Mbowe akiri kuukubali "mziki" wa Rais Samia, agomea wana-Chadema kuingia barabarani, asema ni mihemko

Mbowe akiri kuukubali "mziki" wa Rais Samia, agomea wana-Chadema kuingia barabarani, asema ni mihemko

Halafu kuna nyumbu bado zinaamini Mbowe ni mpinzani.!!
 
Kesha Mbowe., Chadema ime collapse ndani ya mikono ya mama samia, Mbowe hakuwa laini hivi,

Mama kamfutia kesi sasa anamuendesha mbowe anavyotaka

Tanzania bado tunahitaji chama cha upinzani kitakachowakwamua watanzania kutoka kwenye makucha ya ccm., Tutamkumbuka na kumuenzi maalim seif sharif hamad siku zote.,

Mbowe toka aachiwe kutoka jela ashaenda Ikulu mara 5., Tundu lissu naye kalipwa posho zake za ubunge, kafutiwa makesi sasa watanzania na wafuasi waliokuwa na natumaini na chadema si chochote si lolote
Mama anaupiga mwingi Sana
 
Naungana na Mbowe.

Kama utajenga uadui ja Samia, sijui utakuwa unataka nini:

Mimi siyo mpiga debe wala sijawahi kuwa mtetezi wa Rais au CCM, ila kwa hakika, Samia ameonesha uongozi tuliokuwa tunaukosa. Ametuunganisha Watanzania. Ameonesha maana ya kuwa kiongozi ni nini.
 
Watu wanataka waone watu wakifarakana kila siku inasikitisha sana,wote wa Tanzania lengo moja why muwe maadui mzee wa watu hana mambo ya uswahili muacheni!
 
SPIKA WA BUNGE LA WANANCHI MHE CELESTIN SIMBA AKIZUNGUMZA NA WAKAZI YA JIMBO LA KILOMBERO

 
4 June 2022
CLUBHOUSE

PART II : Freeman Mbowe | Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Ameongea na WanaDiaspora~Tanzania Duniani



Source : America swahili news
 
..ukichunguza utagundua kwamba Ccm ni kupe na wanafuja fedha za umma kuliko chama chochote.

..angalia ma-V8 wanayotamba nayo mitaani wakati watoto wetu wanasoma kwa shida, hawana madarasa, na shule hazina matundu ya vyoo.
Mi wala hata siipendi CCM but I think the whole multi-party system in a country like ours is a fucked up system.
 
Mi wala hata siipendi CCM but I think the whole multi-party system in a country like ours is a fucked up system.

..it is fucked up bcoz of Ccm.

..they are the ones who have been gaming the system to favour their party.

..and they scare of and discourage good and competent ppl frm joining other parties.

NB:

..mwaka 2020 wagombea zaidi ya 500 wa udiwani wa Cdm walienguliwa na tume ya uchaguzi.

..wakati huohuo hakuna mgombea hata mmoja wa Ccm ambaye amewahi kuenguliwa na tume tangu tuingie vyama vingi.

..Nakuelewa kabisa unaposema the System is fucked up. Na nafikiri unaelewa ni nani aliyesababisha hali hiyo.
 
Unadhani sijui propaganda za sukuma gang boss? Ni wapi napinga msimamo wa sasa wa CDM kuendana na wanachisimamia sukuma gang? Mimi napinga msimamo wa sasa wa CDM kwa faida ya CDM, sukuma gang wanapinga msimamo wa sasa wa CDM ili kumtakakatisha dhalimu magufuli.
Ni sawa lakini lazima tujiulize, msimamo wa zamani wa CDM umesaidia nini, na katika masilahi mapana ya mabadiliko ya kidemokrasia na maendeleo, tumefanikiwaje? Pia, badala ya kupinga tu msimamo wa sasa wa chama, kwanini tusioneshe njia mbadala!?
Kama ni kuingia barabarani, au kufanya nchi isitawalike kwa migomo na maandamano, ni nani hao watakao hamasishwa washiriki?! Hawa hawa washabiki wa Simba na Yanga?!
Imani ya chama ni kumshawishi kila mtu atusikilize, sasa hivi tunajaribu kushika sikio la, Mazaa na lichama lake! Wakiukubali muziki wetu, kuna shida gani?!
 
Mbowe namuona kwa kasi akifuata njia ya kina Mrema, Cheyo, Lipumba nk. Nimekuwa nikisisitiza sana kuwa Mbowe muda wake wa kuwa mwenyekiti wa CDM umepita. Kimsingi Mbowe alipaswa kujiuzulu au kuachia uenyekiti wa CDM baada ya ile project ya Lowassa kufeli. Ama kama alikuwa anaona aibu kujiuzulu kwa blunder ile ya Lowassa, basi hakupaswa tena kugombea uenyekiti uchaguzi uliopita. Lakini naona alishupaza shingo.

Madhara ya Mbowe kung'ang'ania kukaa madarakani muda mrefu hivi, ndio inapelekea yeye kupoteza ushawishi kwa wafuasi wake. Nashukuru kuwa sasa ametambua kuwa anaanza kupoteza ushawishi kwa wafuasi wake. Kama Mbowe ameamua kuingia kwenye ulaji, ashauriwe Aachie kiti cha uenyekiti kuliko kuipotezea CDM haiba yake.
Kuna muda unafika lazima kuachana na uanaharakati na kufanya siasa zilizokomaa. Ameamua kuachana na mawazo na fikra nyepesi za kupinga kila kitu.

SSH ameonyesha ushirikiano na kupenda siasa za amani, Mbowe kaona hakuna sababu ya kumvimbia kiongozi wa nchi mwenye mawazo chanya na asiye na kiburi.

CCM wanaweza kuwa ni wale wale lakini unatazama nia ya moyoni ya kiongozi mkuu na unaona kabisa uanaharakati haujengi na hauna mwelekeo mwema.
 
Keshapewa asali huyo
IMG_20220602_155959_795.jpg
 
Kuna muda unafika lazima kuachana na uanaharakati na kufanya siasa zilizokomaa. Ameamua kuachana na mawazo na fikra nyepesi za kupinga kila kitu.

SSH ameonyesha ushirikiano na kupenda siasa za amani, Mbowe kaona hakuna sababu ya kumvimbia kiongozi wa nchi mwenye mawazo chanya na asiye na kiburi.

CCM wanaweza kuwa ni wale wale lakini unatazama nia ya moyoni ya kiongozi mkuu na unaona kabisa uanaharakati haujengi na hauna mwelekeo mwema.

Mbowe anaingizwa mjini na bibi wa kikojani!
 
Back
Top Bottom