cocastic
JF-Expert Member
- Nov 30, 2019
- 96,456
- 156,324
Hongera kwa hilo baba mlezi, namtakia mafanikio mema huyo chalii wako.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu mtoto anaandaliwa kuja kuishi huo ulimwengu wa matusi kwanini unamzuia kuyasikia ?? , Kama ana umri mkubwa muongoze kujua hayo ni matusi hapaswi kuwa na hiyo tabia ila sio wewe kumzuia asiyasikie tunakosea maana mwisho wa siku watoto watakuja kuishi ulimwengu huu huu uliojaa kila aina ya uchafu, kazi yetu ni kuwaonesha na kuwachambulia au kuwaonesha huo uchafu wasiushirikiUpo sahihi,lkn mimi huwa namchanganya pia kitaani,mfano huwa naenda nae mazoezin asubuh uwanjan ambapo ni mchangani na akifika hapo anacheza mpira na watoto wa shule za kata. Hii imenifanya kuona tofaut yake yeye na hao watoto, yeye anakosa ushapu lkn siku zinavyokwenda anabadilika. Nisichopenda kwa watoto wa kata ni tabia mbaya kama matusi nk, sasa nikiwepo wanaogopa kutoa hayo maneno ya ovyo.
Una kiwango kidogo Sana cha fikraTafuta peasa jomba hayo yote sijui kubinuka sarakasi, kutjifunza kutega ndege, kuogelea kwenye mabwawa ya kichocho ni umaskini tu.
Familia zenye uwezo huwezikuta na hizo mabo kaka .Mo Dewj ampeleke mwanae kutega ndege sijui sarakasi za kinyumenyume mtaani wakati wataalam wa hizo mambo wapo ni uwazimu.
Pesa ikiwepo shule unachagua mwenyewe. Mbona watoto wanakwenda matour mpaka nje yanmipaka ya nchi achilia vivutio vya humu nchini?
Pesa ikiwepo mtoto anapata exposure ya kutosha tofauti na wakwako anaeshinda anawinda ndege na sarakasi za kinyume nyume bila skills.
Tunaeapeleka watoto kwenye training za kuogelea, marshal art ili baadae ziwe fursa ya kujipatia pesa. Sasa wewe wa kwako anashinda anaogelea matopeni na kupauka inaishia hapo hawezi kushiriki hata mashindano ya kuogelea, kukimbia, marshal art kwa sababu hana skills za kutosha na hajilui rules.
Hana networks zaidi ya wahuni wa mtaani kwao, hana exposure zaidi ya mtaani kwake na bibi ake, hajawai kwenda tour ya maana zaidi ya kwenda porini kuwinda panya.
Yawezekana we ndo kwanza umeanza kuzaa na huyo ndo mtoto wako wa kwanza . Nimekuuliza malezi hayo pia ni kwa mtoto wa kike? Hukujibu.
Kuhusu mtoto kuwa kwenye kumi Bora darasani naona na wewe umekaririshwa kwamba akili inaanzianmoja mpaka kumi, pole sana.
Wenzako hatuagalii hayo manamba bali tunaangalia mtoto anapata nini, amekosa nini, anajua nini, anaweza nini, anapenda nini na anakipaji gani ili aendelezwe huko. Huwezi lazimisha mtoto awe eti kwenye kumi Bora ndo uone ni mafanikio, kumbuka kuna ngazi za elimu hakuna hizo mambo ulizo karirishwa eti kumi bora.
We unadhani hao waliofanikiwa walikuwa kwenye 10 bora? Pesa ikiwa ya mawazo mau ya uganga ndo utakuwa na kuishi katika mawazo ya karne ya 15 wakati dunia inakimbilia karne ya 22.
Nasisitiza, tafuta pesa acha kumtesa mtoto eti azoee maisha halisi.
Kwanini umtabirie mtoto maisha ya kimaskini. Basi hata viatu usimnunulie mwache atembee pekupeku maana ndo maisha halisi ya huko kijijini mnakoishi.
Mwisho jukumu la kulea na kufunza ni lako mzazi, hizo mambo ya kwa bibi ni kukimbia majukumu.
Lazima mzazi aweze kubaini kuwa mtoto anatakiwa afundishwe changamoto za dunia ya sasa na mwelekeo wa dunia ijayo.
Sasa we mshindishe kwa bibi yake afundishwe kutega mitego ya panya eti ndio ujanja tuone itamsaidia nini akisha fahamu.
Usikariri maisha ya kimaskini bro. Tafuta faranga!
