KERO Mfumo wa Ajira Portal unatutesa, mamlaka husika ifanyie kazi changamoto hii

KERO Mfumo wa Ajira Portal unatutesa, mamlaka husika ifanyie kazi changamoto hii

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ajira portal imekuja kunyima ajira kwa vijana na si kutoa ajira kama ilivyotarajiwa mwombaji amesoma kuanzia certificate mpaka degree kaweka cv yake pale unahitaji kuomba kazi ya diploma iliyotangazwa

Kufuta cheti cha degree ni changamoto sana
Msaada kwa anayejua kama naweza update hiyo issue kufuta chet cha degree
Jaribu kuwasiliana nao kupitia nambari: 0739160350
 
Mkuu pole Sana, ila waliweka hivyo ili iwe kikwazo kwa wanaomba ajira.
Ajira ni haki kikatiba , mtanzania ana haki ya kufanya Kazi na kumuingizia kipato bila kuvunja Sheria za Nchi.

Sasa ukiwauliza psrs Kwa nini wamefanya hivyo , wametumia Sheria gani , kumzua mtanzania mwenye degree na diploma, ashindwe kuomba Kazi za diploma ,
Utangundua ni roho mbaya Tu, za viongozi wa TZ,

Psrs walitakiwa washitakiwe Kwa kuvunja Sheria, kwa kuwanyima haki wa Tanzania ya kupata Kazi wanayoitaka ili kujiingizia kipato
 
Shukran mkuu upo sahihi sana hakika umeongea, tunasoma kwa tabu, mitihani migumu bado kwenye mfumo wa ajira na mifumo yao ya ajabu ajabu inasumbua, bado watakutumia control number ulipe deni la HESLB. Kwa kweli kuna mambo yanakera kabisa aisee
 
Nilifungua account ajira portal siku za nyuma,

Nilipoteza simu na emails sikuwa nimenukuu wala siiijui.

Na sahivi siwezi login sina emails hiyo na sikumbuki password 🔑

Nafanje nipate Access ya account yangu

Msaada jamani
 
Back
Top Bottom