Miaka mitano ya hayati Magufuli, bei za nafaka hazikupanda namna hii. Sasa zimepanda na wananchi wanakula mlo mmoja na nusu

Miaka mitano ya hayati Magufuli, bei za nafaka hazikupanda namna hii. Sasa zimepanda na wananchi wanakula mlo mmoja na nusu

Boya kabisa, wakulima gani wanapata pesa.......pesa mnapata nyinyi matapeli mnaojiita wafanyabiashara baada ya kuwaibia wakulima kupitia lumbesa, kangomba na kubana mizani, shwaini!
Tikisa kichwa chako pengine huna ubongo. Suala la lumbesa linatoka wapi hapa? Tunaongelea bei kupanda ambapo haimuachi yeyote aliyepo kwenye mnyororo wa thamani.

Lumbesa IPO wakati wote whether bei ziko chini au ziko juu
 
Wakulima ni watu kama wewe hawajatenda kosa lolote mpaka wapewe mzigo wa kukulimia zao upate kwa bei chee bei unazozitaka weee ilhali hujasaidia chochote kwenye kulima kwao
Jibu swali, acha talalila.....
 
Wewe bila Shaka ulikuwa kupe wa wakulima, Hivi wewe kwa ufahamu wako ulitaka wakulima wauze kwa Bei ipi? Unajuwa gharama walizotumia kwenye pembejeo mwaka Jana? Hapo ulipo unaloshamba la mahindi? Unajuwa adha ya kilimo wewe? Unataka Nani akulimie ili wewe ufaidi jasho lake? Kwanini wewe usiende kulima ili uuze kwa Mia tano kilo moja ya unga?

Utakufa na chuki zako kwa mh Rais wetu mpendwa kipenzi Cha watanzania, Sasa wakulima wanafaidika na jasho lao baada ya mh Rais wetu mpendwa kuhakikisha soko la uhakika linakuwepo na mkulima anauza mazao yake kwa Bei nzuri, Bila Shaka ulikuwa ukifurahi kuona wakulima wakipata hasara kila mwaka, utakuwa ulikuwa mnufaika na mnyonyaji wa wakulima, Nenda na wewe ukalimee shambani ili ujuwe uchungu wake
 
Yeye alendesha nchi peke yake? Jama movies za Rambo?
 
N
Huyu dereva nchi imemshinda kabisa.watu wameanza kula mara moja tu kwa siku kutokana na vitu kupanda bei kiholela.Hadi tufike 2025 tutakuwa kila mwananchi amejikondea na kuonesha mbavu zake zote mwili mzima
Nenda shambani ukalime na wewe ili ujuwe uchungu wake, ulitaka ufuahi kuona wakulima wakiuza kwa hasara kila mwaka ili uanze kusema uongo wako hapa, Sasa umeona mh Rais wetu kahakikisha soko la uhakika linapatikana unaanza Tena mdomo mdomo hapa, Nenda kalime na wewe Kama unatakaaa
 
Jana nimenunua sembe kilo 5 shilingi 8,500/= na kuna watu wanashabikia mahindi yaendelee kupelekwa nje.
Kama ni rahisi kalime wewe uwe unatuuzia kilo 5 kwa miasaba, mama usifunge mipaka na sie wakulima tuendelee kulamba asali.
 
Tikisa kichwa chako pengine huna ubongo. Suala la lumbesa linatoka wapi hapa? Tunaongelea bei kupanda ambapo haimuachi yeyote aliyepo kwenye mnyororo wa thamani.

Lumbesa IPO wakati wote whether bei ziko chini au ziko juu
Bei mnapandisha nyinyi madalali na walanguzi wa mazao baada ya kumlalia mkulima kwa kumpa bei ndogo, kubana mizani, lumbesa na kangomba.......halafu mnakuja kulialia hapa JF mkijifanya wakulima, mkulima gani huko kijijini ataingia humu JF, hovyo kabisa.....​
 
Jana nimenunua sembe kilo 5 shilingi 8,500/= na kuna watu wanashabikia mahindi yaendelee kupelekwa nje.
Kutopeleka nafaka nje siyo suluhisho! Suluhisho ni kuboresha sector ya kilimo ili tuzalishe vingi. Mfano unakuta watu wa kanda ya ziwa tunalia ukame!

Kuna wakati mpaka shetani anatushangaa
 
Kama ni rahisi kalime wewe uwe unatuuzia kilo 5 kwa miasaba, mama usifunge mipaka na sie wakulima tuendelee kulamba asali.
Nyinyi ndo mnaibia wakulima kwa kuwalalia bei, kubana mizani, kutumia lumbesa na kangomba halafu mnakuja kulialia humu, hakuna mkulima mwenye mazao kwa sasa serikali ifunge mipaka.
 
Na wewe uwe unaenda kununulia shambani kwani kuna MTU kawazuia kwenda kununua shambani
Kuna mkulima anayeenda kuuza mazao huko nje,
Bei ya shambani bado iko chini Ila inapandishwa na wafanyabiashara
 
Sie hatulii nyie ndo mnaolia, asa na nyie si mkalangue kwa wakulima, mipaka haifungwi na bei hatushushi, mtajua hamjui.
Nyinyi ndo mnaibia wakulima kwa kuwalalia bei, kubana mizani, kutumia lumbesa na kangomba halafu mnakuja kulialia humu, hakuna mkulima mwenye mazao kwa sasa serikali ifunge mipaka.
 
Mpumbavu mkubwa wewe, wakulima wetu ndiyo wakati wao wa kupata fedha na kuboresha maisha yao. Wewe badala ya kwenda kulima mahindi unakuja kuandika pumba JF.

Nenda na wewe ukalime halafu uone uchungu wa kuambiwa usiuze mahindi nje ya nchi.
Ndo hivyo anaye ona anaumia akalimee
 
Kwa STYLE hii tutakula CHENGA kama NJIWA.

Nchi imefunguliwa.
 
Wameuza sana nje mazao wakati ndani chakula hakitoshi eti wapate kupendwa na wafanyabiashara..
Mkuu msimu ujao kodi mashamba mengi ulime uwe unatuuzia kilo moja kwa shingi mia mbili tutakushukuru sana kwa msaada huo.
 
Ni magufulo huyo huyo enzi ya utawala wake watu walipolia bei ya nafaka ipo juu alijibu na kuwaaambia watu basi kama mnaona nafaka ipo juu limeni ya kwenu muuze kwa bei ya chini. Kilimo kinatesa asikwambie mtu. Tunapambana kulima sisi wakulima nina stock ya gunia kama mia moja mahindi afu 50 za mpunga acha tuwale vichwa nyinyi wavivu wa kulima maana kuna kipindi bei inashuka tunauza mahindi hadi elfu 36 gunia.
 
Back
Top Bottom