Mbowe na CHADEMA mnataka kumkwamisha Rais Samia kwakuwa amewalegezea kidogo?


..Raisi afanye harakati za kujenga uchumi.

..Chadema wafanye harakati za katiba mpya.

..Kutuhumiana mambo ambayo hayapo siyo jambo jema.
 
Alituweza sisi pekeyetu au Taifa zima??

Nan alikuwa Ana nafuu??

Sasa ahuen imeanza kuonekana badala ya wao watulie nchi ipate Aman na utulivu wanaanza leta choko choko

Kudai katiba mpya si choko choko.Katiba mpya ni zaidi ya ahueni,Katiba mpya ndio maendeleo halisi.

Fikiria 80% ya wawakilishi hawakuchaguliwa na wananchi,sasa huu ni zaidi ya ukoloni.

Katiba ndio ilimwingiza Samia Ikulu,lazima wakati wowote atii na kufuata katiba vinginevyo hana tofauti na mtangulizi wake.

Ikiwa tulimpinga Mwendazake kwanini leo unashindwa kumpinga Mama ????.

Ukisikia unafiki wa kiwango cha SGR ndio huu.
 

Kama hajakataa kukosolewa kelele zote hizi za nini Chadema wanapomkosoa? Kama hajapinga hoja ya Katiba kwa nini mnaona wanaozungumzia haja ya kuwa na Katiba mpya mapema iwezekanavyo kuwa hawamtendei haki?

Rais aliomba kura kwa wananchi na anatuongoza kwa ridhaa yetu. Rais sio Mungu na sio mzazi wetu bali ni Mtumishi wetu ambae anatakiwa kututumikia kwa kutusikiliza na kututendea haki raia wote wa nchi hii bila ubaguzi wa aina yeyote.

Unasema Katiba ni yenu wakati mnasema kwa sauti kubwa kuwa haimo katika ilani ya chama chenu na sio kipaumbele chenu? Waachane ambao wanaona ni kipaumbele waendelee kuidai na nyie endeleeni kutekeleza vile vilivyomo kwenye ilani yenu.

Amandla...
 
Hapa umesema kweli! Naona siku za Honey Moon za Mama Samia zimefikia mwisho baada ya siku 100. Mbowe anasahau kuwa huo uhuru wa kumjaribu Mama Samia kaupata kwa Samia mwenyewe. Ingekuwa busara kumpa muda kwa vile aliomba "muda kidogo tu". Wengine tumempa muda.
 
Katiba ni mchakato,kwann wanataka jambo hilo kwa kulazimisha??bajeti ya kuliendea jambo hilo wanayo hao chadema??
Inawezekana una hoja ya msingi, cdm wao wameona sasa ni muda muafaka wa kudai katiba mpya, na wanafanya mikutano ya ndani, je unataka wasubiri hisani ya rais, kwani rais na chama chake wana ajenda ya katiba mpya? Hiyo kuingia mtaani wamesema wataingia kesho asubuhi?

Mikutano ya kisiasa ni takwa la kisheria, je kuna tatizo wao kufanya hiyo mikutano? Mbona kuna mikutano ya kidini nchi nzima na haina tatizo lolote, au kwakuwa hiyo mikutano haihatarishi madaraka ya ccm? Kwahiyo unataka watu wote wakae wasubiri hisani ya rais kupata hiyo katiba mpya? Unajua hatari ya kusubiri hisani ya mwanaccm kupata katiba mpya?
 
Hili suala la kumkwamisha Rais ni fikra za kishamba na ujinga huyo aliyezuia mikutano nchi aliipeleka na kuifksha wap????hawa hawatak challenge na Mama kashanogewa ma kiti
 
Mambo ambayo Rais anaweza kuyafanya ili kuongeza imani kwetu kuwa ana dhamira nzuri kuhusu demokrasia katika nchi yetu:
1. Kuvunja Tume ya Uchaguzi na ya Vyama vya Siasa na kuteua watu ambao wanajulikana kwa misimamo yao kuhusu demokrasia.
2. Kutangaza kuwa hatarajii wasimamizi wa chaguzi watapendelea chama chake na wale watakaoonekana kuwa wameleta figisu figisu katika chaguzi yeyote atawashughulikia. Ili kudhihirisha kuwa yuko serious, aunde tume ya kutoa tathmini za chaguzi zilizofanyika chini ya utawala wake na yeyote atakayeonekana kuwa hakutenda haki awajibishwe.
3. Atoe kauli ya kukubaliana na sheria inayoruhusu vyama vya siasa kuendesha shughuli zao sehemu yeyote nchini bila kuingiliwa na mtu yeyote.
4. Aunde tume huru itakayomshauri kuhusu muelekeo wa Katiba Mpya.
5. Akae na viongozi wa vyama makini vya upinzani kuzungumzia kero zao.

