Mbwembwe za DP World, kwa kuanzia tu wanawekeza Dola milioni 500 bandari ya Dar

Upuuzi mtupu. Dola 500m unaona ni pesa ya ajabu sana?

Barrick awamu ya kwanza tu waliwekeza dola 600m kwenye mgodi mmoja tu wa Bulyanhulu.

Dangote awamu ya kwanza tu aliwekeza dola 700m.

Kampuni ya Brazili ilitumia dola 760m kwenye utafiti tu wa mafuta.

Tuliwakataa Rio Tinto walioraka kywekeza dola billion 3 kwenye mradi wa chuma wa Liganga.

Bomba la gas, iliwekezwa dola bilioni 1.

Halafu wewe unaona kama dola 500m italeta mabadiliko makubwa sana kwa Tanzania.

Ninyi ndio mnaambiwa kuwa mkipata ...... yanalua mbwata.

Hivi sisi kama nchi unaamini tunashindwa kupata dola 500m? Labda ingekuwa dola bilion 500, hapo kweli pangekuwa parefu.
 
Mbona tayari, umelala? Msikilize Mbarawa chini hapo 👇🏾

Hapana, siyo "kulala"; pamoja na maelezo hayo yanayoonekana kuwa mazuri kama umelaza akili, Profesa naye anasema uongo humo humo ndani yake.
Hii dhana ya 'Private sector' pekee ndiyo yenye uwezo wa kuendesha bandari kaitoa wapi? Ni msahafu toka peponi uliotelemshwa kwake, au kakaririshwa tu awe anauimba kila mahali?

Usinielewe kuwa napinga 'private sector', lakini siamini jambo hilo kuwa kama ndio hitimisho la suluhisho.
 
Siku ambayo Watanganyika hawataisahau daima kuuza mali zao kwa Waarabu.
 
".....kazi hiyo waifanye kwa ufanisi".

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Lundo la watu nakuambia over 50Millions wote hatuwezi endesha Jambo dogo kama hilo 'Bandari' mpaka tutafute eti wawekezaji. Watufanyie sisi hatuwezi, Kama vile ni walemavu.
Kama kweli serikali imeshindwa kupata 500m, iuze hisa kwa wananchi, na pia itafutwe kampuni ya kizalendo ya kuweka japo 20% tu ya hiyo. Kiasi kilichobakia cha 80% tuuziwe hisa. Turltapata pesa zaidi ya hiyo dola 500m, hata mara mbili yake alimradi kampuni isiwe ya kipigaji. Mbona NMB walipouza hisa kulikuwa na over subscription mpaka wengine tukarudishiwa pesa zetu tukiambiwa kuwa wanaotaka kununua hisa wamekuwa wengi mno?
 
".....kazi hiyo waifanye kwa ufanisi".

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Maza ameshauza tayari
 
Vyanzo vyao vya habari?

Huo uwekezaji kama wana uwezo wa kuufanya bandari ya Dsm nini kimewashinda kufanya nchi nyingine walizofunguliwa kesi za kutosha?

Hizi propaganda za kitoto hazina maana.

Samia ni Shetani.
[emoji1787][emoji1787]

Chalii...

Umechanganyikiwa sasa....

Mashetani ni wale wanaotaka "status quo" ya ujinga iendelee hapo TPA pamoja na wapotoshaji wote.....


Je na wao hawajafungua kesi dhidi yao?!!!

Hivi kufunguliwa kesi ndio kutiwa hatiani.....

Kwa ujinga wako tuambie DP WORLD wameingizwa hatiani mara ngapi ?!!!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo ni 1.2t, sio hela ya kutisha kwa hivyo. Labda uwaambie wasiojua chochote ndio wataona ni hela ya maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…