Mfumo wa Jeshi la Polisi ubadilishwe, Unakandamiza na kunyanyasa Wananchi hasa wa daraja la chini

Imefika mahali ni afadhari ukutane na jambazi huenda anaweza akaingiwa roho ya huruma sio hawa polisi wetu wana unyanyasaji mkubwa sana aisee sina hamu na hawa watu hasa akisha jiona kabeba bunduki na kavaa jezi anajiona ni mungu.
Jambazi anakupokonya pesa lakini anakuachia roho yako. Polisi anachukua vyote, pesa pamoja na roho yako..
 
Mbona inaeleweka Polisi huzingatia Taratibu zilizowekwa kisheria katika Utekelezaji wa majukumu yao. Wewe ilkuwaje?
Hivi unawajua vizuri polisi au unawasikia tu,kama waliwaua wafanyabiashara wa madini kutoka ulangq morogoro na yule dereva wa tax wa sinza juma ndugu na zombie akatoka kwenye vyombo vya habari na kuaminisha watqnzania wale ni majambazi unawatetea Kwa kipi
 
Mimi wakizingua siku nawaendea pangani tu nawaaangalia kwenye sahani yenye maji,Babu akiniuliza niwafanyeje namwambia tu nope sindano nitoboe maji yanabadilika yanakua red na hao walionitesa.bye bye
 
Ulaya na Marekani hakuna huu upuuzi mkuu. Muulize R Kelly..
r kelly ni kapuku tu marekani system imemlea na ilikuwa ndo mda wake wakumshusha ...diomond unaeza mueka kwenye kundi la matajiri tz ila sio wenye nguvu na ushawishi wakutosha ....mwangalie mtu kama lugumi kaaibia serikali ,akakunja hadi sheria zikawekwa plea bargain tena mbele ya chuma magu
 
Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan yupo jela muda huu.

Rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac alikaa jela kwa sababu ya corruption.
 
Hili sakata liliniuma sana mkuu. Very innocent business people..
 
Kuna baadhi ya familia za polisi hupaswi kuolewa huko au kuoa.Maana zina laana,kwa hiyo hata familia utakayoanzisha itakuwa ya majanga kila kukicha kwa ajili ya machozi ya watu walioteswa kunyanyaswa na saa nyingine kupoteza pumzi
 
Baada ya siku 4 ndugu wanalia kuomba msaada utoke anaambiwa atoe laki 6, ndugu wanajichanga wanatoa laki 6 mtu anatoka akiwa kaumizwa na majeraha mengi mwilini ambayo kapigwa bila kosa.
Polisi wana kauli mbiu yao wanasema "Kituoni unaingia bure ila unatoka na pesa..", na hiyo haijalishi kama una kosa au laah
 
Tatizo elimu form four ndio kigezo kikuu cha kuwa askari waanzie hapa kaujiri watu welevu waliostarabika na kutambua dunia inavyoenda. Huwezi mkuta mwanajeshi,askari mwenye taaluma yake safi anafanya huo ujinga.

Japo wanaweza kuwepo lkn isiwe kwa idadi kubwa
 
Polisi ni wanyama mwitu, hawana utu wala huruma hata kidogo, Huwa sipendi ukaribu au mazoea nao.
Kuna mmoja ni kabila moja na mimi huku kitaa. Sasa nimemkwepa kwa maana naona anatumika kigezo cha ukabila kunipeleleza. Anataka nimuone kama ndugu yangu kumbe ni spy anatumiwa..
 
Kuna mmoja ni kabila moja na mimi huku kitaa. Sasa nimemkwepa kwa maana naona anatumika kigezo cha ukabila kunipeleleza. Anataka nimuone kama ndugu yangu kumbe ni spy anatumiwa..
Kama una namba yake block kabisa na hama hilo eneo, anaweza kukukamatisha usingiziwe umekutwa na bangi au silaha, polisi sio rafiki yako hata kidogo
 
Shida sio Polisi ni Ccm
 
Kama una namba yake block kabisa na hama hilo eneo, anaweza kukukamatisha usingiziwe umekutwa na bangi au silaha, polisi sio rafiki yako hata kidogo
Mwingine yupo humu humu JamiiForums, alitumwa kunivurugia mipango yangu ya maisha mwaka 2019 miezi ya mwishoni, nilikuja kimshtukia too late (Nikiwa nimechelewa) tajari akiwa amenivurugia kila kitu.

Nasikia mwaka jana 2024 Mungu amempiga Kofi zito ilibaki nusu afe katika ajali ya bodaboda kmmae.

Mungu hadhihakiwi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…