Mbona Dkt. Mwigulu haeleweki? Yaaani madeni ya sekta binafsi ni ya Serikali? Mmemuelewa Watanzania?

Vitu vingine huwa simuelewagi huyu waziri lakini kwa hili nimemuelewa ingawa mm sio mchumi..
 
Mkuu Kama shule ilikupiga kusho huwezi elewa chochote. Hii ni lecture ya mwaka wa pili wanaodoma B.A economics au finance.

National debt= public debt + private companies' debts.

Hivyo alichosema mwigulu ndoshule yenyewe.
Wewe ulikariri

Dhamana ndio mpango mzima
 
Duh aisee yako mengi siyajui kumbe...sasa nauliza wenyewe wakiko

pa wanaweka nini bondi au ndo vitu walivyowekeza?ebu wataalam wa masuala ya uchumi tutoeni tongotongo
Definition ya national debt:
"The total amount of money which a country's government has borrowed."
 
Kwanini Asiseme DENI la Serikali ni Tri. 71 na Deni la Sekta binafsi ni Tril.20 kuliko kusema Deni la Serikali ni Tril.91 wakati Serikali atalipa lake na Sekta binafsi itakipa lake
 
Hao wanatuchanganya tu tatizo na bungeni hatuna watu makini huyu ilikua anapigwa maswali mpaka anaeleza ukweli.
 
Haeleweki kivipi ? Haujui ya kua kuna private sector wanakopeshwa na banks na tahasisi tofauti nje ya Nchi masharti ni kwamba serikali inawadhamini, madeni wanalipa hao waliokopeshwa
Sasa inakuaje deni ni la serikali
 
Kwahiyo vile alivyokuwa anasema nchi itapigwa mnada kutokana na madeni alikuwa anamaanisha madeni ya Sector binafsi [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu Kama shule ilikupiga kusho huwezi elewa chochote. Hii ni lecture ya mwaka wa pili wanaodoma B.A economics au finance.

National debt= public debt + private companies' debts.

Hivyo alichosema mwigulu ndoshule yenyewe.
Wasomi njaa pumbavu ndio maana mnaishia kuajiriwa mnalipwa milion 1 umasikini uumewajaa.

Endelea kukariri hivyo vitini vya nyambari
 
Baada ya muda mrefu sasa umekuha na mswali ambayo ya jadilika kimantiki. Heko kwako.
 
Mimi, kwa mara ya kwanza, naomba nimshukuru kwa kutoa ufafanuzi huo, hii igalao inatoa mwanga kidogo kuliko tuliyozoea ya gizani.

Ningeshukuru ufafanuzi wake ungeeleza pia inakuwaje kukopa kwa sekta binafsi, madeni hayo yanajumuishwa kwenye deni la taifa; bila shaka ni kutokana na 'guarantee' inayotolewa na serikali kwa sekta hiyo?

Pili, yeye kama waziri, na pia mtaalam wa mambo haya, siyo sahihi kabisa kuleta taarifa isiyokuwa kamili.
Rough Estimate" ndio kitu gani katika maswala kama haya.

Tatu, kutokana na udhaifu mkubwa uliopo huko serikalini, siyo jambo la kushangaza kabisa waTanzania wakawa ndio wanaobebeshwa kulipa baadhi ya hayo madeni ya sekta binafsi. Hili ninalo wasiwasi mkubwa kutokana na watawala tulionao sasa hivi.
 
Haeleweki kivipi ? Haujui ya kua kuna private sector wanakopeshwa na banks na tahasisi tofauti nje ya Nchi masharti ni kwamba serikali inawadhamini, madeni wanalipa hao waliokopeshwa
Sasa kama wanalipa wao kwann inaitwa deni la taifa, ivi wewe ukimdhamini mtu ameenda kukopa wewe ndo u adaiwa au yeye ndo anadaiwa?

Kwanini ijumlishwe kwenye deni la taifa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…