Pre GE2025 Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka ashambuliwa kwa risasi na Watu wasiojulikana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Soma na hii taarifa ya November 2023

"Katika hali ya kuishiwa na akili za uongozi, Ole Sendeka ameendelea kusababisha vurugu na kushawishi wananchi kuvamia mashamba ya wawekezaji halali. Baada ya vikao anavyodai vya siri na baadhi ya wanachi ,Jana tarehe 11/12/2023 na leo 12/12/2023 wananchi wa Naberera walienda kuvamia shamba la Rotiana Social Investment Ltd Ole Sendeka akiwa nyuma yao.

Bila aibu na hali akijua mashamba hayo yanamilikiwa kihalali na yanaendeshwa na Kampuni ya Rotiana Ole Sendeka amesema uongo kuwa mashamba hayo hayana mmiliki na kuwambia wananchi wayachukue kwa nguvu.

Ikumbukwe kuwa Ole Sendeka 2018 hadi 2022 aliendesha uovu kama huo kwa shamba la Marehemu Yese ambae alikua rafiki yake lililopo Ngage Wilayani Humo Simanjiro hadi alipoumbuliwa na Naibu Waizir wa Waklatyi huo Ridhiwan Kikwete na pia kuzodolewa na binti mkubwa wa Yese."

Isije ikawa ni REVENGE. Maana Ole Sendeka ni mtu wa DEAL chafu
 
Ingekuwa wakati ule tungesema ni RA kutokana na ile issue ya hayati EL, ila sasa tutambebesha nani dhambi hii?

Ova
 
Hapa ndipo kulipo kiini cha tatizo

Kwa kuwa ni fisi anamla fisi mwenzake haina shida kabisa

Kama taifa tuache kuwa tunakaa kimya na kushabikia pindi atokeapo raia anakuwa anawasemea wale ambao hawana sauti
 
Mwanasiasa Ole Sendeka amenusurika risasi, taarifa imetoka na polisi wamethibitisha.

Kwa zaidi ya masaa saba hakuna mahojiano ya moja kwa moja na viongozi wake wa chama, bunge wala wanasiasa wenzake

Kwa zaidi ya masaa saba hakuna Waziri aliyepost kwenye social media account kutoa pole na kukemea, hakuna mwanasiasa wa chama chake aliyejitokeza kulaani. Ila ingekuwa msiba.............

Kwanini sisi siyo wepesi wakurespond kwenye crisis? Pole ole Sendeka.

Mnaosimamia mitandao ya kijamii akaunti za viongozi kuweni active
 
Kwa mwanasiasa, pole yake inategemea sana chanzo cha tukio. Kuna pole ikitolewa inakandamiza upande wa pili.

Mf. Umetoa chuma ukadhibitiwa, risasi ikaenda hewani/pembeni. Ukipewa pole itakuwa ni kumkandamiza aliyetolewa chuma. (ni mfano, hauhusiani na tukio la kwenye uzi huu)

Pole kwa wahanga wa tukio hilo.
 
Ila wabongo tuna ujinga sana. Huyu tayari kishaingiza siasa kwenye hili. Kuwa mbunge haimaanishi kwamba una kinga ya majambazi, wakora, watesi na kudhulumiana kwenye biashara
 
Kama ni hivyo wampasue tu hakuna jinsi nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…