Mbeya: Wenye nyumba za tope mjini kuhamishwa

Mbeya: Wenye nyumba za tope mjini kuhamishwa

Hizo nyumba ziko mbeya maeneo gani
Blok t,forest,blok q,uhindini,ghana au

Ova

Labda Soko Matola , halafu wakati yeye anasema ni aibu awashauri wenzake wapunguze bei ya cement, nondo, mabati ili watu wajenge haraka
 
Kwa hili nawapa heko, nilishangaa kuona nyumba za tope mjini ndani, yaani CBDA ya mji mkuu wa Dodoma, zimesimama pembeni mwa majengo ya maghorofa ya miji....

147078419_2201935233279842_6514764227527779856_n.jpg

WENYE NYUMBA ZA TOPE MBEYA MJINI KUHAMISHWA
HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya imeagizwà kuwahamisha watu ambao nyumba zao hazipo kwenye mpangilio wa mipango miji na kuwapatia viwanja vingine pembezoni mwa mji.
Agizo hilo lilitolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja wakati akizungumza na Madiwani pamoja na watendaji wa halmashauri hiyo katika mkutano wa Baraza la Madiwani.
Mtunguja alisema jiji la Mbeya bado haliendani na hadhi ya kuitwa jiji kutokana na hali ilivyo kwenye mpangilio wa makazi.
“Niaibu sana kuona mpaka leo hii eti ukipita katikati ya mji kuna nyumba za tope, kila Nyumba na langi yake, halafu jiji mnawatalaam wa mipangomiji ambao wanaweza kushauri namna bora ya kupanga makazi yetu na tukawa na jiji linalo vutia kama ilivyo majiji mengine,” alisema.

The look in Nairobi
Kibera_Nairobi_Kenya_slums_shanty_town_October_2008.jpg

Bado zipo!
 
Agizo hilo limetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mh. Mariam Mtunguja alipokuwa anazungumza na madiwani na watendaji wa Halmashauri hiyo katika Mkutano wa Baraza la Madiwani .

"Ni aibu sana kuona mpaka leo hii eti ukipita katikati ya mji kuna nyumba za tope " Alisema .
Kwa kweli wananchi wa Mbeya wako nyuma sana katika kujenga nyumba bora.
Hilo siyo siri.
 
Naunga mkono hoja, waende matundasi, mamba A huko au mtanila kabisa.
 
Ile Simike yote zile nyumba si ni tofali za udongo zile hazijachomwa...

Kule Nzovwe, mitaa ya nyuma ya Mafiat hapo sijui wanakuita Mwenge au Makunguru, kule Majengo, Nonde n.k
Sasa mkuu zile nyumba zina shida gani? Labda wawaambie wapige lipu ila zile nyumba ni bora na ngumu balaa. Zingine zina miaka zaidi ya hamsini
 
Sasa mkuu zile nyumba zina shida gani? Labda wawaambie wapige lipu ila zile nyumba ni bora na ngumu balaa. Zingine zina miaka zaidi ya hamsini
Nadhani ingeshauriwa watumie matofali ya kuchoma hala kama wasipochapia (piga lipu)...Na ujenzi wa hayo matofali choma uwe uniform na smart.

Ukienda nchi kama Zambia, Zimbabwe na nyinginezo za kusini mwa Afrika, nyumba zao nyingi hutumia hizo tofali choma lakini hujengwa vizuri kiasi kwamba hata huwa hawachapii...

Hata nchi za Ulaya, Australia na Amerika, mathalani ukiwa Chicago nyumba nyingi zimejengwa kwa kutumia hizo tofali (ingawa kwa wazungu structure ya nyumba huwa ni mbao) kwa nje wapo wanaojenga hizo tofali kufunika structure ya mbao.

54a4c8a4-2281-4675-9e3f-85b8d370d9f4.jpg
 
Mbeya tofali za kuchoma huwa zinapukuchika. Hazidumu. Zile za Rungwe na Mbozi ndiyo ngumu. Huwezi amini ila kuna watu wanauwezo wa kujengea hizi za kuchoma lakini wanatumia za tope sababu ya uimara.
 
Namuunga mkono katibu tena wamechelewa sana haiwezekana jiji kuwa na nyumba nyingi za udongo tena mjini kabisa. Mbeya mji mkubwa sana lakini ukianza kutafuta nyumba za kupanga ndio utashangaa nyumba nzuri hazipo kila nyumba unayopelekwa na dalalali utakuta either ya udongo, haina rangi au tiles yaani Mbeya ni jiji la tofauti sana.
 
Agizo hilo limetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mh. Mariam Mtunguja alipokuwa anazungumza na madiwani na watendaji wa Halmashauri hiyo katika Mkutano wa Baraza la Madiwani.

"Ni aibu sana kuona mpaka leo hii eti ukipita katikati ya mji kuna nyumba za tope " Alisema.
90% ya nyumba nyingi jijini Mbeya zimejengwa Kwa tofali mbichi na matope na kupigwa plasta na cement na rangi. Jiji la ajabu kuwahi kutokea Tanzania
 
Agizo hilo limetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mh. Mariam Mtunguja alipokuwa anazungumza na madiwani na watendaji wa Halmashauri hiyo katika Mkutano wa Baraza la Madiwani.

"Ni aibu sana kuona mpaka leo hii eti ukipita katikati ya mji kuna nyumba za tope " Alisema.
Mtunguja, umenikumbusha ukiwa Barabarani kutokea bwanga wakati unaingia chato
 
Namkumbuka Mkuu wa Mkoa wa Mbeya enzi za Mkapa Ndugu Mateo Qaresi, lilipotokea Tetemeko na kuangusha nyumba za Wakazi akaibuka na kulitetea Tetemeko kuwa halikuwa kubwa ki hivyo sema wakazi wana vijumba dhaifu hadi Kuku akiwa ndani akapiga teke basi kuta zinaweza shuka
 
Back
Top Bottom