Mbinu nayotumia kumlea mwanangu anayesoma private awe mjanja, awe na furaha, asigeuke kuwa kuku wa kisasa

Safi Sana hongera kwa kutuandalia amiri Jeshi mkuu asiejua kulemba lemba, kazi kazi.


Acha hao wazazi wanaowapakia asali kwenye soseji watoto wao waje kuvuna wanachokipanda Sasa hivi. Mtoto inabidi awe ngangari .. Yuko flexible kwa mazingira yoyote hata akisikia corona ndio kwanza anapandwa na mzuka wa kuikabili , sio mitoto ya ushuani ikisikia corona inajificha chini ya uvungu na kulegeza Sana eti "Daddy I'm gonna Die" huku akirembua.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mtoto anaandaliwa kuja kuishi huo ulimwengu wa matusi kwanini unamzuia kuyasikia ?? , Kama ana umri mkubwa muongoze kujua hayo ni matusi hapaswi kuwa na hiyo tabia ila sio wewe kumzuia asiyasikie tunakosea maana mwisho wa siku watoto watakuja kuishi ulimwengu huu huu uliojaa kila aina ya uchafu, kazi yetu ni kuwaonesha na kuwachambulia au kuwaonesha huo uchafu wasiushiriki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una kiwango kidogo Sana cha fikra

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunafanana kidogo, mi mwanangu yupo grade 3, akiwa likizo namfunza Javascript for kids ambayo baada ya muda ataanza ku develop cartoons na baadae web. Big up.
Hiyo unaipata wapi mkuu? Nataka nijenge misingi ya watoto wangu wote wakiwa wadogo
 
Udhaifu wa malezi usiwe sababu ya kunyooshea kidole fani nyingine. Jifunze kuweka mizania kwenye kila jambo, usidhani huko anakoshinda akiogelea na kuruka sarakasi ndio yuko salama sana. Labda hujui maana ya malezi, huko huko wapo wavuta bangi, mateja, majizi n.k.

mambo yote yafanyike kwa kiasi na pia chini ya uangalizi. Usifurahi sana kwamba mwanao ni mjanja kupita wanafunzi wote shuleni ama darasani kwao, bali furahi kwa sababu anakua katika tabia njema huku akiwa na moyo wa kujifunza. By the way, mtoto ambaye miezi kumi anakuwa shuleni boarding na wanafunzi wenzake bila computer anaweza vipi kuwa anti social? Huoni kwamba hiyo logic yako iko flawed?
 
Mkuu, huyu mdau anafikiri watoto wanashinda kutwa kucha kwenye kompyuta. Ni mtazamo hasi kwani mtaani watoto wengi wanaharibika kwa kuiga tabia zisizofaa, kila kitu kifanyike kwa kiasi. Mimi mwanangu nishasema ni mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya kutwa, sasa sijui huko anajifungia peke yake?
 
Hapo nmekusoma sana mzee kwenye hio point yako "usifurahi sana kwamba mwanao ni mjanja kupita wanafunzi wote shuleni ama darasani kwao, bali furahi kwa sababu anakua katika tabia njema huku akiwa na moyo wa kujifunza", Kuna jambo la ziada imebidi nikubali tu liniingie.

Ohh kumbe yupo boarding hapo sawa, Computers zipo very very adictive, Nina rafiki yangu nakumbuka aikuwa hacker aisee ni balaa, anaweza kukaa ndani siku 3 huko anafanya dumoing za mizigo ya sql, n.k ni addictive sana maana mtu akijua html atataka ajue css akijua hio atataka ajue java script, before you know it kaanza kuwa addictive sana, Ila sio wote. Kwa ushauri wangu naona utafute vijana wa IT hawa ambao wamehitimu ila hawana kazi, wengi wapo nondo kwenye coding ukiwalipa hata 50 per week hawana tatizo

Kwa clarity tu kwenye paragraph yako ya kwanza, Mtoto wangu hashindi na watoto wowote tu wasio na mbele wala nyuma, Hapo nje kidogo ya mji anapokwenda nina historia na wazazi wa watoto wengi ambao ni marafiki zake mtoto wangu, Life la huko lipo kijamii sana maana muda mwingi watu wapo majumbani sio kama huku mijini hata kujua a to z za mtu fulani ni kazi
 
Mkuu unafanana na mimi
Mimi licha ya mzee kuwa mjeda na mkaksi alitufungia sana ndani. Japo mpira nilikua na kipaji ila mzee alinikazia kwenda academy ng'ambo. Ila nilikua sijui kuogelea, kuchinja kuku, kukata kuni, kupika na mengineyo.

