DOKEZO Mfanyabiashara maarufu Arusha aibiwa Tsh. Milioni 100 kwenye akaunti ya Benki ya NMB

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
NDIO MAANA WAKAMUUA CHID BOY
WATU WABAYA SANA
 
...... $4,000 Citibank...... Dubai (Kama HushPuppi !!!)
 
Zinatosha kuanzisha ka mtaji
Unajua maana ya kuchomoa kidogo kidogo?. Hana hata 10. Ilikuwa achukue zote kwa pamoja ndio ungekuwa mtaji. Wezi wengi wa hivyo nawaona wajinga tu ksbb mwisho wa siku wanakuwa hawana hata 100. Ksbb ilikuwa akichomia milioni 5 anasikilizia siku kadhaa then anaanza kuipiga. Ikiisha anarudi kwenye kihenge.
 
Ndiyo maana mimi naamini wasimamizi wa mirathi hupewa taarifa za uongo na benki kuhusu pesa walizoacha marehemu hasa wale wa fixed.
Ni kweli. Kuna kesi nyingi za warithi kudhulumiwa na kudanganywa kuhusu kiasi cha fedha kilichokuwa kwenye account ya marehemu.

Binafsi mzee wangu alikuwa anafanya shughuli zake na alikuwa anaweka fedha benki pia Alikuwa mstaafu so alikuwa analipwa Pension yake via NMB. Mwaka ambao mzee alifariki, alivuna mpunga na akauza gunia zaidi ya 500 ambazo alipeleka benki. Baada ya kufariki na tulikaa muda mrefu kupata utaratibu wa mirathi kwenda benki tunaambiwa mzee alikuwa na laki saba tu benki.
 
Inakuwaje pesa zichomolewe asipewe taarifa kwa ujumbe mfupi? Au huyo jamaa alifanya yake zikitolewa asipate taarifa?
Wanachofanya anagushi sahihi yako kisha kila kitu kinaendelea kwa kughushi tu kuanzia kuomba kadi na kuendelea. Naku-mention kwenye uzi mmoja ambao mfanyakazi wa CRDB ubungo aliiba pesa za mteja zaidi ya milioni 100 kwa mtindo huu mwaka 2019.
 
Hapo ofisini hata wana aliokuwa anakula nao kitimoto Moshi - Arusha na full tank sasa wakimuona watakuwa wanamkimbia kwenye kordoπŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
Kumaa nisha ukionekana nae means mlipiga wote πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Pia mnahakika kuwa aliweka hiyo hela bank? Maana wazee nao huwa wanamafekeche yao.

Kuna dogo mwaka wa tano huu anafuatilia nyumba pale PPF mwanza Baba yao alinunua. Wamecheck database ya PPF jina halipo, kuja gundua kumbe aliandika jina la bimdogo.
 
Kuchomoa hela kwenye akaunti ya mtu halafu jinai hiyo inafanywa na mtumishi wa bank ni wazi NMB si sehemu salama kuweka akiba
Mtanzania haaminiki kwenye mambo ya fedha. Narudia tena: mtanzania haaminiki kwenye mambo ya fedha. Najua duniani kote binadamu kwenye fedha ni kitu kingine lakini kwa Tanzania ni zaidi. Benki nyingi tu (labda ondoa zile za kimataifa) wafanyakazi wake hawaaminiki. Bongo ukiwa na fedha benki inatakiwa kila uchwao uwe unaangalia balance. Na wakati wa kutoa kama unatoa fedha nyingi uwe makini sana kwani unaweza kuwekewa majambazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…