Amandla...
 

Ukiachia cdm wanaodai hiyo katiba sasa mpaka wanakuudhi, ww na hao wananchi wengine mtaanza lini kuidai katiba mpya, au ni mpaka rais awaulize mnataka katiba mpya? Unasema kwani cdm wana hela ya kudai hiyo katiba mpya, unatarajia kuna siku itapatikana hela ya katiba mpya bila kusukuma hiyo hela itengwe? Nyie ndio mko huko vijijini mnalipa kodi lakini hamuwezi hata kudai huduma ya maji, zaidi ya kuomba serikali iwasaidie, matokeo yake mnatumia maji machafu, huku watu wanaishi Dar wanazunguka na maVX tu bila tija yoyote.
 
Kumbuka kuwa wao ni wahanga wa kubwa wa matumizi mabaya ya mianya iliyopo na kupelelea kupata athari mbaya na za mojakwa moja kupitia ile iliyopo pale, ilivyoamuliwa kutumika vibaya, Watanzania ni wahanga, wakubwa pia ila athari yake inawafika kila mmoja kwa wakati wake. Mfano hai no chaguzi zilizovurugwa, na kutupatia viongozi wasio chaguo la wananchi.
 
Nashangaa sana nikisoma thread zenu nyie mnaojiita/kuitwa vikongwe wa jf, mnatumia hoja za kitoto sana kupinga kila jambo lenye umuhimu kwa kuhusisha imani zenu, masuaka ya kitaifa hayachagui imani, hii Katiba iliyopo inatukandamiza wote bila kujali imani zetu.

Lakini nyie "vikongwe wa jf" kwa ufinyu wa fikra zenu mnaona bora watanzania waendelee kuonewa ilimradi yule wa imani yenu aliyepo pale ikulu asiguswe, haya mawazo yenu ni ya kijima, kijinga, na yanastahili kupingwa na kila mwenye akili timamu.

Nyie ndio mnaochelewesha maendeleo ya hii nchi kwa mawazo yenu ya kinafiki kwa kuingiza propaganda za kipuuzi kwenye mambo ya msingi ya kitaifa, wacheni huu upuuzi wenu, hakuna mtu mtakayemrudisha nyuma kwa "ujanja" wenu wa miaka ya 90.

Magufuli alipokosea mlikuwa midomo juu kudai anavunja sheria, leo huyu wa kwenu anaharibu mnaingiza "imani" ili kuwatisha watu wasimuonye, kama mnashindwa kuongoza taifa kwa kuona imani zenu ni muhimu zaidi ya maendeleo ya kitaifa, ondokeni serikalini mkajifungie misikitini huko ndiko kunakowafaa.

Mwisho kabisa, sio Mbowe wala Chadema waliomuogopa Magufuli, wangekuwa wanamuogopa wangejifungia ndani wasiseme chochote, kumpinga Magufuli na matendo yake ndiko kulipelekea wao wawekwe rumande kila siku, huu sio uoga ni ujasiri, na huyu wa sasa nae kama amekubali kukaa kwenye kile kiti lazima aambiwe ukweli anapopotoka bila kujali jinsia wala dini yake.
 
Huyu jamaa kawa jinga siku hizi. Hii katiba inayomfanya kiongozi kuwa Kama kimungu fulani ndiyo anaitetea leo? Ataki katiba inayomfanya kiongozi hajue hakifanya kinyume na Sheria atachukuliwa hatua. Nchi ina watu vituko sana hii.
 
Hii haikuanza leo. Ona hapa ni ya tangu zamani, wakiwa na sapoti kubwa ya mabeberu na magazeti ya Kenya kutangazwa hoja zao:

 
Umeshalainika, huo uchumi ataurekebisha mpaka lini?

Chadema program iliyo muhimu kwao kwa sasa ni Katiba Mpya, vipi unataka kuwa divert wafanye wasichokitaka?

