Hatimaye leo kanjibai amekaa, Baada ya kugongesha miamba mara nne (kwa timu moja kuchana mkeka) ndani ya wiki moja. Hatimaye leo kanjibai nimemuingiza katika 18
View attachment 186896
Mkuu andybird314, Mimi baada ya kupopolewa sana na kanjibai nilikaa nikajiuliza napopolewa wapi na kwa nini ninapopolewa. Baada ya kujitathmini sana nikagundua vitu vifuuatavyo ndivyo vinanichanisha mkeka
1. Kutegemea mkeka wa timu nyingi
2. Kurudiarudia timu kwenye mikeka tofauti.
3. Kubet kwa mazoea na kutoangalia upepo wako upo wapi siku hiyo. Hapa utakuta mtu anabet matokeo ya mwisho wakati dhahiri matokeo ya mwisho yanaonekana kuwa magumu na say labda idadi ya magoli inayoonekana rahisi yeye haibetii. Kumbuka hii ni biashara, Biashara siku zote muuzaji huleta kitu wanachotaka wateja na sio kile akipendacho yeye(siyo kwa kuwa wewe ni mpenzi wa colgate basi unajaza colgate tuu dukani, wakati wateja wanataka whitedent, Usipoangalia colgate zako zitakudodea na mwishowe kupata hasara).
4. Pia Inatakiwa uwe versatile na ukae kibiashara zaidi (inataakiwa upige miguu yote). kuna michezo ni rahisi sana kupiga pesa apart from football. Mimi kwangu michezo myepesi kupiga pesa football nauweka namba nne kwa mtiririko huu 1. Basketball, 2. Baseball 3. Tenis na wa nne ndio football. Katika michezo say basket, ukiwa makini unapiga pesa mpaka basi hususani katika option ya Live betting.
5. Nilikuwa sichezi live betting. Ila baada ya kuichukulia betting kama ajira yangu ya pili, Imebidi nicheze online live betting. Na kulifanikisha hili na kuwa serious na biashara zaidi Nimenunua na kujiunga na kifurushi cha mwezi cha GB 41 (thanks to Airtel kwa 3.75 G yao ya ukweli na bundle za bei rahisi, Kitu muda wote kinasoma H+), Maana masuala ya kuishiwa vocha/data bundle yanaweza kukukosesha pesa kwani within fraction of second kama unacheza online unaweza kuta odds haziko upande wako ukoweka mzigo. hivyo kuulinda mtaji unatakiwa urudishe mpira kwa kipa sometimes kwa kugenerate ticket ambayo inajicancel na ile ya kwanza.
6. Watu wanabet pasipo kufanya research ya kutosha juu ya timu wanazobetia.
Thanks kwa Biohazard na trick yake ya timu moja mkeka mmoja. Hii inafaa sana, na ameniongezea kitu kipya. One love.
Naomba niseme kwamba wiki hii ni wiiki ya faida kwangu, Kwa wiki hii pekee nimetengeneza Net profit ya takriban shilingi Laki tano za kitanzania. Safari yangu ilianza na elfu kumi siku ya champions league. Muhindi anaichukulia hii kama biashara yake, Lakini nimegundua sisi tunaiichukulia poa. Natumai haya tukiyazingatia tutampiga Kanjibai.