Miaka mitano ya hayati Magufuli, bei za nafaka hazikupanda namna hii. Sasa zimepanda na wananchi wanakula mlo mmoja na nusu

Miaka mitano ya hayati Magufuli, bei za nafaka hazikupanda namna hii. Sasa zimepanda na wananchi wanakula mlo mmoja na nusu

Ni magufulo huyo huyo enzi ya utawala wake watu walipolia bei ya nafaka ipo juu alijibu na kuwaaambia watu basi kama mnaona nafaka ipo juu limeni ya kwenu muuze kwa bei ya chini. Kilimo kinatesa asikwambie mtu. Tunapambana kulima sisi wakulima nina stock ya gunia kama mia moja mahindi afu 50 za mpunga acha tuwale vichwa nyinyi wavivu wa kulima maana kuna kipindi bei inashuka tunauza mahindi hadi elfu 36 gunia.
Mahindi zamani yalishuka bei huko Ruvuma, Sumbawanga, Katavi mpaka Gunia la debe 7 lilikuwa 18000-30000 na hapo hakuna mnunuzi.


Ila mwaka huu mvua chache sana na mbolea bei juu. Wengine hata hawajavuna kabisa na wamepata hasara.
 
Nikiwa mkulima nafuraia ongezeko hili,bado Bei hailingani na gharama za uzalishaji.mipaka iendekee kuwa wazi Asante waziri wa kilimo kwa kumshauri mh Rais.
Naomba uje tunduru Mtatiro & Co anawatia hasara kwenye mbaazi kupitia stakabadhi ghalani Ni wizi.
Ongezeko la Bei ya nafaka litashawishi vijana wengi kuingia kwenye kilimo.huduma zenu wasomi ziko juu na wakulima siku zote huvumlia bila malalamiko.bei panda mkulima apate pembejeo
 
Mapori yapo mengi nchi hii nendeni mkalime. Wakulima ni wakati wao nao kupumua. Mnakaa mnabeti tu mjini huko halafu mnataka tuwalimie mle Bure.....
 
Linaloshindikana kwa mwanadamu kwa AK 47 halishindikani
 
Na bado watu wanaambiwa wauze nje ya nchi wanavyojisikia.

Hapa tunakaribisha njaa.
 
Mchele 1kg 3,000 super kyela nilikua nanunua 2,000 haya maisha sio poa[emoji23][emoji23][emoji1373][emoji1373]
 
Jana nimenunua sembe kilo 5 shilingi 8,500/= na kuna watu wanashabikia mahindi yaendelee kupelekwa nje.

Hao wanaoshadadia ni watoto wa mama anamka asbh anakuta chai mezani akitoka anarudi seblen kucheki movie mchana anawekea chakula dining ale. Watoto mchelemchele hajui hata bei ya sukari lazima ashibikie mahindi na mchele kuuzwa nje[emoji23][emoji23].

Jana nilikua Nyuki sokoni pale kununua lishe ya mtoto na baadhi ya mahitaji kweli hali mbaya

Mahindi ya njano 1kg 1,800
Mbegu za maboga 1kg. 10,000
Ufuta. 1kg. 5,000
Ngano 1kg 2,600
Soya. 1kg. 4,000
Karanga nyeupe kg 4000
Ulezi kg 2,600

Imenitoka 19,000 kununua hivo vitu kwa ajili ya lishe zamani ilikua haizid 10,000.

Uje kwenye mchele sasa ili upate mchele mzr ambao angalau ukila usikie ladha 2,700-3,200 kwa kilo[emoji23][emoji23][emoji23].

Dagaa wa bukoba wale ambao hawana mchanga nilikua nanunua kg kwa 8,000 now ni 12,000.

Sato kilo 14,000. Maisha yamekua juu sana aisee
 
Back
Top Bottom