Mbunge wa Muheza, Mwana FA alipataje Master's Degree bila kuwa na Bachelor degree?

Kuita magumashi uwe na ushahidi....
 
Mi nimeangalia hiyo cv yake kwenye bunge. Sasa comment yangu ina kasoro gani? Umeona wapi mtu kufanya masters bila first degree au equivalent qualification.
Hapo tunachoona ni diploma and then masters kitu sio cha kawaida.
Aliyeandaa profile za wabunge anatakiwa achunguzwe
 
Ni advanced diploma hio maana inaonesha alikaa miaka mitatu darasani toka 2004-2007!
Inaonesha ni diploma hata kule mwisho imeandikwa diploma walitakiwa kuandika degree kusema kwamba C.V inaonesha alikaaa miaka mitatu darasani haina uzito sana maana inawezekana katika ile miaka miwili ya diploma kuna mwaka mmoja alidisco ndo ikawa iyo mitatu alafu kwenye political experience naona kuna BASATA pale wakati BASATA ni baraza la sanaa alihusiana na siasa. Kama sio kafanya udanganyifu basi kuna makosa kwenye uandishi wa C.V yake na hii inaonesha wasomi wetu hawapo competence, just imagine makosa kama hayo yapo kwenye C.V ya mtu mwenye master hivi C.V ya mwenye diploma itakuaje
 
MwanaFA alikuwa IT staff NBC ni kweli
 
MwanaFA alikuwa IT staff NBC ni kweli
Bro humu tunadili na vitoto vya 2000 havijui lolote hawajui hata Kama kulikua na TMK na East Coast Team
Hawajui hata Kama Kulikua na chamber Squad,uswahili matola,mabaga fresh na GWM
Tuwasamehe bure kabisaa
Hawajui ht km kulikua na shindano la mkali wa rhymes na mfalme ni Afande Sele
 
Hakuna magumashi yoyote aliyofanya Mwanafalsafa kwenye elimu yake. Alisoma Advanced Diploma.
 
Ni kweli alishafanya kazi benki.
 
Advanced diploma ni equivalent to Degree hata ukiomba masters pale Udsm kuna hicho kigezo, unapata vizuri tuu
Tena kwa vyuo vya kati kuna mambo yale ya NTA, mtu akiwa na NTA level 7 anasoma hatua nyingine za elimu
 
Huwa hatuchunguzi kwa umakini hawa wateule ila wengi wana makando makando ya history zao za kitaaluma na hata kiutendaji.

No Wonder wapo so incompetent katika kushika na kuzitendea haki nafasi zao za kiutendaji.
Wajanja wa short cut,chawa ,wasifuo ndio wanaonekana wanateuliwa Mana wanamfurahisha mteule. Sema mwenye uwezo wake hategemei kuwa chawa mwishowe anaiishia kuongozwa na ngwini.
Mana Hana fitina skills za ku survive in this jungles full of sharks,whales,lions,puma,hyena,black mamba,Crocs,fox,wolves,cobra ,Thorn bushes, tiger,cheetah, leopards, and dinosaur,saber tooth tiger etc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…