Hizo kelele za wanawake mara nyingi ukiangalia ni kuhusu usawa na mgawanyo wa majukumu na si kitu kingine, lakini kelele za wanaume ni kuhusu kila kitu kinachohusiana na mahusiano na ndoa kwa ujumla hasa kwenye suala la wanawake kujitunza, kiufupi wanaume siku hizi ndio wanaoongoza kwa kulalamika
Wapo wanaume wengi sana wanaokataa ndoa tena siyo kwa maneno tu bali hata kwa vitendo, sasa kama mnazihitaji hizo ndoa na mnahitaji kupata wanawake sahihi kwa ajili ya kuoa, kwanini msianze ninyi wenyewe kuchukua hatua ya kujitunza na kuacha kutongoza wanawake ambao hamna malengo ya kuwaoa
Ni kwa misingi ipi unaona ndoa ni msalaba kwa mwanaume tu na si kwa mwanamke pia hebu nijibu hapo, aliyekuambia mimi nahitaji ndoa ni nani siku hizi wanawake desperation ya ndoa inaisha taratibu kadiri miaka inavyozidi kuenda, wanawake wengi wanaona heri kukaa bila ndoa au kuwa single mothers kuliko kuwa na wanaume ambao ni too demanding na tena ni mizigo