Sent using Jamii Forums mobile app
Hata sijui kwanini aisee, mtoto anarudi nyumbani kachoka balaaSijaelewa sababu ya watoto kukaa shule hadi saa 10.
Mbona shule za IGCSE na IB hawasomi hadi huo muda?
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisa swahibaAhsante Swahiba.
Mleta uzi kaamua kizuri kula na nduguze hapo ni kuangalia kilicho bora basi tuchukue na kufanyia kazi.
Hiyo unaipata wapi mkuu? Nataka nijenge misingi ya watoto wangu wote wakiwa wadogoTunafanana kidogo, mi mwanangu yupo grade 3, akiwa likizo namfunza Javascript for kids ambayo baada ya muda ataanza ku develop cartoons na baadae web. Big up.
Udhaifu wa malezi usiwe sababu ya kunyooshea kidole fani nyingine. Jifunze kuweka mizania kwenye kila jambo, usidhani huko anakoshinda akiogelea na kuruka sarakasi ndio yuko salama sana. Labda hujui maana ya malezi, huko huko wapo wavuta bangi, mateja, majizi n.k.Ntaka nikupe taarifa tu, Hakuna watu ambao wapo very socially awkard kama watu wanao deal mno na computers, kuanzia hackers, software developers, n.k hawa watu asilimia kubwa mno wapo socialy awkard na ninakupa homework ufanye research,
Muwe mnawatoa toa nje watoto wenu wasishinde ndani Hayo mambo ya kujifunza lugha za computer hizo mlizozitaja ama kukesha sana na pc yanaanzaga kutenegeneza uraibu flani hivi wa kuwa na pc muda mwingi na kujitenga na jamii, Ndio maana maisha ya programmers, online workers, gamers, internet trolls, web developers wengi yanakuaga ni lonely sana na kuanza kusingizia anti social na intrivert kumbe ni maisha wanayoishi
Nawashauri watoto wenu wafanye shughuli za nje ya nyumba kuliko kukaa kaa ndani, Hayo mambo ya java script, html, n.k naona tuwaachie wenzetu wazungu ambao ni wapweke mno rafiki zao ni mbwa, Ila kama utamfundisha hakikisha ana muda wa ku participate kwenye mambo ya social.
Huyu wangu saizi kawa muongeaji na mcheshi sana na pia anaruka sarakasi na bora iwe hivi kuliko awe introverted geek
Mkuu, huyu mdau anafikiri watoto wanashinda kutwa kucha kwenye kompyuta. Ni mtazamo hasi kwani mtaani watoto wengi wanaharibika kwa kuiga tabia zisizofaa, kila kitu kifanyike kwa kiasi. Mimi mwanangu nishasema ni mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya kutwa, sasa sijui huko anajifungia peke yake?Upo sahihi,lkn mimi huwa namchanganya pia kitaani,mfano huwa naenda nae mazoezin asubuh uwanjan ambapo ni mchangani na akifika hapo anacheza mpira na watoto wa shule za kata. Hii imenifanya kuona tofaut yake yeye na hao watoto, yeye anakosa ushapu lkn siku zinavyokwenda anabadilika. Nisichopenda kwa watoto wa kata ni tabia mbaya kama matusi nk, sasa nikiwepo wanaogopa kutoa hayo maneno ya ovyo.
Hapo nmekusoma sana mzee kwenye hio point yako "usifurahi sana kwamba mwanao ni mjanja kupita wanafunzi wote shuleni ama darasani kwao, bali furahi kwa sababu anakua katika tabia njema huku akiwa na moyo wa kujifunza", Kuna jambo la ziada imebidi nikubali tu liniingie.Udhaifu wa malezi usiwe sababu ya kunyooshea kidole fani nyingine. Jifunze kuweka mizania kwenye kila jambo, usidhani huko anakoshinda akiogelea na kuruka sarakasi ndio yuko salama sana. Labda hujui maana ya malezi, huko huko wapo wavuta bangi, mateja, majizi n.k.
mambo yote yafanyike kwa kiasi na pia chini ya uangalizi. Usifurahi sana kwamba mwanao ni mjanja kupita wanafunzi wote shuleni ama darasani kwao, bali furahi kwa sababu anakua katika tabia njema huku akiwa na moyo wa kujifunza. By the way, mtoto ambaye miezi kumi anakuwa shuleni boarding na wanafunzi wenzake bila computer anaweza vipi kuwa anti social? Huoni kwamba hiyo logic yako iko flawed?
