Uchaguzi 2020 Mbowe: Ndani ya saa 72 nitakuwa Waziri Mkuu

Uchaguzi 2020 Mbowe: Ndani ya saa 72 nitakuwa Waziri Mkuu

Dj na muendelezo wa comedy, na wana chama wa saccos yake wataamini hili igizo, ajabu la 8 la dunia hili [emoji16][emoji23]
Dogo nchi tunaichukua mapema saa nne asubuhi Jumatano. Si utakuwa humu nitakutag. Tatizo Mbowe katoboa siri mapema angekuwa mvumilivu tuu kuna wachawi wengi
 
FB_IMG_1595009729173.jpg
 
Mango zangu ni kukuonyesha kuwa kura halali hadi zipigwe ndio tutajua

kwan kura znapigwa uganda, si ni wale wale watu wa tanzania ndo maana nkakwambia mm natumia factor ya 2015 nkaangalia na mwenendo wa 2020, wapiga kura ni wale wale, nkisema mwenendo wa 2020 namaanisha external factors maaana kuna ambao hawana vyama, hawa ndo external factors lakini wengine wooooote ni wapiga kura wa mahaba, yaani hata chama kifanywe nn hawabadiliki maisha yao yote ndo znaitwa kura za mahaba, mfano magufuli ana worse side yake lakini kuna watu hawataki elewa wao ni magufuli kwenda mbele na kuna watu hata lissu agekua kilema miguu yote wanapigia, ndo siasa za tanzania zilivo, hii yote ni elimu tu haijafika kwa watu, na pia kuna wengine ni wahudhuriaji wazuri sana wa mikutano lakini hawajawahi participate kwenye kura, external factors ndo kama hizi kila kitu kingine kinabaki constant
 
Mbowe amesema katika saa 72 zijazo Tundu Lissu atakuwa Rais wa Tanzania na Mimi nitakuwa Rais

Chanzo: Mwananchi online

====

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema ndani ya saa 72 zijazo, mgombea wao wa Urais, Tundu Lissu anakwenda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbowe ametoa kauli hiyo leo Jumapili Oktoba 25 katika mji mdogo wa Bomang'ombe wilaya ya Hai wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni huku akisema Mungu akipenda, yeye anakwenda kuwa Waziri mkuu.

Hata hivyo, Mbowe ambaye pia anagombea ubunge jimbo la Hai, alitahadharisha kuwa kitendo chochote cha kuwazuia mawakala wao 80,160 nchi nzima wasiingie kwenye vituo vya kupigia kura Oktoba 28, kunaweza kubadili historia ya Tanzania.

Hivyo, aliisihi Tume ya Taifa ya Uchaguzi na vyombo vya Usalama, kuhakikisha hakuna jaribio lolote la kuwazuia mawakala wao kuingia kwenye vituo kusimamia upigaji kura na wao watakuwa tayari kukubali matokeo kama uchaguzi utakuwa wa huru na haki.

"Uchaguzi huu sio kati ya Chadema na CCM wala uchaguzi huu sio kati ya Lissu na Magufuli (mgombea urais wa CCM) bali ni kati ya wanaopenda uhuru na haki na waliokandamiza uhuru na demokrasia," alisema Mbowe.

Mbowe amesema wamezunguka mikoa yote ya Tanzania na wananchi wapo tayari kufanya mabadiliko ya uongozi na kusisitiza kuwa kwa mwonekano na hamasa waliyoionyesha Watanzania, Lissu anakwenda kuwa Rais ndani ya saa 72 zijazo.

Hivyo, ameitaka NEC kuhakikisha uchaguzi huu hauvurugwi kwa namna yoyote kwa sababu gharama yake itakuwa kubwa na kusisitiza kuwa wako tayari kukubali kushindwa kama NEC na vyombo vingine vitahakikisha uchaguzi umekuwa wa wazi, huru na haki.
Marais wako wengi labda atakuwa Rais wa tff
 
Watanzania Leo Kuna jamaa yangu kaniambia yupo kwenye usimamizi wa uchaguzi

Sasa semina Yao ya siku mbili iliyoanza leo wamepewa 80000/=

Chakushanga maneno waliyoambiwa kwamba presha huku nje ipo kubwa sana kwaiyo ikiwezekana kuua wakala waue tu ili mradi Maghufuri ashinde.

Kwanza walitolewa wote ambao walifatiliwa habari zai zikaonekana zinavinasaba vya upinzani.

Jaman tuweni makini uchaguzi huu ni hatari sana Kuna watu wapo tayari kuwa ili Meko ashinde usimwamini mtu.

Haki huinua TAIFA

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Huo ni uchochezi, hakuna uhatari wowote wa kuuogopa uchaguzi, nenda katimize wajibu wako, usitishe watu
 
Upepo umebadilika sana

siasa za tanzania ni siasa za mahaba ndo maaana miaka yote matokeo ni yale yale kila uchaguzi, hata ukiangalia uchaguzi wa kutafuta mwenyekiti wa chadema matokeo ni yale yale,
 
pesa kidogo tu umeanza kujitangazia uwaziri mkuu . Ndugu mwenyekiti wa maisha mbona unatupa mawazo sisi wanachama . Hebu tulia basi unacheza na hisia zetu kama macho yako yanavyocheza . Mbowe usituchanganye ujue 😂😂😂😂
 
Naomba niwatahadharidhe wale wanaokusudia kumpigia kura Lissu wasiongee wala kujadili vijiweni. Mabalozi wa shina wa CCM wameelekezwa kuhakikisha kuwa watu hao hawakanyagi vituoni. Posho waliyopewa wanaccm ni kuwa ni heri usipige kura ila uteke wapinzani hasa Chadema watatu na kuhakikisha kuwa hawapigi kura siku hiyo. Posho ni Tshs laki moja.
Hivyo tahadhari ni muhimu. Pia ikiwezekana siku ya kwenda kupiga kura badili njia na muda wa kutoka!
Hao mabalozi wa mashina walivyozeeka wataenda vijiwe vingapi ? Acha tuendelee kuwatesa tutamtaja Lissu hadi wazibe masikio .
#NiYeYe#
 
Back
Top Bottom