Mbwana Samatta ilikuwaje ukashindwa kumhamishia baba yako ‘ushuani’ ukakubali afie Mbagala?

Sema nn kuishi mazingira maziri ni unyama sana.
Mazingira mazuri iko kwenye tafsiri ya mtu binafsi. Kuna mtu mazingira mazuri ni kuona purukushani za wanakitaa, mwingine kuona mbuzi na ng'ombe. Hawa ukiwatoa kwenye asili yao unawavuruga kabisa kama wakina Dudukwe na Chaba. Ukiwaleta huku ambako kila kitu unanua wakati wao wanajua vyote ni bure mtapiga mtaua.

Maisha yale ndio yenyewe. Nimeshashuhudia mzee Sammatta akiwa kwenye moja ya apartments za mwanae. Mnafikiri angemuambia mwanaye nijengee sehemu fulani ingechukua hata mwezi?

Kuna bibi alijengewa na wanaye sehemu nzuri huko kwa washua alihama baada miezi sita. Akiwa peke yake vibaka walimvamia mara 4 na kuiba, na hata wakipiga kelele sauti zinaishia kwenye uzio wao. Akaamua kurudi uswahilini ambako alikuwa anaishi na wapangaji.

Sometimes good life is not good and safe at all
 
Hujaishi vijijini mkuu. Kuna vijiji ili uwe salama hutakiwi kufanya unayosema. Na mzazi anakuambia kabisa acha niishi humu ili tuendelee kuwa salama. Kuna vijiji kufanya maendeleo ni kutengeneza maadui usiowafahamu na kuwaona kwa macho
 
Umetumwa
 
Hasira za nini na maisha ya watu mkuu? Acha watu waishi wanavyotaka.
 
Sahihi, hasa wazee wa Kiswahili ambao wamezoea kupiga soga mtaani,
 
Point
 
Mkuu itakuwa tu masharti ya maganga. Si unawajua tu kobaz.


adriz Tanganian Adiosamigo
 
Tunavyowajuwa wazee wetu, hutakiwi kuwahamisha kwenye mazingira yao. Boresha mazingira yao basi wataishi tu kwa furaha. Labda watake wao.
Hata siye tukizeeka tusingependa kuhamishwa amishwa na watoto bila ridhaa yetu!
 
Bro, mtu kaishi Mbagala miaka 40+ (probably), akitoka anakutana na washkaji zake anakunywa nao kahawa kwa miaka yote hiyo wanapiga story za mapito yao halafu uje umuhamishie Masaki ndani ya fensi kama gereza?
Hawezi kukubali.
Besides, si busara kucontrol maisha ya mtu kwa sababu ya kujiridhisha.
 
Wazazi wengine wanakataa ujue,Ushuani rafiki yake awe nani?
Yaan akae karibu na Bakhresa wakati hana kama za bakhresa anategemea za mwanae😂😂😂.
Basi boresha mazingira yake hapo alipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…