Mfano wa jengo la Chadema makao makuu

Mfano wa jengo la Chadema makao makuu

Hapo inatafutwa njia ya kuchangisha wanachama ili viongozi wapige Hela, walimpiga sabodo milioni 500, aliwapa za kujenga Ofisi, miaka nane iliyopita,mpaka Leo hakuna hata tripu ya mchanga.

Juzi Joni ze cheni wanasema wamechanga watu karibu milioni mbili,halafu eti makusanyo milioni 400, wakati hata hao wachangiaji wangetoa 1000 ilikuwa bilioni mbili.

Kwa hesabu rahisi, wanasema wachangiaji kwa wastani walichangia shilingi mia mbili (200) kwa Kila mmoja
Nyie maccm ni wachawi Sana. Manina. Majengo yote ya ccm na viwanja vyote vilijengwa kwa michango na kodi za watz wote kwa utapeli wenu wakati wa chame kimoja.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hilo jengo likijengwa sasa itakuwa POA sana. Lakini lingejengwa kipindi Cha mwendazake lingevamiwa na kuchomwa moto.

Chadema jengeni kipindi hiki ambapo Tanzania kuna kiongozi Bora.

Kipindi kile Cha marehemu roho mbaya lingebomolewa na kikundi Cha wasiojulikana.

Soon nitajiunga rasmi chadema
Umesema kweli kbs. Jiwe!!!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
😀Baada ya kusemwa sana

Bado jambo moja... kuwe na ukomo wa awamu ya uongozi.. maximum iwe vipindi viwili vya miaka 5 kwa 5

Siyo kiongozi anakuwa kiongozi wa milele halafu mnahubiri deomokrasia; demokrasia ianze ktk vyama kwanza
Huko tutafika. Na wewe waambie serikali waache kuwanunua wapinzani. Hatuwezi kuweka mwenyekiti mwenye njaa pale. Tunamuandaa John Heche aje aongoze chama
 
..Chadema waepuke kuiga na kutamani kila kitu walichonacho Ccm.

..Ccm wana maofisi makubwakubwa kitu ambacho ni gharama.

..Ccm wana magari ya bei mbaya ya kifahari, ma-V8, ambayo ni gharama nyingine.

..Ccm ina watumishi wengi sana ambao wote wanahitaji kulipwa na kutunzwa.

..Chadema wajielekeze kuendesha chama kwa kutumia gharama ndogo, na watu wachache wanaofanya kazi kwa ufanisi.

Uko sahihi kabisa, mimi ni mmoja kati ya watu wasioamini katika maofisi makubwa. Dunia ya sasa taarifa zote zinapatikana kidigitali, na sio kushinda maofisini. Ccm wana maofisi kila mahali, matokeo yake ofisi hizo zimegeuka vijiwe vya majobless, washirikina, kupiga majungu, na kupanga siasa za hila, fitina na wizi wa kura.

Kwa sasa ni vyema Cdm wakawa na ofisi za wastani, zenye watendaji wachache watakaofanya kazi za uratibu kwa ufanisi, ikibidi na sehemu moja ya mikutano yao ya kitaifa. Kwa mikoani ambako bado ardhi ni bei nafuu, wanunue ardhi kama heka 2@ofisi, ili wapate sehemu ya kufanyia mikutano yao ya hadhara. Maana sasa hivi wanafanyiwa hujuma kila wakitaka kufanya mkutano wa hadhara wananyimwa ruhusa ya maeneo ya kufanyia mikutano.

Kwa ulimwengu wa sasa wa Digitali, unaweza kuwafanya Cdm wakatumia njia hiyo ya kidigitali kuwapa taarifa wanachama na wafuasi wake. Kusajili TV ya mtandaoni ni 50,000 tu kwa sasa. Hivyo ni vitu viko ndani ya uwezo wao. Sishauri maofisi makubwa yatakayojaza majobless ofisini, labda kama majengo hayo yatakuwa na ofisi za kupangisha ili kukitengenezea chama mapato.
 
Nimeona Majengo kadhaa yanayosemwa ndo Ofis za chadema ! Kuna Ofis ilioneshwa kuwa imegharimu Milion 80 na haijamaliziaka nilijiuliza sana Hivi nani anaratibu michango inayochangishwa na natumizi yake ?
Tujenge taasisi imara zenye uwezo wa kuhoji Alafu baadae tujenge Taifa imara !!

Chadema wote ni ndiyo mzee hakuna wa kuhoji mambo ya msingi!

Nawatakia kila la heri kwenye ujenzi wa ofisi


Britanicca
Umejiuliza hizo pesa za kujengea zinatoka wapi, kama hujui zinatoka wapi huna uhalali wa kuhoji.
 
Nimeona Majengo kadhaa yanayosemwa ndo Ofis za chadema ! Kuna Ofis ilioneshwa kuwa imegharimu Milion 80 na haijamaliziaka nilijiuliza sana Hivi nani anaratibu michango inayochangishwa na natumizi yake ?
Tujenge taasisi imara zenye uwezo wa kuhoji Alafu baadae tujenge Taifa imara !!

Chadema wote ni ndiyo mzee hakuna wa kuhoji mambo ya msingi!

Nawatakia kila la heri kwenye ujenzi wa ofisi


Britanicca
Wewe mwana ccm mambo ya chadema yana kuhusu nini? Ya nyumbani kwako hujayamaliza unarukia ya wenzako?
 
..hizo fedha zingeelekezwa kuimarisha chama mpaka ngazi ya chini.

..bado sijaona haja ya Chadema kuwa na makao makuu ya kifahari na gharama kiasi hicho.

..TEKNOLOJIA imebadilika kiasi kwamba hakuna ulazima wa makampuni kuwa na maofisi makubwakubwa.
Gere imeanza kabla haijajengwa🤣
 
Hayakuhusu .....

Ndo jibu rahisi ninaloweza kukujibu maana nyie CCM mnachokitaka ni kuibomoa Chadema kwa kuwatumia mapandikizi ili yakagombee nafasi za uongozi ktk Chama na ndio target yenu, ila hayo mapandikizi yanapojitokeza tu yanakutana na Kiongozi makini mhe, Freeman A. Mbowe na jopo lake wanayatupilia mbali...

Mfano, kuna moja hilo hata ukiliangalia tu usoni unaona kuwa halikuwa na dhamira nzuri, eti likagombea ujumbe wa sijui pwani....🤔
Alichokutana nacho hatakaa asahau, ila zilisikika kelele tu kuwa Chama hakina demokrasia..... Kumbe dhamira yake iligundulika mapema tu na sasa karudi kwa waliokuwa wamemtuma na aibu juu.

Chezea Chadema wewe......✌🏽💪🏽👍🏽
Chadema Forever Being
 
Jengo jipya, katiba Mpya….. sio unabwabwaja katiba mpya huku upo banda la zamani.
 
Back
Top Bottom