Hakuna Dikteta yeyote aliye hapa jukwaani tupo humu kwa nia moja na sio ya kuizungumzia kila mmoja anajua tupo kwenye hili jukwaa kwa madhumuni gani, vita yetu haituhusu sisi bali vita yetu tunaipeleka kwenye betting wote tunashambulia kwa mbinu mbalimbali ili tu tupate ushindi, sasa ikitokea leo hii tunakwaruzana sisi kwa sisi ni sawa na kumsaidia adui ambaye tunapambana nae.
Kila mtu ana haki ya kutumia hili jukwaa atakavyo ni kweli hata akiweka mikeka ya 1970 ni haki yake aiweke ila kwetu sisi hiyo mikeka haina maana tena kwetu safari yetu iko mbele sio nyuma, huu ni unafiki ambao bila kuusema utazidi kuwa juu leo hii kuna watu hapa wanategemea watu ili wapate Odds waweke mikeka na wanakuwa na mara nyingine hawaamini katika maamuzi yao kwani sio wote hapa wanaweza kuchambua timu na kuweka pesa sasa watu hao wenye shauku ya ushindi ukiwaletea vipeperushi vyako ambavyo umeshinda utazidi kuwachanganya "bora uweke kabla ya mechi ili ikitokea amefata bahati yako basi iwe kheri kwake ila kuvileta baada ya mechi ile hali mwanzoni hujuviweka ni sawa na unafiki"
Nakumbuka kuna mdau wetu mmoja majuzi kashinda mikeka 3 mfululizo ila hakuiweka hapa kabla ya mpambano aliiweka baada ya kushinda watu waliruka na kusema dhima ya jukwaa ni ushirikiano katika kuhakikisha kila mmoja hapa anapata mwanga kwa wale wasio na mwanga, hapa kuna watu ni wageni hawajui 1.5 over wala 0.5 over watajua vipi kama kila mmoja wetu ataanza kuweka hapa win ticket badala ya kuweka mkeka ili na wao wajifunze kupitia wewe.
Sina wivu na mtu wala kinyongo na mtu ila nakumbuka msemo mmoja wa Kiswahili unasema "Maskini akipata basi matako hulia Mbwata", lazima masikini watapata na matako yao yatalia mbwata kwa kelele za ajabu ila kabla ya kelele unakuta wametulia kimya.
Heko kwa wale wote ambao wanashiriki kuweka hapa mikeka yao ambayo i hai P didy, Koncho hawa wakiwa miongoni mwa wanajukwaa hili ambao wanafurahia maendeleo yao na yetu sote.
Bet Kistaarabu hii ni ajira kwa baadhi ya watu tusiwavuruge.
Kumbe unafahamu kuwa kuna vingi vya kushea siyo tu hiyo mikeka ambayo mtu tayari ameshaisuka kwa akili yake mwenyewe na experience zake kisha anaiweka hapa. Kuna vingi sana vya kushea humu zaidi hata ya hicho kimoja. Hapa watu ndio wanatakiwa waone mikeka kabla ya mechi kuchezwa ili kama ni kufuata wafuate na ndio mana huwa tunasema
"We live together or we die together".... Lakini mimi nadhani kikubwa kuliko hicho ni kumsaidia mtu aweze kuuelewa huu mchezo vizuri ili mwisho wa siku hata kama wewe haupo, Pdidy hayupo, Buddy, Koncho77 au nyegere hawapo huyu mtu asishindwe kusuka mkeka akiwa peke yake.
Kumbuka kwenye betting kuna experience tofauti tofauti, mfano mimi inawezekana kabisa timu flani flani zikawa zinanikataa na kila nikiziweka kwenye mkeka basi automatically na loose lakini kwa mwingine timu hizo zikawa hazimwangushi hata kidogo, hivyo hata kama yeye atashea huo mkeka wake automatically mimi sitautumia. Na usije kusahau pia huu mchezo/kazi japokuwa tunasema haina kanuni lakini huwezi amini kila mtu kuna vitu aki-violate tu lazima ataloose sasa experience kama hizi wakati mwingine ni bora mtu akajitengenezea tu hata kama atakuta mkeka humu akafanya
kuchanganya na akili zake kama Kikwete alivyosema.
Tunapeana guidelines kama ligi gani zina magoli mengi, zipi hazitoi magoli. Ligi gani zinatoa gg kwa wingi zipi hazitoi, Timu gani hazitabiriki zipi zanaeleweka n.k......tunaelekezana namna ya kuregester kampuni flani, kampuni ipi inafaa ipi haifai. Tusolve vipi matatizo tunayokutana nayo kwenye betting nakadhalika. Hivi ni vichache miongoni mwa vingi tunavyoshea kwenye hili jukwaa letu pendwa zaidi ya hiyo mikeka iliyotafunwa ambayo unaililia Kutwa hapa.
Nasema hivi, tokea ulipoanza kuleta dukuduku lako just from the first time tubumeonyesha wewe sio mstaarabu na huna awareness ya kufikisha jambo kwa ajili ya kupata suluhisho. Kama nakumbuka vizuri naweza kukuquote, ulisema "wakishinda vi 3000 vyao ndo wanapost humu".... Dah hii ni Akili mbovu kabisa kuwahi kushuhudia toka kwa mtu wa jukwaa hili toka nimejiunga humu!
Kwani wewe huwa unashinda millions ngapi ngapi mkuu mpaka udharau vi 3000 alivoshinda mwenzako?. Lakini hata kama ungekuwa unashinda hizo milioni milioni zako mimi nakuapia hata kidogo nisingeumia kwa kuwa umeingiza pesa ambayo inaweza kukusaidia maishani mwako ikakutoa kwenye hatua moja hadi nyingine ya mafanikio. Lakini hata kama ungekuwa umesinda 100 (mia) nisingeidharau kwa kuwa umeingiza pia maana hata milioni huanza na moja. Pamoja na yote hata ungeloose nisingekuona fala kwa kuwa najua ni bahati mbaya imemkuta mpambanaji, wakati mwingine ni lazima tukubali.
Kwa ulichokifanya wewe, kitendo cha kuonyesha dharau tu imeonyesha kuwa wewe huna nia ya dhati kwa wenzako hata kama unashea kila siku asubuhi, mchana, jioni na usiku mikeka yako humu..... Stupid!
Nasema hivi yote na yote huwezi kupose sheria yoyote humu jukwaani. Nimekereka sana na tabia ya ajabu uliyoionyesha kwa kisingizio cha kukosoa ambacho hukupenda.
Anyway, sitaki kusema sana. Humu jukwaani kuna watu nawarespect sana kwa niaba ya legacy yao na Mapambano yao wanayoyafanya sitaki kuwa nje ya dhamira. Acha niishie hapa huwa sipendi sana kuague na mtu especially kwenye suala ambalo halina msingi lakini kwa kuwa niliona imekuwa too much nikasema "sitokaa kimya"
Naomba niishie hapa kwa niaba ya wote humu, peace, love & consciousness be spread.