Niache Nteseke
JF-Expert Member
- Apr 29, 2020
- 2,162
- 2,616
Ulitambuaje kiongozi tufungue kidogo.Siwatetei, bank ni wezi, ila huyu ameketa kwa kutoitaja hiyo bank.
Mimi bank waliwahi pita na hela yangu ya kwenye account, ila waliirudisha. Walidhani nisingetambua
Beba mashine ya kuhesabia pesa , unaenda nayo mpaka Dirishani...Bank Teller anahesabia Hela Kwa mashine, halafu Mimi nihesabie manually si nitatumia muda mwingi? Basi waweke mashine ya kuhesabia Hela Kwa wateja pia
How long does it take to count 10m in 10,000/- notes? Hardly 10 minutes. Now you waste 10 minutes or risk losing your hard earned 50,000/-. The choice is yours.Mkuu yani huakiki kwa kuhesabiwa million 10 si utapoteza muda. Uaminifu kwa watanzania ni zero.
Hata akitoa vibunda unaweza kumwambia ahesabu. Wanaojitambua wanakuuliza tuhesabu tena au?Anapokupa cash teller anatakiwa ahesabu kwa mashine pale na wewe unaona upande wa pili. Kisha, aifunge ndio akupe. Shida ni pale anachukua tu vibunda anakupa.
Unamwambia zihesabu. Atafungua na kuhesabu hana mamlaka ya kukataa. Pale pameandikwa mteja hesabu hela zako kabla hujaondoka kaunta ni haki yako. Na akikwambia sogea wateja wemgine wahudumiwe muoneshe hilo tangazo kuwa uhakika kabla ya kuondoka kaunta.Mkuu, kuna bank ukianza kutoa kuanzia million hata 2 unapatiwa kibunda tayari kimeshapigwa rababendi. Hakihesabiwi kwenye mashine. Utahakiki wewe mwenyewe. Nafuu millioni 2.
Ukitoa kuanzia millioni 10 mpaka 20 mpaka 30 utaitwa ndani utapewa kibunda chako kimeshapigwa utepe wa BOT n.k
Au labda mimi sielewi. Unaweza ukaomba wakuletee mashine uzihakiki pale pale au inakuwaje?
Hivi vijistori vya kutunga vya Twitter ndo unaichukua kama habari ya kureport hapa? Hauko serious bibiSalamu Wakuu,
Nimegundua Suala la uaminifu bado ni changamoto kubwa sana hapa nchini
Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi ya watu kupatiwa fedha pungufu kila wakichukua hela kupitia kwa benki tellers
Katika mjadala unaondelea huko X inaonesha kuna benki ambazo zinahusishwa na tabia hii mbaya. Yaani kwao matukio ya aina hii ni kawaida kwao
Na mara nyingi imekuwa nguvu kwa mtu kugundua kama ameibiwa kwa sababu Watanzania ni wavivu wa kuhesabu hela zao mara baada ya kuwithraw
Swali langu ni je, kwa nini kama benki na tellers wenye tabia hii mbovu hawachukuliwi hatua?
Haya ni malalamiko ya mteja kutoka Mtandao wa X
"Hivi ni mimi tu nikienda bank kutoa pesa kuanzia 10M huwa nakuta pungufu ya noti? Mfano unakuta kibunda kimoja kina noti 96-97 badala y amia? Na imeshatokea zaidi ya mara nne. Kuna siku nikiwa Mafinga napakia mbao nilikuta kwenye kibunda kimoja kimepelea noti 13 badala ya mia, nikajua labda nimejichanganya.
"Leo tena nipo Mafinga napakia mbao nimetoa zaidi ya 12M, jioni nawalipa wenye mzigo kibunda kimoja nakuta kina noti 82 za elfu kumi badala y amia. Jamani inaumiza sana, sitaitaja ni bank gani lakini hii kitu inaniuma sana, kama haijawahi kukupata unaweza hisi ni ungo, ila omba sana isikutokee.
"Noti 97-98 nilikuwa nachukulia kaiwada, ila hii sasa Hapana kwa kweli.
"NB: Huwa natolea bank sio kwa wakala, mtu asije fikiria huwa natoa kwa wakala."
Angetumia dakika 10-15 kuhesabu angeokoa 500,000/-. Tatizo watu kujifanya wamezoea hela.Mwaka 2016 nipo Tanga kaka yangu alikwenda kukopa 12million sasa akabeba ule mzigo mpaka home,na wala hakuhangaika nao.
Sasa kesho akachomoa kibunda akanipa ili niende kwa wakala nimuwekee tigo pesa amtumie mtu,nami sikihangaika kihesabu.
Alcohol,nikampa wakala anahesabu zipo 750,000 badala ya million moja,nikarudi mpaka home nikamwambia huu mzigo haukuenea ikabidi tukaanza kuchambua lile bunda tumekuta 500,000 haipo,maana imekuwa million 11.5
Ni haki yakoKauli zao wanasema HESABU HELA KABLA HUJATOKA KAUNTA.......lakini mazingira sio wezeshi.....
Umejuaje ni milioni 10 kama hujahesabu?Yaani upokee tu bila kuhesabu ukidhani ni milioni 10? Huo ni uvivu wa kufikiri.unahesabuje milioni 10... 😭😭😭
Hahaha, anazificha huko kwenye ushungi wake sivyo?Mambo ya kawaida sana
CRDB BANK KKOO hili tawi la njiani hapa kama unaelekea mnazi mmoja kutokea kongo.
Teller anavaa ushungi
Yule ni utaratibu wake kukata cha juu