Nimekuja kubadilika ukubwani japo kuna mambo nalipia gharama zake. Yaani nimejifunza sana aisee...binti yangu ninamkuza tofauti sanasana. Namjengea uwezo wa aina yake.
 
Umenena vizur....
 
Una kiwango kidogo Sana cha fikra

Sent using Jamii Forums mobile app
Yuko sahihi kabisa. Huenda we ndo unakiwango kidogo cha fikra

Malezi ya mtoa mada ni ya lower class na middle class, yanamsaidia mwanae kukopi na huko huko middle class kwake na lower class kwake.

Mwanangu wa baadae eti nije kumuexpose muda wote sijui kwa bibi kwa mjomba kwa shangazi kwa watoto wa mtaa nisiojua malezi yao wala akili zao ni Noo kubwa, maana najua influence kubwa kwa mtoto kutoka kwa watu anaohusiana nao, wanamtendea vipi?! Anapitia experince zipi?! Ni za muhimu au ni garbage za kuja kumuathiri kiakili huko mbele!!
Watu maskini na wa kati ndo huwa na muda sana na ujinga mwingi wa kujua jua watu na marafiki wasio na tija maana hawana individual identity ila identity ya mtaa mara ooh kijijini kwetu mara ooh wilayani kwetu, wanataka wamjue kila mtu na wamzoee kila mtu maana hawajitegemei

Upper class hawana marafiki ila wanaconnection. Wanakutana na watu wa class yao tu, hayo yote sijui social skills wanafundishwa na proffessional mentor na wanasocialize within their class na ndio wanalead uchumi na hata nchi pia.Na wengi wapo mentally strong kutoka na exposure kubwa ya watu wa hali ya juu na Dunia kwa ujumla.Na wala hawawafungii watoto bali wana limit na mipaka, wanawapa watoto wao nafasi ya kuwa exposed kwa watu wa class yao marafiki wa class yao,na kwenda sehemu za class zao na hivyo wewe wa kawaida sio rahisi kuwaona, hawaendi endi tu eti kwa jirani, eti mtaani eti kisa tu ni kwa jirani au ni mtaani, hawahusiani na watu wasiowajua kiundani.

Kuwafungia ndani ya geti watoto anakokumaanisha mtoa mada labda ni yale maget kali yale middle class family na lower class family. Unakuta nyumba ipo katikati ya tandale lakini yenyewe tu ndo nzuri na inageti kwa hiyo wazazi wanaoishi humo watakua na akili za kitandaletandale zile hawalei chochote ila wanasema wanalea, zile mtoto anaamka anavaa anaenda shule anakula analala kesho yake mzunguko unaendelea hivyo hivyo, yaani mzazi hana muda na mtoto wala hana muda wa kuinteract na mtoto, akimpeleka tuition ni zile tuition za kemia historia jiographia, yaani anasoma ya darasani tu. Mtoto hampeleki hata tour ndani ya nchi/nje ya nchi kumfundisha vitu vya muhimu au kumsajili kwenye madarasa ya muhimu. Huyo anafuga halei, matokeo yake ndo anafikiri sasa kumfungulia mtoto ni kumfungulia kwenda kucheza na watoto wa mtaani eti ndo watamfundisha na kumfanya awe mjanja.
 
dudu jeupe,
Vipi Kama wapo swimming club za shule home Wana jifunza karate na mafunzo ya ukakamavu, wanakwenda kucheza tenesi na wenzao wa gate Kali...

Yaani sijakuelewa unataka wacheze na watto wa mitaani, Yaan wale watoto wasio na heshima Wana matusi mazito na tabia mbovu na adabu chafu...Aisee Bado ujanishawish wewe mlee mtoto Wako hivyo alafu siku akutane na junior wangu Yaan nikumuacha kwako utamrudisha mwenyewe maana utundu wake umepitilizaa... Point yangu ni kwamba sio kila mtoto wa geti kali ni boya au zoba Inategemea na malezi ya wazazi...Acha kukarir..mkuu
 
na muda mrefu kukutana na mtu makini hivi ,hebu nisanitize mikono afu ntachangia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…