Rais kuambiwa ukweli sio kutishwa, wewe ulitaka aambiwe vipi? au ulitaka apigiwe magoti? utampigia vipi magoti mtu anayevunja sheria makusudi?

Ninachoamini, Chadema kama chama wataidai Katiba Mpya kwa kufuata njia zinazokubalika kisheria, iwe kwa mikutano ya hadhara au njia nyingine, hawatalazimisha kuidai Katiba Mpya kwa kuvunja sheria, na kama wakifanya hivyo hata mimi na wengine hatutakuwa upande wao.

Kwa namna hii kama taifa tutasubiri sana kufikia kile tunachokipigania, kama hata wale mnaoonekana mnauelewa wa jambo fulani mnapogeuzwa mawazo yenu kirahisi namna hii tena kwa propaganda za kitoto kabisa.
 

Umeishiwa na hoja sasa umerudia zile hoja zako za kisengerema za Udini na ukabila. Akina askofu Shoo, Bagonza, Mwamakula, Niwemugiz, Kakobe mpaka akasalimu amri, hao walikuwa ni waisilamu enzi za yule dhalimu? Ni kipi ambacho haki kudaiwa enzi za huyo Magu mpaka akaishia kuteka watu, kuwabambikia kesi, kuwaaacha na vilema vya maisha? Unataka kujifanya hukuona ulevi wa madaraka aliokuwa nao dhalimu, bali unataka kuonyesha eti watu walitulia kisa ni mkristo? Kwanza yule hakuwa mkristo, bali shetani aliyekuwa anahudhuria kanisani.

Acha wanaotaka kudai katiba mpya waidai kwa mbinu zao. Nyie mnaotaka kusubiri mpaka siku rais atakuwa tayari kwakuwa ni muisilamu, hakuna aliyewakataza.
 
NDUGU ZANGU UKABILA NA UDINI HAVIWEZI KUTUACHA SALAMA! AWE SAMIA AU MLALA HOI. UDINI NI SUMU! TUMWANGALIE SAMIA KAMA RAIS NA SIO DINI YAKE. TUFANYE HIVYO KWA WOTE WANAOTOA MAONI YAO! TUMPE MAMA YETU BENEFIT OF DOUBT. NI MZOEFU NA LAZIMA ANAJUA NINI NCHI HII INAHITAJI ILI TUWE NA UMOJA. Hizi post za Udini ni hatari!
 
Jokakuu,

With all of my due respect,

Naomba nipe sehem ambapo RAIS SAMIA amepiga marufuku mikutano ya kisiasa tafadhal,

Halafu pia,hili la katiba ni lao wao chadema au la wananchi??
 

It's Astonishing,

If you are really men why don't you guys organized your selves during the era of Magufuli and go to the road crying for katiba mpya??

Mnaoongeaa kwa courage na ubabe utadhan kama sio nyie vile ambao mlikuwa mmejifungia ndan na kuunga mkono juhud,

Kama ni wanaume kweli ambao mlikuwa mnahitaj katiba mlipaswa kuonesha guts zenu kipindi Cha jiwe,msitake saiz kujifanya saiz mko na hiyo morale simply because mnaona hakuna mkono wa chuma kama ule
 
Jokakuu,

With all of my due respect,

Naomba nipe sehem ambapo RAIS SAMIA amepiga marufuku mikutano ya kisiasa tafadhal,

Halafu pia,hili la katiba ni lao wao chadema au la wananchi??
Nimsaidie na naomba na wewe uwe objective. Kwanza niseme nakubaliana na Samia kabisa kuhusu kuhitaji muda katika hili suala la Katiba. Lakini ni kweli kuwa:
1. Kama JPM , Samia pia kazuia mikutano ya hadahara nje ya majimbo. Openly kasema "mtu kutoka jimbo moja kwenda jingine kufanya siasa hiyo hapana".
2. Katiba ni suala la wananchi, chama cha siasa kama Chadema (japo mimi sio supporter wao) wanawakilisha mawazo ya wananchi wenye mtazamo kama wao. Kumbuka CCM ndio walianzisha suala hili. Kwa hiyo Katiba ni ya Wananchi na Vyama vya siasa vinawasemea.
 
Uko sahihi! Na wazo kuwa Magu alikuwa dictator ni mtazamo tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…