidhani labda mnafaidika na mfumo huu wa hovyo, labda mna neemeka kwenye uongozi au mnachota faida kupitia mianya ya upigaji.

Lakini kwa jinsi ulivyoandika hapa, inaonekana wewe ni raia muangaikaji kama sisi unaumia, unakerwa, unahofia usalama wako tena dhidi ya fisi.

Sasa swali ninalojiuliza mpaka sasa: kwa nini basi mnapata morale ya kuwatetea watawala au kupinga mabadiliko ya msingi kama katiba mpya, ilhali mnateseka na matokeo ya mfumo huo huo mnaoutetea?
Punguza siasa kwenye kila kitu. Hiyo katiba mpya ndo itafanya watu wawe watakatifu? Uadilifu unaanzia kwenye familia kabla ya kufika ngazi ya taifa. Wewe anza kwanza kubadili fikra za familia yako ndo uje kwenye katiba.
 
Simba kwa siku anakula kilo ngapi za nyama?
 
Punguza siasa kwenye kila kitu. Hiyo katiba mpya ndo itafanya watu wawe watakatifu? Uadilifu unaanzia kwenye familia kabla ya kufika ngazi ya taifa. Wewe anza kwanza kubadili fikra za familia yako ndo uje kwenye katiba.
Unalalamikia uzembe wa taasisi, ukosefu wa uwajibikaji, na madhara wanayopata wananchi ambayo kwa asili ni malalamiko ya kisiasa.

Lakini kwa mshangao, unajaribu kupinga hoja ya katiba mpya kwa madai kuwa ni 'siasa tu'. Hapo tayari kuna contradictioni.

Kwasababu huwezi kulalamikia matokeo ya mfumo bila kuzungumzia chanzo chake, ambacho ni katiba inayounda na kuongoza mfumo huo.

Halafu uadilifu hautoki kwenye familia pekee, kumbuka Katiba ni chombo cha kusimamia maadili ya viongozi wa umma kwa kuweka mipaka, uwajibikaji na uwazi.

Na ndio maanaa hata wewe ulipoona uzembe unafanyika kwenye hiyo taasisi ya TANAPA ulishauri ivunjwe, hiyo ni kuonesha kwamba tatizo si ya tabia ya mtu mmoja inayosababishwa na changamoto ya uadilifu ndani ya familia yake, bali ni mfumo wote unaoruhusu uzembe huo kufanyika bila adhabu.

Hiyo ndiyo sababu tunasisitiza mabadiliko ya katiba, si kwa sababu tunaamini kila mtu ni mwema, bali kwa sababu tunajua si kila mtu ni mwema, na hivyo tunahitaji mfumo unaowajibisha.
 
Kuandika hesabu kazi vialama vyake

Wewe maswali yako ni ya kitoto hapa jf walikuja waprofesa feki wa UDSM wakanikimbia nioiwatega je transformer inafanya kazi na umeme wa dc wakaja na jibu la hapana ...waulize kilicho wakuta mimi sitoi majibu gpt hiyo gpt nimeizidi logic
Acha mbaambaa, jibu swali...
Hii ni therapy, nakutibu huu ugonjwa wako wa obsessive hatred syndrome kwa Rostam
Maana hapiti siku bila kumtajataja.
 
Unalalamikia uzembe wa taasisi, ukosefu wa uwajibikaji, na madhara wanayopata wananchi ambayo kwa asili ni malalamiko ya kisiasa.

Lakini kwa mshangao, unajaribu kupinga hoja ya katiba mpya kwa madai kuwa ni 'siasa tu'. Hapo tayari kuna contradictioni.

Kwasababu huwezi kulalamikia matokeo ya mfumo bila kuzungumzia chanzo chake, ambacho ni katiba inayounda na kuongoza mfumo huo.

Halafu uadilifu hautoki kwenye familia pekee, kumbuka Katiba ni chombo cha kusimamia maadili ya viongozi wa umma kwa kuweka mipaka, uwajibikaji na uwazi.

Na ndio maanaa hata wewe ulipoona uzembe unafanyika kwenye hiyo taasisi ya TANAPA ulishauri ivunjwe, hiyo ni kuonesha kwamba tatizo si ya tabia ya mtu mmoja inayosababishwa na changamoto ya uadilifu ndani ya familia yake, bali ni mfumo wote unaoruhusu uzembe huo kufanyika bila adhabu.

Hiyo ndiyo sababu tunasisitiza mabadiliko ya katiba, si kwa sababu tunaamini kila mtu ni mwema, bali kwa sababu tunajua si kila mtu ni mwema, na hivyo tunahitaji mfumo unaowajibisha.
Sasa kama familia yako haina maadili unadhani taifa ndo litakuwa na maadili kupitia katiba? Hao viongozi wanatoka ndani ya familia zetu hawajashushwa kutoka mbinguni.
 
Jambazi Rostam azizi mmiliki wa koloni lake la tanganyika🤔 au wewe ni chawa wake...hiyo familia imeua watu wengi sana
Acha mbaambaa, jibu swali...
Hii ni therapy, nakutibu huu ugonjwa wako wa obsessive hatred syndrome kwa Rostam
Maana hapiti siku bila kumtajataja.
 
Back
Top Bottom