camerlengo
JF-Expert Member
- Jun 28, 2025
- 1,034
- 1,002
Kwa mantiki hiyo hata wabudha nao ni waislam!Na kwa ushahidi wa Kiakiolojia ni Maandishi ya Kiarabu ya kale (pre-Islamic inscriptions) kama yale ya (Qaryat al-Faw) na (Najran) yanaonyesha baadhi ya watu waliamini Mungu mmoja.
(Inskripsheni ya Umm al-Jimal) (Jordan) ya karne ya 5–6 BK inaonesha matumizi ya neno (Allah) kabla ya Muhammadi.
Na Maandiko ya Nabataean (karibu Petra) pia yanaonyesha imani za karibu na tauhidi kabla ya Muhammadi kuja rasmi.
Ushahidi wa simulizi huru Wanahistoria wa Kirumi na Wagiriki kama (Pliny the Elder na Diodorus Siculus) walirekodi kuwapo kwa watu wa jangwani waliokuwa na maisha ya kiroho yenye kanuni kali.
(Monotheistic sects) kama "Ebionites, Essenes" na baadhi ya "Nazarenes" waliamini nabii atakayekuja na walikataa Utatu ni sawa na mtazamo wa Kiislamu.
Kwa Maneno ya wanahistoria wa kimagharibi
Baadhi ya watafiti, kama "Montgomery Watt" "Karen Armstrong"na "John Esposito" wameandika kwamba Uislamu haukuanzishwa upya bali uliendeleza ujumbe wa dini ya Ibrahim.
Uislamu ni mfumo wa kumwamini Mungu mmoja kuishi kwa maadili na kumuabudu Muumba Uislamu una historia ndefu inayorudi nyuma kabla ya Mtume Muhammad (SAW) Uislamu wa sasa ni kilele cha muendelezo wa dini ya mitume.
Wenye babu yao Ibrahim mayahudi hadi leo wanaamini katika Mungu mmoja nao ni waislam?
Hebu kuwa serious basi Mkuu.
Kwani hujui kuwa uislam ni sawa na Kiswahili ambacho kimekopa maneno kutoka lugha mbalimbali (Lahaja)?
Uislam ni muunganiko wa practizes za mayahudi,wakatoliki,makureshi na didi mbalimbali zilizokuwa zikiabudiwa pale Meccah yaani kwa ufupi ni CHAUMA ya wakatoliki chini ya Khadijah,Bahirah na Waraqah!
Unajua aliyemtabiria unabii Mwamedi alikuwa dini gani?
Aliyemwambia mtume kuwa kile kiumbe kilichomkaba pangoni kuwa ni Gibril alikuwa dini gani?
Za kuambiwa changanya na zqko basi!