Mkuu unafanana na mimiHata kuwa shoga kabisa...... Lazima mtoto mfundishe mazingira yote yote.
Mimi sifurahii mazingira niliyolelewa yaani sijui kucheza mpira, sijui kuogelea, sijui kucheza draft wala bao, sio shabiki wampira aina yoyote yaani nipo ipo2 kidogo tena kidogo sana kwenda club au live band
Sent using Jamii Forums mobile app
Umenena vizur....Tafuta peasa jomba hayo yote sijui kubinuka sarakasi, kutjifunza kutega ndege, kuogelea kwenye mabwawa ya kichocho ni umaskini tu.
Familia zenye uwezo huwezikuta na hizo mabo kaka .Mo Dewj ampeleke mwanae kutega ndege sijui sarakasi za kinyumenyume mtaani wakati wataalam wa hizo mambo wapo ni uwazimu.
Pesa ikiwepo shule unachagua mwenyewe. Mbona watoto wanakwenda matour mpaka nje yanmipaka ya nchi achilia vivutio vya humu nchini?
Pesa ikiwepo mtoto anapata exposure ya kutosha tofauti na wakwako anaeshinda anawinda ndege na sarakasi za kinyume nyume bila skills.
Tunaeapeleka watoto kwenye training za kuogelea, marshal art ili baadae ziwe fursa ya kujipatia pesa. Sasa wewe wa kwako anashinda anaogelea matopeni na kupauka inaishia hapo hawezi kushiriki hata mashindano ya kuogelea, kukimbia, marshal art kwa sababu hana skills za kutosha na hajilui rules.
Hana networks zaidi ya wahuni wa mtaani kwao, hana exposure zaidi ya mtaani kwake na bibi ake, hajawai kwenda tour ya maana zaidi ya kwenda porini kuwinda panya.
Yawezekana we ndo kwanza umeanza kuzaa na huyo ndo mtoto wako wa kwanza . Nimekuuliza malezi hayo pia ni kwa mtoto wa kike? Hukujibu.
Kuhusu mtoto kuwa kwenye kumi Bora darasani naona na wewe umekaririshwa kwamba akili inaanzianmoja mpaka kumi, pole sana.
Wenzako hatuagalii hayo manamba bali tunaangalia mtoto anapata nini, amekosa nini, anajua nini, anaweza nini, anapenda nini na anakipaji gani ili aendelezwe huko. Huwezi lazimisha mtoto awe eti kwenye kumi Bora ndo uone ni mafanikio, kumbuka kuna ngazi za elimu hakuna hizo mambo ulizo karirishwa eti kumi bora.
We unadhani hao waliofanikiwa walikuwa kwenye 10 bora? Pesa ikiwa ya mawazo mau ya uganga ndo utakuwa na kuishi katika mawazo ya karne ya 15 wakati dunia inakimbilia karne ya 22.
Nasisitiza, tafuta pesa acha kumtesa mtoto eti azoee maisha halisi.
Kwanini umtabirie mtoto maisha ya kimaskini. Basi hata viatu usimnunulie mwache atembee pekupeku maana ndo maisha halisi ya huko kijijini mnakoishi.
Mwisho jukumu la kulea na kufunza ni lako mzazi, hizo mambo ya kwa bibi ni kukimbia majukumu.
Lazima mzazi aweze kubaini kuwa mtoto anatakiwa afundishwe changamoto za dunia ya sasa na mwelekeo wa dunia ijayo.
Sasa we mshindishe kwa bibi yake afundishwe kutega mitego ya panya eti ndio ujanja tuone itamsaidia nini akisha fahamu.
Usikariri maisha ya kimaskini bro. Tafuta faranga!
Sent using Jamii Forums mobile app
Yuko sahihi kabisa. Huenda we ndo unakiwango kidogo cha fikra
sijakusoma mkuu
na muda mrefu kukutana na mtu makini hivi ,hebu nisanitize mikono afu ntachangiaNilistuka mapema sana juu ya madhara ya kusomesha watoto hizi private, unakuta mtoto anatoka saa 10 jioni, akitoka hapo ni tuition, akitoka hapo ni homework na wengi hawatoki nje ni geti kali ni ndani tu hii inahirbu sana maisha ya mtoto.
Pia Malezi ya siku hizi pia yamechangia mno kuwafanya watoto wawe mazube maana watoto ni kuwafuga kama kuku ndani ya mageti (geti kali) huku wazazi wengi wakijidanganya kwamba wanapata furaha kamili kwa katuni na kunanunulia games.
