Miaka 22 ya TICTS nchini yafika mwisho, mamlaka ya bandari kutosaini mkataba mpya

Mwisho wa TICS ni mwanzo wa TICS nyingine, kwa Tanzania tegemea yaleyale au zaidi ya yale, God father wa TICS hayupo sasa amelala Lupaso, shamba linawaniwa na wahuni wengine..
Hiyo miaka 3 ya mwishoni ya huo mkataba aliwaongeza nani?nakusudia ni awamu ya Rais yupi kikwete au magufili ?
 
Waje waarabu tu sasa ili tuendelee na mambo mengine.
 
Hapo kaondolewa TICTS lakini akina JK ni wazi wameshaandaa mdau wao mwingine wa kuja kuwakusanyia mapato.
 
Kwa utawala wa sasa watakachoshauriwa na watakachofanya ni kubadili jina na kuja kama kampuni mpya... na watapata dili...
 
Mwisho wa TICS ni mwanzo wa TICS nyingine, kwa Tanzania tegemea yaleyale au zaidi ya yale, God father wa TICS hayupo sasa amelala Lupaso, shamba linawaniwa na wahuni wengine..
Kabisa...
 
Niliwai kuomba Kaz katk kampuni hyo ya karamagi [emoji41]
 

Kina Nizar Karamagi hao!
 
Ninakubaliana nawe mkuu 'sblandes', matatizo yetu yote hapa nchini kwetu ni uongozi mbaya na kwa hiyo serikali mbaya, ndiyo maana nchi hii pamoja na kubalikiwa sana, haitaendelea hadi hapo tutakapowapata viongozi wanaojali maslahi ya nchi yao na wananchi wake.

Sasa tatizo linabaki palepale jinsi ya kuwapata viongozi hawa. Najua wapo, na pengine wengi wao hata hawajitokezi mbele watu wawaone.

Tanzania kwa sasa inahitaji kutikiswa sana iondokane na usingizi mkubwa unaoinyemelea.

Kwa mwendo huu wa sasa, hatufiki popote.
 
Ninakuomba uelewe kwamba TICTS ni kitawi tu kilichopo hapa Tanzania ambacho ni sehemu ya kampuni kubwa duniani.

Hata hao Dubai wakija hapa, wanaweza kuunda tu kitawi chao hapa kwetu kuendesha shughuli zao.
Ni Tawi la Hutchison Port Holdings, hao wakima DP World hawana tofauti.

Bora ajaribiwe APM Terminal, hao watu wa Asia hawajatofautiana sana
 
Mwisho wa TICS ni mwanzo wa TICS nyingine, kwa Tanzania tegemea yaleyale au zaidi ya yale, God father wa TICS hayupo sasa amelala Lupaso, shamba linawaniwa na wahuni wengine..
Nimemuona Karamagi karudi upya kwenye siasa za CCM....

Huenda ikarudi hiyo hiyo ila kwa mtindo wa Richmond na Dowans
 
Utumwa wa kiakili ni mbaya kuliko ule waliopitia mababu zetu enzi zile. Kweli serikali inashindwa kujipanga na kuendesha kwa ufanisi mradi kama wa Container terminal ambao fedha iko nje nje na wazi
Sijui tutayasema haya hadi lini na wapi, mkuu 'Shehullohi'! Tutaimba sana, na kulia sana, hakuna atakayestuka, hasa hao viongozi wanaonufaika sana kwa kutuuza utumwani.

Umeandika mengi kwenye bandiko hilo, ambayo mengi ninakubaliana nawe, lakini hatuna njia ya kutokea wakati tukiwa chini ya hawa viongozi wanaofaidika na kutuuza utumwani, na wala hawastuki kwa kujua hatuna lolote la kuwafanya.
 
Ni Tawi la Hutchison Port Holdings, hao wakima DP World hawana tofauti.

Bora ajaribiwe APM Terminal, hao watu wa Asia hawajatofautiana sana
Mkuu 'Offshore Seamen', hebu nikuulize wewe, pengine unao ufahamu mzuri zaidi wa haya mambo, hasa nikichukulia jina lako.
Hivi kuna mambo gani magumu sana ambayo waTanzania kwa ujumla wao, kati yao millioni zaidi ya 60 sasa ambayo ni magumu sana kuyafahamu katika uendeshaji wa bandari?
Hapana, kisehemu tu cha makacsha ambacho hawakuweza kujifunza kwa miaka zaidi ya 22 toka kwa hawa wataalam wa TICTS katika muda wote huo?

Zaidi ya miaka 22, tukifanya kazi na hawa TICTS, lakini hatukuweza kabisa kuwa na ujuzi nacho kwamba hawa jamaa watakapoondoka kazi hiyo tutakuwa tayari tunaimudu sisi wenyewe!

