1000 digits,
Ni kweli cdm inaweza kukosa wawakilishi bungeni ila sio kwa sababu unazosema ww. Cdm hakitegemei wasomi bali wananchi wenye mapenzi mema na hicho chama. Wasomi ni sehemu tu ya cdm, na sio nguzo pekee ya chama.
Wote tumeona kilichofanyika wakati wa chaguzi za marudio, na uchaguzi wa serikali za mitaa, ni mtu mwenye chuki binafsi tu anaweza kusema cdm itakosa uwakilishi kwasababu hakuna wasomi. Ni hivi, unapotaka kuweka sababu za taasisi kushindwa, jitahidi kutengenisha sababu halisi na chuki zako binafsi dhidi ya mtu.
Sikatai usemachho kuhusu Komu kuwa msomi na mtengeneza sera mzuri. Ila zaidi ya asilimia 70 ya wapiga kura huwa hawachagui chama, au mtu kwasababu ya sera, bali huchagua kutokana na hamasa/mvuto, rushwa, vitisho, ujinga nk. Wanaochagua kwa ajili ya sera nchi hii hawazidi 10%.
Kama ingekuwa watu wanachagua kwa sera basi uchaguzi uliopita cdm wasingepata kura 6m, kwani mgombea wao alikuwa anaongea dakika chini ya mbili, na kusema sera na ilani ipo mitandaoni. Je hao milioni 6 waliingia mitandaoni kuangalia hizo sera? Acha upotoshaji tafadhali.
Kwa taarifa yako cdm hakipiganii kuwa chama kikuu cha upinzani, bali kinapigania kuchukua dola, kuwa chama kikuu cha upinzani kunatokana na matokeo ya uchaguzi. Kwa sasa kuna mtego ccm wanaocheza wa kuwafanya wapinzani wajione wanashindana wao ili kuwa chama kikuu cha upinzani.
Hata kama ukiwa chama kikuu cha upinzani kuna faida gani, kama bunge ndio hilo la kuburuzwa na rais? Cha muhimu ni kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi, hiyo ikipatikana namba hazitaongopa.