Nakumbuka zamani tukitoka shule tulikua hatukai ndani ucheza games au kuangalia katuni, Tulikua na vikundi vya watoto mitaani tunacheza mpira, kuogelea na hata kujifunza kuto onewa hovyo hovyo, dada zetu walicheza rede, kupika, n.k Hii michezo na maisha haya yalifanya tujue kuishi na jamii tofauti na siku hizi unakuta litoto linachojua na games, katuni na what is water. ukimpeleka huyu mtoto nje kuna uwezekano mkubwa wa yeye kuonewa na hata kuwa mpweke asiwe na marafiki maana hajui ku interact na watu (Hili tatizo ni kubwa ulaya).
Binafsi mtoto wangu wa kiume namsomesha english medium hizi, mara ya kwanza shule niliyompeleka walikua darasani 18 tu na wanatoka saa kumi, kwa huu uchache nakumbuka alikuwa ana rafiki moja tu na muda mwingi ulikuwa ni kusoma hadi saa kumi.
nikaona huu upuuzi sasa, shule ndio ni muhimu ila sio kila kitu kwa mtoto wangu kuna maisha mengi mno anayopaswa kujifunza, Nikamwamishia shule ambayo wapo 48 darasani na wanatoka saa saba na nusu ila tu darasa la saba tu ndio wanatoka saa tisa. Yeye yupo darasa la tatu shuleni huwa yumo kumi bora na hii inatosha kwangu siamini sana mambo ya kuwa wa kwanza.
akitoka shuleni anakula, anafua nguo zake, Zamani nilikuwa nimempiga geti kali ila baada ya hapo nikaanzisha utaratibu anapelekwa nje kidogo ya mjini kwa bibi yake ambako kawa na marafiki wanaocheza nae, kuogelea nae, kuwinda nae, n.k Pia kajufunza kuchinja kuku na kusonga ugali wake.
Siku hizi kawa muongeaji mno nlivyomwanzishia huu utaratibu, Kawa mjanja, Shuleni kwao kageuka kuwa aina ile ya mwanafuzni darasani ambae kila mwanafunzi anataka kuwa rafiki yake na nadhani hii ni kwasababu huwa anawapa stori ama kuwafundisha wenzake vitu alivyofundishwa au alivyofanya huko kwa bibi yake,
Shule aliyopo ni yeye peke yake anaweza kuruka zile sarakasi za nyuma basi wenzake wanamkubali sana,
Nimeitwa shuleni kwa kesi za utundu utundu huu wa wavulana kama kupiga kelele na kutania wasichana, Binafsi ndivyo navyotaka awe mchangamfu na nikiri tu nilifurahi hizi kesi japo nilimkanya kwa shingo upande , Sitaki mtoto azubae zubae
Sijamlipia school bus kwa maksudi kabisa japo nina uwezo, nilishangaa aliponiambia wenzake pia shuleni wanapenda sana wawe wanatembea kama yeye pamoja na wenzake wawili ambao hawajalipiwa school bus 🙂🙂
Michezo ambayo kuku wa kisasa wanaofungiwa ndani ambayo hawataijua
-Kutengeneza manati, kuwinda ndege porini ,shabaha na raha ya kula ulichowinda
-Kuunda magari ya waya au udongo
-Kujifunza kupigana (kuku wa kisasa wanajua kupigana kwenye game)
-Kidali poo
-Kibabababa na kimamamama
-kombolela
-Kushona makambakamba vidoleni na kuyachezesha kwa mitindo mbalimbali
-kujifunza kugawana - ukija na kimbama,kisheti,gimbi au muwa marafiki zako lazima wapate.
-Mchezo wa kuzungusha betri kwa mijeredi
-Kupuliza kimhwepelo
-kukimbiza malingi ya baiskeli
-mpira wa chandimu
-Mchezo wa goroli
Elimu ni muhimu ndio ila mwenyewe nina degree ya uhasibu na CPA nimeajiriwa vizuri tu japo nilikuwa na uwezo wa kawaida tu shuleni ila huku kazini nafanya kazi vizuri tu na kuna wenzangu waliokuwa wanakua wa kwanza darasani hadi leo wamehitimu hawana kazi. Malezi sio kumfungia mtoto na kumbana sana ukiamini ndio njia ya kumlinda , LA HASHA!! kuna siku atakua mkubwa na ataishi maisha yake anaweza kupata changamoto kibao ambazo hakupata nafasi za kukabiliana nazo utotoni.