Mgeni mwalikwa Mkutano Mkuu wa CCM kuita CCM 'Chama cha Mambuzi' ni kwa bahati mbaya au kweli?
Huyo kiswahili sio lugha yake, ww umeona furaha ipi? Shida yako uitukane CCM, please CCM uiheshima kama Baba na Mama yako..
Usiwahusishe Baba na Mama zetu na vitu vya ajabu. Kama Uchawa umewaambukiza mpaka Wazazi wako, endelea.
 
Kwa aliye wahi kuchunga mbuzi bilashaka atakubaliana na mimi kuwa mbuzi huwa ni mwizi na ni mrafi kupindukia
 
Nadhani huu ungekuwa wakati mzuri sana kukiondoa chama hiki cha mambuzi kama pangekuwepo na chama sahihi na chenye nia njema na thabiti kwa nchi. Miaka 60 ya uhuru nchi yenye rasilimali za kila aina kuteseka kwa mgao wa umeme, maji ni AIBU! Baadhi ya mbuzi sasa wamegeuka chawa! Kwao maslahi ya matumbo yao ni bora kuliko ya watanzania!
View attachment 2438782
Nchi inakopa kufanya mikutano kama hii? waliyataka wenyewe, Mungu amewalipua. Nchi inazo shida nyingi sana zinazohitaji pesa hizi zinazotumika kualika watu unnecessary kwenye mkutano wa kifahari.
 
Ukikaa chini ukatafakari namna tunavyoenda kama taifa huwezi kuyakataa maneno ya huyo jamaa maana wanayoyafanya waliojipa dhamana huwezi kusema wanatumia akili za kibinadamu wale ni mbuzi meeh kabisa.

Umeme tabu maji tabu hela zinachotwa hovyo kinachofanyika hakionekani,raisi anasimama hadharani anasema ”wote tunakula najua ila kila mmoja ale kwa urefu wa kamba yake" means watu wajipigie alimradi usimtingishe mwenzako akadondosha kijiko kuna namna yoyote ya kujitetea kusema CCM siyo chama cha mambuzi?
kualika wageni wote wale maana yake matumizi makubwa ya pesa kuwaalika, kusafiri, kukaa, na kuondoka. Mbona tunaambiwa miradi inakwama kwa ukosefu wa pesa? vipaumbele hatuna. Leo hii tunatifuatifua barabara nzuri kabisa za lami ili kujenga barabara za mwendokasi, yaani mipango hakuna kama mbuzi tu, siku sote tunakua reactive badala ya proactive, hasara juu ya hasara, deni juu ya deni, maana barabara hizi tunazozichimbua tukijenga mwendokasi ni za mkopo pia. Utashangaa hata huko Dodoma sasa hivi wanajenga barabara bila kuweka provision ya kujenga reli au barabara za mwendokazi huko mbele ya safari miaka 30-50 ijayo jiji litakapokuwa limejaa.
 
Ni tumie mfano wake wa nchi ni kama nyumba/familia. Kwamba huwezi kuwatimizia wanafamilia wako kila kitu. Uko ukweli katika hili. Lakini famila ambayo Wazazi/Walezi/ Wakuu wake wanawambi a twendeni tukalime shambani. Wanavuna mazao yasiyo weza kukidhi mahitaji yote ya familia walitegemea Baba na Mama wa familia waishi kwa kiasi watoto kama hivyo baadhi wamevaa .midebwedo wana lishe duni na hivyo hivyo mambo mengine ya msingi kwa wana familia. Kwa upande mwengine wsnaona Walenzi wao wanaishi kwa ufahari wote. Wana kula wanasaza hawawezi kuamini wanapoambiwa utaenda shule na kandambili mguu mmoja umetoboka na kaputula ya viraka.

Sasa mitazamo ya hivi ndio ya viongozi Mungu aliotuachia wawe visima vya hekima katika nchi. Mumbuka hawa wanao uzoefu tanguc wa kufanya kazi na Mwl Nyerere na awamu nyengine baada ya.

Nilimsikia Mkutano uliopita akionge ukaribu wake na Makamu Mwenyekiti Bara. Hawa ndio brain behind CCM, Nchi na Uongozi wake. Kwa maana wakitoa ushauri hauwezi puuziwa utapewa uzito unao stahili.

Bila Watanzania kustuka na kutafuta uso wa Mungu kwa bidii ili aingilie kati sijui ama kwa hakika sijui.
 
Hivi yule mgeni mlimtoa wapi? Kwa kweli ametubariki sana.
Mgeni ni wa chama cha mapinduzi, alibarikiwa kujumuika na chama tawala na ujumbe wake ulipokelewa kwa furaha pamoja na changamoto za matamshi ambazo zimekuwa hoja kwa baadhi ya wapinzani wa ccm. Itapendeza zaidi iwapo hoja hii itabebwa na viongozi wa upinzani pia kama moja ya hoja za uchaguzi 2025. Itarahisisha ushindani unaotegemewa.
 
Back
Top Bottom