Milo mitatu kama hufanyi kazi ngumu ni tamaa na ulafi tu

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Kwanza tufahamu utaratibu wa milo mitatu(breakfast, lunch na dinner) ni utamaduni wa magharibi ulioibuka karne ya 17 kutokana na mambo mengi mojawapo ikiwa ni mapinduzi ya viwanda yaliyowafanya wafanyakazi wanaofanya kazi ngumu wahitaji kula mara nyingi kuhimili kazi ngumu. Kabla ya hapo binadamu wengi walikuwa wanakula mlo mmoja au miwili kwa siku.

Kwa upande wa daraja tawala na mabepari huko magharibi wao baada ya mafanikio ya kiuchumi walianza kula milo mitatu kama anasa na kufanya networking, baadaye karne ya 19 huko Marekani suala la breakfast(kifungua kinywa) liligeuzwa biashara zaidi baada ya jamaa mmoja kusahau kubeba mahindi yake aliyochemsha kula kazini na yakaharibika ndipo likamjia wazo la kutengeneza cornflakes kwa kuyakandamiza kama chapati na kuyaanika kuyafanya yadumu zaidi, ndipo wazungu wakaibuka na bidhaa chungunzima za breakfast.

Leo hii mtu anakula asubuhi na mchana anashinda dukani, saloon au ofisini anabonyeza keyboard tu ndio mwanzo wa janga la kiribatumbo na vitambi kwa wanawake na wanaume.
 
Kwanza tufahamu utaratibu wa milo mitatu ni utamaduni wa magharibi ulioibuka karne ya 17 kutokana na mambo mengi mojawapo ikiwa ni mapinduzi ya viwanda yaliyowafanya wafanyakazi wanaofanya kazi ngumu wahitaji kula mara nyingi kuhimili kazi ngumu. Kabla ya hapo binadamu wengi walikuwa wanakula mlo mmoja au miwili kwa siku.

Sio lazima mitatu hata SITA kula,Ni wewe tuu na tumbo lako!
 
Acha watu wale mkuu milo hata 6 sema wale kwa kiasi.

Mfano asubuhi mayai 2 ya kukaanga na chai, mchana kaugali ama ka wali kadogo na maharage, mboga mboga, protini kwa sana kisha jioni ka wanga kadogo na protini kwa sana kuna ubaya gani?

Shauri watu waachane na ma junk food kama soda, chips, mijuisi ya azamu, energy drinks na mabia yasiyo na maana.

Ukila kwa adabu na kula msosi sahihi hata ukila masaa 12 kwa siku hakuna madhara.
 
breakfast within 2 hours of rising with focus on lean protein and low-sugar fruit;
lunch: midday paying attention to lean protein + complex carbs;
dinner before 8 pm with focus on fiber + low saturated fat;
and snacks focusing on high fiber + lean protein.
 
Kiongozi una hoja
sio huyo limbukeni mleta mada amekuja hapa kukashfu watu wakati hana elimu yoyote ya namna ya kula (diet)
 
Watu wengi hawajawahi ku experience njaa, Njaa wanazosisema ni hizi ambazo imetokea kuvurugika tu kwa ratiba ya Milo yao mfano mtu mwenye ratiba ya kula Milo mitatu ndani ya mda Fulani ikitokea amechelewa kula ndani ya mda huo atakwambia anahisi njaa ila njaa, njaa kweli ni Ile ambayo mtu anatoboa kuanzia masaa 12 na kuendelea bila kula chochote
 
Sahihi, mazoea yamewaharibu watu wengi katika ulaji, mtu anakula kwa sababu ni ratiba tu kula hata kama hana njaa kiuhalisia.
 
Janabi alishasema unatakiwa ule pale unapohisi njaa tu siyo unakunywa chai kwasababu ni Asubuhi kama hauhisi njaa skip breakfast kula hata saa 6 mchana ikifika muda wa lunch huskii njaa skip had saa 11 jion ndo ule, usiku siyo muhimu sana kula kama unataka kula usiku basi kula masaa matatu kabla ya kulala
 
Kwanza tufahamu utaratibu wa milo mitatu ni utamaduni wa magharibi ulioibuka karne ya 17 kutokana na mambo mengi mojawapo ikiwa ni mapinduzi ya viwanda yaliyowafanya wafanyakazi wanaofanya kazi ngumu wahitaji kula mara nyingi kuhimili kazi ngumu. Kabla ya hapo binadamu wengi walikuwa wanakula mlo mmoja au miwili kwa siku.

Kwa upande wa daraja tawala na mabepari huko magharibi wao baada ya mafanikio ya kiuchumi walianza kula milo mitatu kama anasa na kufanya networking, baadaye karne ya 19 huko Marekani suala la breakfast(kifungua kinywa) liligeuzwa biashara zaidi baada ya jamaa mmoja kusahau kubeba mahindi yake aliyochemsha kula kazini na yakaharibika ndipo likamjia wazo la kutengeneza cornflakes kwa kuyakandamiza kama chapati na kuyaanika kuyafanya yadumu zaidi, ndipo wazungu wakaibuka na bidhaa chungunzima za breakfast.

Leo hii mtu anakula asubuhi na mchana anashinda dukani, saloon au ofisini anabonyeza keyboard tu ndio mwanzo wa janga la kiribatumbo na vitambi kwa wanawake na wanaume.
HATA CHAI ASUBUIHI NI KUIGA NCHI ZA BARIDI ...KULE UKIENDA NDIYO UTAJUA KUWA WAAFRICA TUNAIGA TU KUNYWA CHAI MAANA KULE BARIDI NI KALI SANA HIVYO UMUHIMU WA CHAI NI DHAHILI...KWA HAPA TANZANIA MIKOA YENYE BARIDI KAMA NJOMBE NA MBEYA NK NDIYO WALITAKIWA KUNYWA CHAI ILA KAMA HAPA DAR KWA JOTO TULILO NALO CHAI NI KUJITIA UVIVU TU
 
Watu wengi hawajawahi ku experience njaa, Njaa wanazosisema ni hizi ambazo imetokea kuvurugika tu kwa ratiba ya Milo yao mfano mtu mwenye ratiba ya kula Milo mitatu ndani ya mda Fulani ikitokea amechelewa kula ndani ya mda huo atakwambia anahisi njaa ila njaa, njaa kweli ni Ile ambayo mtu anatoboa kuanzia masaa 12 na kuendelea bila kula chochote
Acha kabisa, msosi ni muhimu jombaa.

Kuna kipindi nikipitia msoto mpaka kwenda toi ukibanwa na gogo unaogopa, maana unaenda kutoa nini huku na hujala chochote cha maana, nikitoa hiki si ndo tumbo litabaki tupu kabisa.

Hapo umechapa uji tu maana unga hata ugali hautoshi.
 
Kwahiyo unashaurije?

Mlo gani ufutwe?

Je ni tabia mbaya kula mara tatu ?

Tulitegemea wataalamu wa lishe ndo wawe wa kwanza kukemea hili anyway.

Kabla ya mapinduzi ya viwanda watu walilima kwa jembe la mkono, unaweza kututhibitishia kuwa kazi za viwandani ni ngumu kuliko kulima kwa mkono?
 
Back
Top Bottom