Mchengerwa: Maelekezo ya Makonda kuhusu Wananchi kumtembeza Diwani kwenye matope sio maelekezo ya Serikali

Mchengerwa: Maelekezo ya Makonda kuhusu Wananchi kumtembeza Diwani kwenye matope sio maelekezo ya Serikali

Waziri Mchengerwa amethibitisha kwamba yeye ni mwanasheria. Ameiletea sifa kubwa taaluma yake ya Sheria.

Baada ya Makonda kuwapomgeza wananchi waliokuwa wanawadhalilisha viongozi wao, Mchengerwa amesema wananchi wakatazwe kujichukua sheria mkononi.

View attachment 3182117

====================​

"Sasa niliona ile clip pale Arusha wananchi wakimtembeza Diwani (na viongozi wengine kwenye matope, madimbwi na maji machafu) na nikaona maelekezo ya Mkuu wa mkoa (Paul Makonda, Mkuu wa mkoa wa Arusha) akisema endeleeni kuwatembeza, kwanza niwapongeze Wakuu wa Mikoa mnafanya kazi nzuri, lakini lazima nikiri kwamba yele sio maelekezo ya serikali, hayo si maelekezo ya Serikali, wajibu wetu ni kwenda kutatua kero za wananchi na kwa Wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya (Wakuu wa mikoa na wilaya) tuna wajibu wakati wote kuhimiza wananchi kutochukua sheria mkononi, huu ni wajibu wa kila mmoja wetu, tuwahimize wananchi kutochukua sheria mkononi," -Mchengerwa.

"Matukio haya leo yatatokea Arusha, kesho yatatokea huku, keshokutwa yatatokea huku, si utamaduni wetu Watanzania, kwa hiyo ninawataka Wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya kujizuia kuhamasisha wananchi kuchukua sheria mkononi, si maelekezo ya serikali na si utamaduni wa Watanzania, nadhani nimeeleweka vizuri," -Mchengerwa.

"Kunapokuwa na dimbwi sehemu na sisi tupo maofisini hii haipendezi na nina imani kwamba ofisi zetu hususani ofisi za Wakurugenzi hazikosi fedha za kwenda kutatua kero ndogondogo za namna hii, hatukosi hizo fedha, tukote maofisini twende tukatatue kero za wananchi, huo ndio wajibu wetu," - Mchengerwa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa ameelekeza hayo alipokutana na viongozi walioko chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo Wakuu wa Mikoa.
Tatizo nchi imekosa watu wenye uzalendo, watu wanapenda maslahi Yao Wacha wanyooshwe si waliahidi wakati wa kuomba kura?
Nchi zilizoendelea viongizi walihojiwa na wananchi.
 
Mwanasheria asiyejua maana ya uchaguzi hii nchi ni ya ajabu na ndio maana tunashindwa kesi za mikataba.
 
Back
Top Bottom