Itatusaidia sana sisi wengine tusiokuwa na ujuvi wa eneo hili vizuri, kama utaweza kulizungumzia hili ili nasi tujifunze.
 
Baada ya kuhudumu kwa miaka 22 katika Bandari ya Dar es Salaam, hatimaye ndoa ya kampuni binafsi ya kimataifa ya kuhudumia makontena Tanzania (TICTS) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imekoma rasmi mwaka huu.

Hatua hiyo inakuja baada ya mkataba wa miaka mitano wa wawili hao uliosainiwa Julai 6, 2017 kufikia ukomo Septemba 30, mwaka huu, licha ya kuwepo kipengele cha kuuhuisha, menejimenti ya TPA imetaka kuusitisha.

TICTS imehudumu katika bandari ya Dar es Salaam kwa miaka 22 sasa tangu mwaka 2000 kwa mara ya kwanza iliposaini kutoa huduma ya makontena.

Kulingana na taarifa hiyo ya ndani kutoka menejimenti kwenda kwa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, mkataba kati ya wawili hao uliisha Septemba 30, 2022 na mazungumzo kati ya pande mbili hayakufanikiwa.

Chanzo chetu kilieleza tayari TPA imewasilisha taarifa kwa Bodi ya Wakurugenzi inayoongozwa na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Ernest Mangu kusudio la kutokuendelea na TICTS.

Aidha, TPA inayoongozwa na Plasduce Mbossa imeomba baraka za bodi ili waweze kuiandikia barua kampuni hiyo kutohuisha mkataba huo, na tayari wamejipanga kusimamia wenyewe shughuli zilizokuwa zikifanywa na TICTS.

“Sina shaka hata kidogo kwamba bodi itakubali ombi hili. Na tayari tumejipanga kuhakikisha tunasimamia wenyewe wakati tunatafuta mtu mwingine ambaye atakuwa na uwezo mkubwa zaidi,” alisema kigogo mmoja wa TPA.

Gazeti hili jana kwa nyakati tofauti, lilimtafuta Mbosa kujua wapi hawakuelewana kwenye mazungumzo yao na TICTS, lakini hakupatikana kwani simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita pasina kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe hakuujibu. Jitihada hizo zilifanyika pia kwa kuutafuta uongozi wa TICTS bila mafanikio.

Katika maelezo ya menejimenti ya TPA kwenda kwa bodi yanaeleza kumweka kando TICTS kunalenga mahitaji ya hatua nyingine zinazopaswa kuchukuliwa na uongozi, katika kutekeleza wajibu wake wa kusimamia mkataba ili kulinda masilahi ya mamlaka, Serikali na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo, mtoa taarifa wetu alieleza kabla ya kukamilika kwa mkataba huo Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mei 16, mwaka huu iliunda timu ya wataalamu kujadiliana na TICTS kuhusu kuongeza mkataba na ilihusisha vikao vitatu.

Alisema vikao hivyo viliendelea Septemba 7, mwaka huu kutengeneza njia ya mashauriano zaidi na mamlaka za juu katika maeneo matatu ambayo hawakuwa wamefikia muafaka ambayo ni ukodishaji wa kudumu wa mwaka, ada ya mrabaha ya kila mwezi na upitishaji wa kontena.

Chanzo chetu hicho kiliendelea kueleza kuwa Septemba 23, mwaka huu bodi ya wakurugenzi ya TPA iliridhia ombi la menejimenti la nyongeza ya mkataba wa miezi mitatu kukamilisha makubaliano ambao utaisha Desemba 31.

Hata hivyo, Oktoba 21, mwaka huu TICTS iliwasilisha ombi la kuongeza mkataba ambalo halikufikia viwango vilivyotakiwa na TPA.

“Hatua ya kutohuishwa kwa mkataba huo ni muhimu kwa kuwa menejimenti itapata fursa ya kuendesha gati 8 hadi 11 ambazo zimekuwa chini ya sekta binafsi kwa muda miaka 20, ili kupata mapato yanayotarajiwa kukusanywa,” alisema

Kabla ya uamuzi wa menejimenti wadau walianza kupinga kuendelea kwa mkataba kati ya TICTS na TPA, kwa madai kuwa kampuni hiyo haina utendaji wa kuridhisha.

Julai 23, mwaka huu, msemaji wa sekta ya mawasiliano, teknolojia, habari na uchukuzi wa ACT Wazalendo, Ally Salehe alisema suala la TICTS kukodishwa tena au la, linapaswa kuchukuliwa kwa umakini na kufikiwa uamuzi wenye kujali na kulinda uzalendo.

“Serikali isitishe nyongeza ya mkataba wa kukodisha kitengo cha makasha kati yake na TICTS, kwa kuwa ni wazi imeshindwa kukidhi matarajio ya Serikali yanayolenga kuongeza tija kwenye bandari yetu,” alisema Salehe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…