Joshua Mollel: Mtanzania wa pili kuuawa aliyetekwa na Hamas
BBC Swahili, Nairobi
CHANZO CHA PICHA,JOSHUA MOLLEL
Maelezo ya picha,
Joshua Mollel aliwasili Israel mwezi mmoja tu kabla ya shambulio la Hamas
Serikali ya Tanzania imethibitisha kupokea taarifa kutoka serikali ya Israel kuhusu kifo cha mwanafunzi Joshua Mollel aliyekuwa anasoma nchini Israel na aliyetekwa nyara tarehe 7 Oktoba 2023 wakati kundi la Hamas liliposhambulia Israel.
Kupitia ujumbe wa X iliyojulikana kama Twitter hapo awali,Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania January Makamba amesema ameongea na baba ya marehemu Joshua, Mzee Mollel kuhusu ujumbe huo