Mchungaji Msigwa agoma kupanda gari za CCM, alakiwa na wana-CHADEMA


Ila naona hata undugu utapungua sana sasa, Msigwa akipata tu shida kuanzia sasa Mh. Rais hawezi kabisa msaidia kwa hili lililotokea, na hata ingefaa Msigwa angetoa neno la shukrani kwa Mh. Rais, sasa hizo hela zikirudishwa kwa Mh. Rais navyojua hatakubali tena kutoa msaada hata huko kwao nyumbani, sbb atasema niliingiwa na huruma nikatoa msaada baada ya ndugu zenu kunijia, ila nikapata fedheha. Yaani Msigwa shauri yake
 
Hii habari imeishachuja! Rais ALIOMBWA NA NDUGU WA MSIGWA awasaidie mchango wa kumlipia ndugu yao kutoka jera! Rais alikuwa anatekeleza ombi la hao wazee hivyo mambo ya alikuwa kaishalipiwa hama la!! hayamuhusu Rais!
Yani hili jamaa tangu liandike upumbavu wake Nikiliona napata hasira Sana Eti "Hela zote ni Mali ya raisi "
 
Elimu na exposure ni kitu muhimu sana
 
Kwani alimuomba wakati anawabambika kesi alifikiria kuhusu undugu au baada ya kiki kubuma na kuona nguvu ya umma.kama aliweza mtoa lulu bure alishindwa vipi kuwafutia mashtaka
 
Sio tatizo kikubwa kalipiwa faini Na mh. Rais Na katoka.
Mchango wa Rais umesaidia sana kutoka kwa msigwa leo Na kujumuika Na familia yake.

Bonge la aibu, hakuna mtu alikuwa anataka mchango wake. Yeye aache tu kuagiza mahakama na vyombo vya dola kuwakomoa wasiomkubali. Tunahitaji tume huru ya uchaguzi na sio michango yake huku akiwa ndio anayeagiza upindishaji wa sheria.
 
maigizo hata yale ya Kaole yana afadhali..ngoja tuone...
 
Ndioooooooooooo ndugu wa Msigwa ambao pia ni ndugu wa Mh. Rais kwani wameoleana, walimwendea Mh. Rais na kuomba msaada. Ww ulijua alitoa tu bila kuombwa?
Wakati anamfunga akujua kuna undugu?
 
Mh. Rais anatengeneza tatizo na kulitatua ili apate huruma ya wananchi...

Ila kwa hili ameanguka pakubwa maana ameiahia kupata fedheha kubwa sana...

Swali la kujiuliza ni kwamba alikua wapi siku zote hizo kutoa mchango? na kwanini leo? hii inaonesha kwamba mpango aliokuwa ameuandaa umeanguka vibaya mno...

Hakika huu mchezo hatourudia tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda mmtumie wasiojulikana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…