Mbeya: Wenye nyumba za tope mjini kuhamishwa

Hizo nyumba ziko mbeya maeneo gani
Blok t,forest,blok q,uhindini,ghana au

Ova

Labda Soko Matola , halafu wakati yeye anasema ni aibu awashauri wenzake wapunguze bei ya cement, nondo, mabati ili watu wajenge haraka
 
The look in Nairobi


Bado zipo!
 
Kwa kweli wananchi wa Mbeya wako nyuma sana katika kujenga nyumba bora.
Hilo siyo siri.
 
Naunga mkono hoja, waende matundasi, mamba A huko au mtanila kabisa.
 
Ile Simike yote zile nyumba si ni tofali za udongo zile hazijachomwa...

Kule Nzovwe, mitaa ya nyuma ya Mafiat hapo sijui wanakuita Mwenge au Makunguru, kule Majengo, Nonde n.k
Sasa mkuu zile nyumba zina shida gani? Labda wawaambie wapige lipu ila zile nyumba ni bora na ngumu balaa. Zingine zina miaka zaidi ya hamsini
 
Sasa mkuu zile nyumba zina shida gani? Labda wawaambie wapige lipu ila zile nyumba ni bora na ngumu balaa. Zingine zina miaka zaidi ya hamsini
Nadhani ingeshauriwa watumie matofali ya kuchoma hala kama wasipochapia (piga lipu)...Na ujenzi wa hayo matofali choma uwe uniform na smart.

Ukienda nchi kama Zambia, Zimbabwe na nyinginezo za kusini mwa Afrika, nyumba zao nyingi hutumia hizo tofali choma lakini hujengwa vizuri kiasi kwamba hata huwa hawachapii...

Hata nchi za Ulaya, Australia na Amerika, mathalani ukiwa Chicago nyumba nyingi zimejengwa kwa kutumia hizo tofali (ingawa kwa wazungu structure ya nyumba huwa ni mbao) kwa nje wapo wanaojenga hizo tofali kufunika structure ya mbao.

 
Mbeya tofali za kuchoma huwa zinapukuchika. Hazidumu. Zile za Rungwe na Mbozi ndiyo ngumu. Huwezi amini ila kuna watu wanauwezo wa kujengea hizi za kuchoma lakini wanatumia za tope sababu ya uimara.
 
Namuunga mkono katibu tena wamechelewa sana haiwezekana jiji kuwa na nyumba nyingi za udongo tena mjini kabisa. Mbeya mji mkubwa sana lakini ukianza kutafuta nyumba za kupanga ndio utashangaa nyumba nzuri hazipo kila nyumba unayopelekwa na dalalali utakuta either ya udongo, haina rangi au tiles yaani Mbeya ni jiji la tofauti sana.
 
90% ya nyumba nyingi jijini Mbeya zimejengwa Kwa tofali mbichi na matope na kupigwa plasta na cement na rangi. Jiji la ajabu kuwahi kutokea Tanzania
 
Mtunguja, umenikumbusha ukiwa Barabarani kutokea bwanga wakati unaingia chato
 
Namkumbuka Mkuu wa Mkoa wa Mbeya enzi za Mkapa Ndugu Mateo Qaresi, lilipotokea Tetemeko na kuangusha nyumba za Wakazi akaibuka na kulitetea Tetemeko kuwa halikuwa kubwa ki hivyo sema wakazi wana vijumba dhaifu hadi Kuku akiwa ndani akapiga teke basi kuta zinaweza shuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…